image

HUKUMU ZA KUSOMA QURAN, HUKUMU ZA TAJWID, HUKUMU ZA NUN SAKINA, MIM SAKINA, QLQALA NA IQLAB, TANWIN NA MADA

HUKUMU ZA KUSOMA QURAN, HUKUMU ZA TAJWID, HUKUMU ZA NUN SAKINA, MIM SAKINA, QLQALA NA IQLAB, TANWIN NA MADA

Darsa za Quran

Ustadh Rajabu

DARSA ZA TAJWID

TAJWEED.
UTANGULIZI
Neno ‘Tajwiyd ’ linatoka na neno جَ و د (jawwada) kilugha ina maana ‘ufundi’,
yaani kufanya kitu kwa uhodari au ustadi.
Maana yake Kishariy’ah:
Kuitamka kila herufi kama inavyotakiwa kutamkwa, kwa kuipa haki yake
na swiffah zake huku ukifuata hukmu zote za Tajwiyd.Katika qurani na sunnah imehimizwa sana kusoma qurani kwa tajwid au tartila. Elimu hii ya tajwid imeanza zamani toka enzi za masahaba na toka mtume yupo hai. Pia alikuwa Mtume akiwaelekeza masahaba kwa watu maalumu ili wapate kujifunza qurani kiufasaha. Imepokewa kuwa Mtume (s.a.w) amesema: ((Mwenye kupenda kuisoma Qur-aan kama vile ilivyoteremshwa basi na asome kwa Qiraa-ah [kisomo] cha ibn Ummi ‘Abd)) (amepokea Ibn Majah na ahmad)Pia Allah amesema :وَرَتِّلِ ٱلْقُرْءَانَ تَرْتِيلً “na soma Qur-aan kwa tartiylaa (kisomo cha utaratibu upasao” Katika kuonesha maana ya neno tartiyla ‘Aly Ibn Abi Talib ambaye ni khalifa wa nne baada ya kufariki mtume amesema: التَّتيلُ هُوَ تَجيد الحْوفَ ومَ عْ رِفةِ الوقوفِ “Ni kuisoma Qur-aan kwa ujuzi wa kutamka herufi ipasavyo na kuwa na ujuzi wa hukmu za kusimama”Hukumu ya kujifunza tajwid:
Kusoma qurani bila ya tajwid yaani kuchunga herufi ni katika makosa mbele ya maulamaa wa tajwid. Maulamaa wa elimu hii wanazungumza kuwa kujifunza tajwid ni faradh al-kifaya kwa kauli za walio wengi. Pia wapo wanaosema ni faradh ‘ayn yaani ni faradhi ya lazima kwa kila muislamu.Hawa waliosema ni faradhi kifaya yaani sio faradhi ya lazima kwa wote ila inatosha kwa wachache wakiwa na elimu hii, kundi hili pia linazungumza kuwa inapasa kwa msomaji asisome kwa kukosea ijapokuwa hajui hukumu za tajwiid. Yaani achunge matamchi kama yalivyoandikwa asije akatamka vinginevyo na kubadilisha maana.Aina za usomaji wa qurani:
Wataalamu wa elimu ya tajweed wamegawa aina za usomaji katika makundi makuu yafuatayo;-1.At-Tahqiyq huu ni usomaji wa taratibu kwa kuzingatia hukumu za tajwid na kuzingatia maana. Msomaji atasimama panapotakiwa na atapumzika panapotakiwa. Kila herufi itapewa haki yake kulingana na inavyotamkwa. 2.3.Al-Hadr huu ni usomaji wa haraka kwa kuzingatia hukumu za tajwid. Hapa msomaji atazingatia hukumu zote na anatakiwa awe makini katika kufanya ghunnah. Hapa msomaji anaweza kuvuta kwa kiwango cha chini mada. Yaani kama mada ina haraka 2 mpaka sita anaweza kuishia kwenye mbili.3.At-Tadwiyr hapa msomaji atasoma qurani kati ya usomaji wa aina mbili tulizozitaja hapo juu. Na huu ndio uso wa kawaida na wengi wa watu watu wanautumia.Viraa saba na herufi saba.
