Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar



Zipo tofauti za kimawazo kuhusiana na uchaguzi wa Khalifa wa kwanza, Abubakar(r.a.) mara baada ya kutawafu Mtume (s.a.w.).


Wapo wasemao uchaguzi ule ulifanyika katika mazingira ya kuchanganyikiwa, kwani mkutano haukuwa rasmi. Maelezo ya kundi hili yameegemea kauli zisemazo kuwa Abubakar(r.a.) na Umar(r.a.) walistushwa na taarifa kuwa Ansar walikuwa wamekutana kwenye ukumbi wa mikutano wa Thaqifa Bani Saidah, kumchagua kiongozi anayetokana na wao ambaye


angeshika uongozi wa dola ya Kiislamu baada ya Mtume(s.a.w.). Kwa mujibu wa kauli hizo, Abubakar(r.a.) na Umar(r.a.) walilazimika kwenda kwenye mkutano huo wakiwa na dhamira ya kuzuia usiendelee, hasa ikizingatiwa kuwa Mtume alikuwa bado hajazikwa na hilo ni suala zito lilohitajia muafaka wa Waislamu wote.


Kundi jingine lina mawazo kuwa, pamoja na kuwa mkutano wa Ansar haukuwa rasmi, lakini kuchaguliwa Abubakar(r.a.) kuliwafiki, kwa kuzingatia dokezo za Mtume(s.a.w), ishara zitokanazo na Qur’an na aliyokuja kuyafanya Abubakar(r.a.) wakati wa uongozi wake, ambayo yalidhihirisha usahihi wa chaguo la mkutano wa Thaqifa Bani Saidah.


Wapo wanaosema kuwa kutokuwepo kwa watu wa nyumba ya Mtume (Ahlul-Bayt) katika mkutano ule, kunabatilisha zoezi zima la uchaguzi wa Khalifa wa kwanza. Maelezo ya kundi hili yanatiwa tashdid na usia, unaodaiwa kuachwa na Mtume(s.a.w.) kwa “Ahlul- Bayt” muda mfupi kabla ya kutawafu kwake; unaosema kwamba haki ya uongozi wa ummah huu baada yake ni ya “Ahlul-Bayt”. Kwa hivyo Ali(r.a.) ndiye aliyestahiki nafasi hiyo, na warithi baada yake ni wanawe Hassan na Hussein kwa kuwa ni wajukuu wa Mtume(s.a.w.). Kundi hili linadai Ukhalifa wa Abubakar(r.a.), Umar(r.a.) na Uthman(r.a.) ni batili kwa kuwa hao si katika watu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.) na walipewa uongozi katika mikutano isiyo rasmi. Aidha hatua ya kuwafanya Makhalifa ni kudhulumu haki ya Ali(r.a.) akiwa ndugu wa Mtume.


Na kuna wasemao kwamba, kwa kuwa Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu si ya ukoo, kabila au Taifa fulani, na kwa kuwa hakuna aya katika Qur’an inayomwamrisha Mtume(s.a.w.) kurithisha dhima ya uongozi baada yake kwa watu wa nyumbani kwake (Ahlul-Bayt), basi jukumu la uongozi wa ummah limeachwa mikononi mwa waumini wenyewe. Kiongozi atachaguliwa kwa kuzingatia sifa mbali mbali zikiwemo uoni, ucha Mungu, siha n.k.


Sifa zote hizo zimpelekee kuongoza kwa haki na uadilifu. Kwa hiyo
Ukhalifa wa Abubakar, Umar na Uthman si suala la kubishaniwa.





                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 835

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake

Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri.

Soma Zaidi...
Bara arabu enzi za jahiliyyah, jiografia ya bara arabu

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nani alikuwa ni Sahaba wa kwanza kufariki akiwa Shahidi

Sahaba wa kwanz akufariki akiwa shahidi, alifariki kwa sababu ya mateso aliyoyapata kutoka kwa Makafiri wa ki Quraysh

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake

Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s.

Soma Zaidi...
Khalid Ibn al walid katika vita vya Muta

Yiomyokea khalid Ibn al walid katika vita vya Muta

Soma Zaidi...