Sunnan Ibn Majah


Sunnan Ibn Majah ni miongoni mwa vitabu sita vya Hadith sahihi kilichoandikwa na Muhammad bin Yazid anayejulikana kwa jina la Ibn Majah aliyezaliwa 209 A.H. na akafariki 295 A.H. Katika kukusanya Hadith alisafiri nchi mbali mbali palimokuwa na vituo vya elimu kama Basra, Kufa, Baghdad, Makka, Syria (Sham) na Misr.


Kitabu chake cha Hadith kinachojulikana kwa jina la "Sunnan" kimejishughulisha na Hadith zinazohusu sharia zinazoonyesha halali na haramu. Katika uchambuzi wa Hadith sahihi hakuwa makini sana kama walivyokuwa Maimam wawili wa mwanzo. Hivyo Hadith zake zimewekwa kwenye daraja la pili la usahihi. Hadith za daraja la kwanza ni Hadith za Bukhari na Muslim.