Ruhusa ya Wachumba Kuonana Kabla ya Ndoa
Pamoja na sifa ya ucha-Mungu na wema, tunatakiwa tuwaoe wanawake tunaowapenda kwa sura na umbo; hivyo hivyo wanawake nao wachague wanaume wanaowapenda kwa sura na umbo ili kuzidisha mapenzi na upendo baina yao katika familia. Kwa mantiki hii Mtume (s.a.w) ameruhusu wachumba kuonana kabla ya kufunga ndoa kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa mwanamume mmoja alikuja kwa Mtume (s.a.w) akasema: "Ninakusudia kumuoa mwanamke miongoni mwa answari." Akasema Mtume
(s.a.w), 'Mwangalie kwanza kwa sababu kuna dosari katika macho ya Answari." (Muslim)
Jabir (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) amesema: "Mmoja wenu atakapochumbia, na akawa na uwezo wa kumtazama yule anayemchumbia na afanye hivyo." (Bukhari na Muslim)
Pamoja na ruhusa hii, bado waislamu wanalazimika kuendelea kuzingatia mipaka ya "Hijaab", kwamba hawaruhusiwi kukaa faragha au kutembea faragha mwanamke na mwanamume wasio maharimu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Tafsiri ya Quran kwa iswahili iliyotafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-BArwani
Soma Zaidi...Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu?
Soma Zaidi...Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.
Soma Zaidi...