Wataalamu wa tajwid wanaeleza kuhusu herufi saba za usomaji wa qurani. Itambulike kuwa qurani imeshuka kwa lugha ya kiarabu. Na pia itambulike kuwa waarabu wenyewe walitofautiana katika lahaja za lugha ya kiarabu. Lahaja hizi zilikuwa katika makabila saba ya kiarabu yaliyopo maka. Yaani ni kuwa waarabu walikuwa na makabila saba wakati ule. Na makabila haya ijapokuwa yalizungumza kiarabu lakini walikuwa wakitofautiana katika maneno, utamkaji na hata uandishi. Hivyo lahaja hizi zilijulikana kama herufi saba (za usomaji wa qurani).Hivyo lahaja saba hizi ndizo chanzo za hizi herufi saba. Na hili linathibitika katika maneno ya Mtume (s.a.w) aliposema: ((Jibriyl alinisomea kwa herufi moja, nikaifanyia marudio mpaka akanifundisha nyingine, nikaendelea kumuomba nyinginezo mpaka mwishowe zikawa herufi (lahaja) saba)) (Bukhari na Ahmad).Makabila haya yalikuwa Quraysh, Hudhayl, Thaqiyf, Hawaazin, Kinaanah, Tamiym na Yeman. Hivyo qurani ilishuka katika lahaja saba kulingana na makabila. Hivyo ikawa kila kabila linasoma qurani kwa namna ambavyo lahaja yao inawafanya waelewe. Wakawa watu wanaandika qurani kwa namna ambavyo wanaelewa wao. Kulingana na lahaja ya kabila lao. Hali hii ilifanya usomaji wa qurani utofautiaane.Amesimulia ‘Umar Ibn Al-khatab kuwa: “Nilimsikia Hishaam ibn Hakiym akisoma Suwratul-Furqaan tofuati na vile ninavyoisoma na alivyonifundisha Mtume ( لى لله عليه وسلم B). Nilikaribia kumsimamisha (asiswalishe) lakini nikamvumilia mpaka akamaliza kisha nikamshika nguo yake shingoni na kumvuta mpaka kwa Mtume لى لله عليه وسلم) B) nikasema: “Nimesikia huyu mtu akisoma (Suwratul- Furqaan) kinyume na ulivyonifundisha”. Mtume ( لى لله عليه وسلم B) akasema: ((Mwachie!)) Akamwambia (Hishaam): ((Soma)). Akasoma. Akasema ((Hivi ndivyo ilivyoteremshwa)). Kisha akaniambia mimi: ((Soma)). Nikasoma. Akasema: ((Hivi ndivyo ilivyoteremshwa. Hakika Qur-aan imeteremshwa kwa herufi saba, hivyo someni iliyokuwa sahali kwenu)Uislamu ulipoenea zaidi ikawepo haja ya kuiandika qurani katika lahaja moja ambayo itasomwa. Na hii ni kutokana na kuwepo makosa katika usomaji wa qurani. Hivyo katika utawala Kikundi cha Maswahaba, kilichoongozwa na Hudhayfah bin al-Yamaaniy ambaye alikuwa Iraq, kilikuja kwa ‘Uthmaan ( رضي لله عنه ) na wakamsihi "auokoe ummah wa Kiislamu kabla haujatofautiana juu ya Quraan." ‘Uthmaan ( رضي لله عنه ) akaamrisha chini ya uongozi wa Zayd bin Thaabit رضي لله عنه) ) nakala za Qur-aan ziandikwe na nakala zote zisizo rasmi zichomwe moto.Lahaja iliyotumika kuandika Qur-aan ni ile ya ki-Quraysh na Msahafu ukajulikana kuwa ni ‘Msahafu wa ‘Uthmaan’. Nakala hizo zilisambazwa miji mikuu ya Waislamu zikiwa kama nuskhah (kopi) rasmi. Na nuskhah ya asili ikabakishwa kwa Mama wa Waumini Hafswah ( رضي لله عنها ). Alimwacha Zayd bin Thaabit