image

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?

1.

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?

1.2.Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
Au
Haja ya kuhitaji mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Mwanaadamu pamoja na ujuzi na utundu alionao, hana uwezo wa kujiundia dini sahihi (mfumo sahihi wa maisha) utakaomfikisha na kumbakisha kwenye lengo la kuumbwa kwake. Na hii ni kutokana na sababu zifuatazo;

(a)Mwanaadamu anaathiriwa na matashi ya kibinafsi;
Pamoja na ujuzi, utambuzi na vipawa alivyopewa mwanaadamu, bado uamuzi na fikra zake ziaathiriwa na matashi ya nafsi yake katika upendeleo, uonevu na chuki, hivyo hawezi kuunda mfumo utakaosimamia haki na uadilifu.

(b)Nyenzo anazotumia mwanaadamu kujielimisha ni dhaifu;
Mwanaadamu hujielimisha kupitia nyenzo zifuatazo;


i.Milango ya fahamu.
Kama vile pua, masikio, ulimi, macho, ngozi, n.k, ambavyo vyote vina udhaifu na mara nyingine hutoa taarifu zisizo na ukweli.

ii.Akili na fikra.
Uamuzi wa mwanaadamu wa akili na fikra peke yake hauwezi kutoa jibu/mwongozo sahihi wa maisha kwani huathiriwa na wakati, matashi, mazingira, uelewa, upeo wa kufikiri na pia una kikomo.
Rejea Qurโ€™an (10:36,66), (25:43,45), (6:116) na (28:60)

iii.Sayansi na Uchunguzi;
Sayansi na majaribio haviwezi kutumika kama nyenzo kuu ya kuunda muongozo sahihi kwani vyote hivyo vinategemea milango ya fahamu ambayo nayo ina madhaifu mengi na kikomo pia.

iv.Historia;
Kutumia uzoefu wa kihistoria katika kuunda muongozo sahihi wa maisha ni dhaifu kwa sababu mwanaadamu huathiriwa na uzoefu na ujuzi wa awali na hivyo kutokubaliana na mabadiliko yeyote yatakayojitokeza.
Rejea Qurโ€™an (2:170, 257), (5:104) na (6:116).                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 149


Download our Apps
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-