image

Historia ya kuhifadhiwa na kuandikwa kwa quran toka wakati wa Mtume (s.a.w)

Historia ya kuhifadhiwa na kuandikwa kwa quran toka wakati wa Mtume (s.a.w)

Kuhifadhiwa kwa Qur-an



Tofauti na vitabu vingine vya Allah (s.w) vilivyotangulia, Qur-an ina ahadi ya Allah (s.w) ya kuhifadhiwa kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


"Hakika sisi ndio tulioteremsha mawaidha haya (hii Qur-an) na hakika sisi ndio tutakaoyalinda". (15:9)


"Haitakifikia batili mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye Hikima ahimidiwaye." (41:42)
Kutokana na aya hizi, Qur-an iko vile vile kama ilivyoteremshwa na haijabadilika hata kidogo. Kila aya zilivyoshuka zilihifadhiwa kwa njia tatu zifuatazo:



Kwanza, alihifadhishwa Mtume (s.a.w) na kuahidiwa na Mola wake kuwa hatasahau kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



"Tutakusomesha wala hutasahau ila akipenda Mwenyezi Mungu. Yeye anajua yaliyodhahiri na yaliyofichikana." (87:6-7)


"Usitikise ulimi wako kwa (kuufanyia haraka) wahyi. Kwa hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. Wakati tunapokusomea basi fuata kusomwa kwake. Kisha ni juu yetu kuubainisha." (75:16-1 9)



Pili, Waislamu walihifadhi Qur-an vifuani mwao baada ya kusomewa na Mtume (s.a.w).



Tatu, Qur-an ilihifadhiwa katika maandishi chini ya usimamizi wa Mtume (s.a.w) mwenyewe. Kila aya ya Qur-an iliposhuka iliandikwa wakati ule ule katika karatasi maalumu za ngozi (Qur-an 52:3) na waandishi wa Mtume (s.a.w) chini ya uangalizi na usimamizi wake kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:



Uthman bin Afan (r.a) amesimulia: "Wakati wowote Mtume wa Allah alipoteremshiwa wahyi humuita mmoja wa watu waliochaguliwa kuandika." (Tirmidh)



Naye Zaid bin Thabit mmoja wa waandishi wa Qur-an anasema: "Nilikuwa jirani na Mtume wa Allah, kwa hiyo kila alipoteremshiwa wahyi ilikuwa kawaida yake kuniita nami niliandika aliyoniamuru." (Abu Daud)


Idadi ya waandishi wa Qur-an aliowateua Mtume (s.a.w) ilifikia hadi 42. Miongoni mwa waandishi wa Mtume (s.a.w) ni pamoja na Makhalifa wake wanne - Abu bakr, Umar, 'Uthman na Ally (r.a). Waandishi wengine waliokuwa mashuhuri ni Zaid bin Thabit, Abdullah bin Mas-'ud, Ubayyi bin Ka'ab, na Khalid bin Walid.



Mtume (s.a.w) baada ya kuwaamuru waandishi wake wa Qur-an waandike kile alichowasomea, pia aliwaamuru wamsomee walichoandika na alifanya marekebisho pale walipokosea kama tu navyoj ifu nza katika had ith ifuatayo:



Zaidi bin Thabit amesema: "… Kila nilipomaliza kuandika (Wahyi) Mtume aliniamuru nisome nilichoandika na nilikuwa ninamsomea. Kama palikuwa na kosa alilisahihisha kisha aliwapa watu (kunakili na kuhifadhi vifuani).



Pia Mtume (s.a.w) ndiye aliyewaelekeza waandishi wake wa Qur-an wazipange aya na sura kama zilivyo katika msahafu tulionao hivi leo kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:



'Uthman bin Afan (r.a) ameeleza: "Ilikuwa kawaida ya Mtume wa Allah kila aliposhushiwa aya za sura mbali mbali (za Qur-an) au kila aya iliposhuka alimuita mmoja wapo wa waandishi wa Qur-an na kumwambia, "Andika aya hizi katika Sura kadhaa baada ya aya kadhaa."



