Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri.
Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake
Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri.Watu wakamiminika Misri kuhemea chakula. Miongoni mwao wakawa ni wale ndugu zake Yusufu(a.s).
Wakaja ndugu zake Yusufu, na wakaingia kwake akawajua(12:58)
Wakapewa chakula na wakarejeshewa bidhaa zao walizoleta kubadilisha na chakula. Kisha Yusufu (a.s.) akawaagiza:
Na alipowapatia chakula chao alisema. (mkinijia mara ya pili) Nijieni na ndugu yenu wa kwa baba. Je hamuoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, na ni mbora wa wakaribishao. (12:59)
Basi waliporejea kwa baba yao, walisema: “Ewe baba yetu! Tutazuiliwa (chakula mara ya pili mpaka twende na ndugu yetu); basi mpeleke ndugu yetu pamoja nasi ili tupate kupimiwa; na yakini sisi tutamlinda.” (12:63).
Mzee Ya‘aquub(a.s), akasema:-Sitampeleka pamoja nanyi mpaka munipe ahadi kwa jina la Allah kwamba lazima mtamrejesha kwangu, isipokuwa nyote mzungukwe (na hatari au kufa). Basi walipompa ahadi yao alisema: Mwenyezi Mungu ndiye mlinzi juu ya haya tuyasemayo (12:66)
Baada ya kuchukua ahadi hii, Mzee Ya‘aquub aliwaambia wanawe kuwa wasiingie Misr kwa kutumia mlango mmoja,bali kila mmoja apitie mlango wake katika milango inayoingia humo(rejea Qur’an 12:67).
Kwa kuingia milango tofauti, Yusufu(a.s) alipata fursa ya kukutana na ndugu yake,Bin-Amin (wa kwa baba na mama) kabla ya wale wengine na kujitaambulisha kwake kisha kumfahamisha dhamira yake ya kumbakisha Misr-(rejea Qur’an 12:69)
Yusufu(a.s) alifanya hila ya kumbambikizia wizi ndugu yake kwa kuweka pishi ya kupimia ndani ya mzingo wake. Mara tu ya kuchukua mizigo yao na kuaga, palinadiwa kupotea kwa kipimo cha mfalme. Wote ndugu zake Yusufu(a.s) walikataa kuwa hawakuhusika na wizi wa chombo kile. Ikabidi ipitishwe sachi(search) na kikakutwa kwenye mzigo wa Bin Amin ambaye alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Misr. (rejea Qur’an 12:70-75).
Ndugu zake Yusufu(a.s) waliporejea nyumbani walimfahamisha mzee wao mkasa uliowapata. Mzee Ya‘aquub(a.s) alizidi kupata majonzi kwa kupotelewa na watoto wawili, lakini baadae alikuwa na matumaini ya kuwapata wote, ndipo akawaagiza wanawe:
Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusufu na nduguye, wala msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hawakati tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri (12:87)
Walipofika Misri walimtaka Yusufu(a.s) awafanyie ihsan kwa kuwapa chakula bure kwa vile hawakuwa na fedha ya kulipa huku wakimkumbusha kuwa Mwenyezi Mungu huwalip a watu wanaowatendea wema mwenzao. Hapo Y usufu(a.s) akawakumbusha:
Akasema: Je! Mnajua mliyomfanyia Yusufu na nduguye mlipokuwa ujingani?(12:89)
Wakasema: Je! Wewe ndiye Yusufu? Akasema: Mimi ndiye Yusufu, na huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anayemcha Mungu na kusubiri , basi Mwenyezi Mungu hapotezi malipo ya wafanyao mema(12:90)
Nduguze wakakiri makosa yao waliyomfanyia Yusufu(a.s) na kumuomba awasamehe. Wakasema: Wallahi! Mwenyezi Mungu amekuchagua juu yetu, na hakika sisi tulikuwa wenye makosa. (12:91)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 ai web app 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Nabii Isa(a.s) Azungumza Akiwa Mtoto Mchanga
Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba.
Soma Zaidi...Maandalizi ya Hijra ya Mtume na Mafunzo tunayoyapata kutoka katika hijra hii
Maandalizi ya Hijra ya Mtume (s.
Soma Zaidi...Mapambano ya waislamu dhidi ya maadui wa kiyahudi madina
Mayahud Mwanzoni Mayahud walipoona kuwa Waislamu wanafunga siku ya Ashura pamoja nao na wanaelekea Qibla cha Baitul- Muqaddas pamoja nao hawakuonyesha chuki ya dhahiri dhidi ya Mtume(s.
Soma Zaidi...KAZI ALIZOFANYA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KABLA YA UTUME
KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S.
Soma Zaidi...