Musa(a.s) Ahamia Madiani
Mchana wa siku moja Musa(a.
Musa(a.s) Ahamia Madiani
Mchana wa siku moja Musa(a.s) alimuona mtu wa Firauni amemuelemea Muisrail akimtwanga makonde mazito. Musa alichukizwa na kitendo kile, hivyo alipoombwa msaada alijikuta amemtwika Mmisri huyo ngumi nzito na kumuuwa palepale. Hapo Musa(a.s) akashituka na kuleta toba:
Mola wangu! Bila shaka nimedhulumu nafsi yangu, basi nisamehe; naye (Allah) akamsamehe. Kwa hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. (28:16)
Akasema: Mola wangu! Kwa kuwa umenineemesha, basi sitakuwa kabisa msaidizi wa watu wabaya. (28:17)
Habari ile ya kuuliwa mtu na Musa(a.s) ilifika kwa Firaun na ikatoka shauri kuwa Musa(a.s) akamatwe na kuuliwa. Musa(a.s) alipopata habari za kuaminika kutoka kwa mtu mwema,kuhusu hukumu ile, aliamua kutorokea nchini Madian katika mji awa Al-Bid uliopo kilometa 480 hivi mashariki ya Misr. Alipofika Madian hakuwa na pakwenda bali alijipumzisha kisimani ambapo aliwasaidia wasichana wawili kuwanywesha wanyama wao. Wasichana wale hawakuweza kupigana vikumbo na wanaume katika kunywesha wanyama wao, wakawa tu wanabakia pembeni wanaangalia. Kitendo kile kilimfurahisha Mzee wa Madian na akaagiza Musa(a.s) aitwe ili apate ujira wa kazi ile.
Basi akamjia mmoja katika (wasichana) wale wawili, anakwenda na huku anaona haya, akasema: โBaba yangu anakuita ili akulipe ujira wa kutunyweshea..........(28:25)
Musa alipofika kwa yule mzee alimsimulia hali halisi kuhusu dhulma, ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu uliopo nchini Misri, pamoja na kisa kilichompelekea yeye kuhamia Madiani. Yule mzee akamtuliza Musa(a.s), akasema: Usiogope umekwisha kuokoka na watu madhalimu (28:25)
Akasema: Mimi nataka nikuoze mmoja wapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane na kama ukitimiza kumi hiari yako, lakini mimi sitaki kukutaabisha utanikuta Inshaa-Allah miongoni mwa watu wema .(28:27)
Musa(a.s) aliafiki suala hilo, na mmoja katika wale mabinti aliridhia kuolewa na Musa(a.s) kwa mahari ya kutoa nguvukazi:
โAkasema(Musa: โMapatano) hayo yamekwisha kuwa baina yangu na baina yako; muda mmoja wapo nitakaoumaliza, basi nisidhulumumiwe; na Mwenyzi Mungu ni Mlinzi juu ya haya tunayoyasema.โ(28:28)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 kitabu cha Simulizi ๐2 ai web app ๐3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) ๐4 Kitabu cha Afya ๐5 Kitau cha Fiqh ๐6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Mbinu walizotumia makafiri wa kiqureish katika kuupinga uislamu makkah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sifa au vigezo vya dini sahihi
Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu
Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu.
Soma Zaidi...Historia ya kujengwa kwa Alkabah (Maka)
Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a.
Soma Zaidi...