Pamoja na Hadithi hii kuna hoja kadhaa za kihistoria zinazothibitisha kuwa Qur-an iliandikwa na kukusanywa katika msahafu tulionao hivi leo chini ya usimamizi na uangalizi wa Mtume (s.a.w) mwenyewe. Baadhi ya hoja hizo ni hizi zifuatazo:



Kwanza Anas (r.a) aliyekuwa miongoni mwa masahaba wa Mtume (s.a.w) ameeleza kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliwaamuru waigawanye Qur-an katika mafungu saba baada ya Suratul-Fatiha (sura ya ufunguzi). Fungu la kwanza katika haya lilikuwa na sura tatu, kisha likafuatiwa na fungu la sura tano, kisha la sura saba, kisha la sura tisa, kisha la sura kumi na moja, kisha la sura kumi na tatu na mwishowe sura zote zilizobakia ziliwekwa katika fungu moja. Fungu hili la mwisho limeanza na Suratul Qaaf. Ukihesabu sura zote pamoja na sura ya ufunguzi (Suratul-Fatiha) utakuta Suratul-Qaaf inakuwa ni sura ya hamsini (50). Sura hii pia ni ya 50 katika Msahafu tulionao hivi leo kuthibitisha kuwa mpango wa sura katika msahafu ulioelekezwa na Mtume Muhammad (s.a.w) haujabadilika mpaka hivi leo.



Pili Katika Hadithi ya Abu Daud, Hudhaifa (r.a) anasimulia kuwa amemuona Mtume (s.a.w) akisoma sura ya Al-Baqara, Al-Imran, An-Nisaa,Al-Maida na Al-An-'am katika mfuatano huo. Mpango wa sura hizi kama zilivyotajwa katika Hadithi hii ni kama ziivyo kwenye msahafu baada ya sura ya ufunguzi ambayo pia imebakia sura ya kwanza katika msahafu tangu alivyoiweka Mtume(s.a.w) katika nafasi ilipo. Hii inaonesha kuwa mpango wa sura lazima uwe umepangwa na Mtume(saw) mwenyewe kama alivyoongozwa na Allah (s.w).



Tatu Imam Tirmidh katika kitabu chake cha Hadithi anatufahamisha hadithi ifuatayo:
"Mtu mmoja aliuliza: "Ewe Mtume wa Allah! Tendo lipi ambalo Allah hulipenda kuliko yote?" Akajibu (Mtume) ("Tendo) la yule amalizaye safari na kisha akaendelea nayo". Pakaulizwa: "Nini maana ya kumaliza safari na kuanza nyingine?" Mtume alijibu: "Mwenye kuisoma Qur-an anaisoma tangu mwanzo hadi mwisho na amalizapo anarudia mwanzo na kusoma tena hadi mwisho na hufanya hivi kuwa kawaida yake; yaani kila amalizapo anaanza upya" (Darmi). Suala la kusoma Qur-an tangu mwanzo hadi mwisho ni hoja tosha ya kuwepo kwa mpango wa sura ya kwanza hadi mwisho.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2682


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Maandalizi ya kujiandaa mwenyewe kabla ya kufa ama kufikwa na mauti (kifo)
Kwakuwa kila mtu anatambua kuwa ipo siku atakufa hivyo ni vyema kuanza kujiandaa mapema. Soma Zaidi...

Umuhimu wa kusimamisha uislamu katika jamii
1. Soma Zaidi...

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan
Soma Zaidi...

Kuamini qadar na qudra katika uislamu
Kuamini Qadar ya Allah (s. Soma Zaidi...

Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram
Soma Zaidi...

maana ya swala kilugha na kisheria
Soma Zaidi...

mgawanyiko katika quran
MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani. Soma Zaidi...

SHIRK
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Swala ya Kuomba Toba (tawbah) na namna ya kuiswali
Soma Zaidi...

SIKILIZA QURAN KUTOKA KWA WASOMAJI WA TANZANIA
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Mbegu za maboga
Soma Zaidi...

Vituo vya kunuia ibada ya hija
Soma Zaidi...