image

Jinsi tukio la Karatasi lilivyotokea wakati wa Mtume siku chache kabla ya kifo chake

Tukio la kartasiTukio la ‘kartasi’ lililonakiliwa katika vitabu vya Muslim na Bukhari kuwa siku tatu kabla ya kutawafu Mtume (s.

Jinsi tukio la Karatasi lilivyotokea wakati wa Mtume siku chache kabla ya kifo chake

Tukio la kartasi
Tukio la ‘kartasi’ lililonakiliwa katika vitabu vya Muslim na Bukhari kuwa siku tatu kabla ya kutawafu Mtume (s.a.w.) alitamka: “Nipeni peni na wino ili niwaandikie maelekezo yatakayowafanya watu wasipotee”, halina ukweli. Kutokana na kauli hii inadaiwa kuwa Umar alihutubia watu na kusema “Mtume yuko katika maumivu makali, Qur’an kama muongozo unatosha kwa watu. Baadhi ya watu wakasema Mtume amepoteza fahamu. Ipo kauli pia isemayo maneno haya yamesemwa na Umar (Khalifa wa pili)!


Moja ya Hadithi hizo imo katika kitabu cha Bukhari juzuu ya Hadithi namba 114 katika ukurasa wa 86 tafsiri ya Kiarabu Kingereza isemayo hivi:
Amesimulia Ubaidullah bin Abdullah kuwa Ibn Abbas amesema: Hali ya Mtume (s.a.w.) ilipokuwa mbaya alisema: “Nileteeni
karatasi ya kuandikia, na nitawaandikia tamko litalowapelekea
kutopotea”. Lakini Umar akasema; “Mtume anaumwa sana na tuna kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho kinatosheleza. Lakini Maswahaba wa Mtume wakatofautiana juu ya jambo hili. Kutokana na zogo hili Mtume akawaambia; “Ondokeni (na niacheni peke yangu) sio sahihi mbishane mbele yangu. Ibn Abbas akatoka nje na kusema: Imekuwa bahati mbaya na msiba mkubwa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amezuiwa kuandika tamko kwa Sababu ya kutokubaliana kwao na makelele yao.



Zingatio


Kutokana na Hadithi hii ni dhahiri kuwa Ibn Abbas ameshuhudia tukio hili na akatoka nje na kusema kauli hii. “Ukweli sio huu kwa Sababu Ibn Abbas alikuwa anatamka kauli hii alipokuwa anasimulia Hadithi hii, lakini yeye binafsi hakushuhudia tukio hili. Kwa maelezo zaidi juu ya hili rejea Fat-h al-Barr juzuu ya I, ukurasa wa 220).


Pamoja na kuwepo kwa maandishi juu ya tukio hili na wanahistoria kuwa na mifano na tafsiri tofauti, hakuna ushahidi wa kutosha kama tukio hili limetokea kweli au ni maandishi tu yenyewe yaliyopachikwa ili kukidhi haja ya waliyobuni tamko hili. Tukio hili halina ukweli wa kihistoria kwa sababu zifuatazo:


Ni muhali kudhania kuwa Mtume anaweza kuzuiwa na swahaba au na yeyote asiye Allah(s.w.) kutekeleza jambo la Utume wake; inashangaza zaidi kuwataja maswahaba kuwa wanaweza kumpinga Mtume katika Utume wakati huu akiwa katika kitanda cha mauti. Linaloshangaza zaidi ni lengo la tukio hili: Kwa mujibu wa maelezo yaliyopo ni kuwa Mtume(s.a.w.) hakuandika tamko alilokusudia ingawa aliishi siku nne baada ya tukio hili akiwa katika hali isiyo mbaya sana hata Abubakar akarudi kitongojini kwake, kulipokuwa na umbali wa maili mbili hivi kutoka mjini Madina. Kama hali ilikuwa hii kwa nini basi usia huu usiandikwe?


Hivyo Mtume(s.a.w.) kwa makusudi hakuacha uteuzi wowote wa nani ashike uongozi baada ya kutawafu kwake kwa kuwa ameacha mafunzo ya kudumu ya namna ya kupata viongozi, watu wachague wenyewe kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 351


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

tarekh 06
MAISHA YA UTOTONI YA MTUME S. Soma Zaidi...

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa
Soma Zaidi...

Musa(a.s) Ahamia Madiani
Mchana wa siku moja Musa(a. Soma Zaidi...

Vita vya Uhud na sababu ya kutokea kwake, Mafunzo ya Vita Vya Uhud
Vita vya Uhudi. Soma Zaidi...

Kisa cha Israa na Miraji na kufaradhishwa swala tano
Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME YUNUS(A.S)
Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA MTUME IDRISA (A.S)
Mtume aliyemfuatia Nabii Adam(a. Soma Zaidi...

Vita vya uhudi
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

tarekh
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUSUFU(A.S.): Ndoto ya nabii Yusufu
Mtume Yusufu(a. Soma Zaidi...

Uendeshaji na Kupanuka kwa Dola ya Kiislamu Kipindi cha Makhalifa Waongofu
Soma Zaidi...