Madiynah, ‘Abdullaah bin Swaa’ib alitumwa Makkah,Mughiyrah bin Shu’bah alitumwa Syria, Abu ‘Abdir-Rahmaan As-Sulamy alitumwa Kuwfah, ‘Aamir bin ‘Abdil-Qays alitumwa Baswrah. (www.al-hidaayah.com)Baada ya msahafu huu kusambazwa katika dola ya kiislamu lahaja zote ambazo siorasmi zilipotea. Msahafu huu ndio chimbuko la misahafu tulionayo leo. Ijapokuwa kuna tofauti kubwa za kiuandishi kati ya misahafu ya leo na msahafu huu. Kwa m fano msahafu huu haukuwa na dot kwenye herufi za dot au irabu pia hazikuwepo. Hayo yato yalifanyika baadaye kadiri uislamu ulipoenea maeneo mbalimbali ya dunia na ikaonekana ugumu wa kutumia msahafu ule kwa watu wasiokuwa waarabu.Viraa saba.
Viraa hivi saba ndivyo ambavyo vimetokana na lahaja ya kikurayshi ambayo ndio msahafu wa ‘Uthmani umeandikiwa. Viraa hivi wataalamu wa elimu ya tajwid wamevizungumzia katika vitabu vya elimu hii.Fadhila na umuhimu wa tajwid.
Kwa hakika tunatambuwa sasa kuwa elimu ya tajwid ina umuhimu mkubwa kwenye umma wetu wa kiislamu. Kwani msomaji kama hatachunga kisomo anaweza kubadilisha maana ya qurani kabisa. Hivyo elimu ya tajwid inaweza kuwa ni msingi wa kuchunga maana ya matamshi ya qurani katika usomaji.Tunahitajia imamu mwenye kiraa kizuri kwa sauti pia awe anajuwa tajwid na anaitumia ipasavyo. Amesema Mtume (s.a.w): Kutoka kwa Abu Mas’uud Al-Answaariyy ( رضي لله عنه ) amesema: Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) amesema: ((Awaswalishe watu yule mwenye kujua kusoma zaidi Kitabu cha Allaah na wakiwa katika kusoma wako sawa, basi mwenye ujuzi zaidi wa Sunnah, na wakiwa kwenye Sunnah wako sawa, basi aliyetangulia Hijrah, na wakiwa katika hijrah wako sawa, basi mkubwa wao kwa umri, wala asiswalishe mtu (mwengine) katika nyumba yake wala katika mamlaka yake wala asikae mahali pake pa heshima isipokuwa kwa idhini yake))Halikadhalika watu hupenda kusikiliza kiraa cha mtu anayesoma vizuri kwa sauti na kuchunga hukumu za tajwid. Na hivi pia ndivyo Mtume (s.a.w0 anvyotuambia:Kutoka kwa Abu Muwsaa Al-’Ash’arriy ( رضي لله عنه ) kwamba Mtume kamwambia: ((Ungeliniona jana nilivyokuwa nakusikiliza kisomo chako. Hakika umepewea mizumari miongoni mwa mizumari ya aila ya (Daawuwd)Msomaji wa qurani atakukuwa pamoja na malika wema wenye kuandika. Imetoka kwa ‘Aaishah ( رضي لله عنها ) kwamba Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) amesema: ((Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi [wa Allaah] watukufu wema, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili)).

Kupata muendelezo wa Darsa hizi pamoja na mifani na hukumu za tajwid Pata kitabu chetu hapo chini
bofya hapa Kuendelea na somo hili
ama download kitabu cha tajwidBofya hapa           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1057


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-