image

Kukomeshwa kwa Riddah na Chokochoko Nyingine katika dola ya kiislamu

Kukomeshwa kwa Riddah na Chokochoko Nyingine katika dola ya kiislamu

Kukomeshwa kwa Riddah na Chokochoko Nyingine


Miongoni mwa makabila yaliyovamia Madina ni Bani Abbas na Zukian. Makabila haya yalipokuwa yanakimbilia Rabaza baada ya kushindwa kuivamia Madina waliwaua kikatili watu wa makabila yao ambao hawakuasi. Khalifa Abubakar aliongoza msafara wa kuwafukuza. Adui alishindwa, wengi waliuliwa na baadhi yao kuchukuliwa mateka. Khalifa Abubakar, kwa ujumla aliendesha vita dhidi ya makundi yote ya waasi na muda mfupi akaurudisha utulivu wa Dola ya kiislamu kama alivyoiacha Mtume(s.a.w). Si tu kuirudisha Dola katika hali ya utulivu, basi huifanya Dola kuimarika zaidi kijeshi na kiusalama.


Mitume wa uongo nao ambao idadi yao ilikuwa wanne walinyamazishwa. Mitume bandia hawa ni Aswad Ausi, Tulaiha,


Sajah bint Alharith na Musailamah Al-kadh-dhab(mzandiki). Aswad alitangaza utume wake Yemen baada ya kukusanya jeshi kubwa. Mtume huyu wa uwongo aliyekuwa anajitanda uso wote hata akaitwa mtume anayejitanda aliuliwa na Qais ibn Makshuh aliyekuwa chifu wa Waarabu akishirikiana na Feroze Dailme na Darweih.


Tulaiha anatoka katika kabila la Bani Asad kaskazini mwa Arabia. Mara baada ya kifo cha Mtume, alijitangazia utume. Khalifa Abubakar alimtuma Khalid bin Walid kuzima uasi huu. Khalid alikuwa jemadari mwenye kipaji cha kupigana na amerikodiwa kuwa miongoni mwa majemadari wa dunia. Mtume(s.a.w.) kwa uhodari wake alimwita “Upanga wa Mwenyezi Mungu. Khalid alishinda makabila yote yaliyokuwa yanamuunga mkono Tulaiha, wakiwemo Bani Tay, Bani Ghatfan na Bani Asad. Katika vita vilivyopiganiwa mahali paitwapo Bozakha, Jeshi la adui liliongozwa na Uyeina. Tulaiha alikimbilia Syria na mkewe, Uyeina alikamatwa mateka na kupelekwa Madina pamoja na watemi wengine wawili ambako baada ya kuomba msamaha walisamehewa.


Sajah bint Al-Harith anatoka katika kabila la Bani Tamim. Baada ya kifo cha Mtume(s.a.w.) watemi wengi wa kabila hili waliritadi ndipo Sajah akajitangazia utume. Sajah alikusanya watu elfu nne tayari kuelekea Madinah. Alipokuwa anakwenda Madina akapata habari za jeshi la Khalid bin Walid lililomuangamiza Tulaiha. Aliingiwa na khofu kwenda Madinah. Kwa udhuru huu akamuandikia Musailamah Mzandiki washirikiane ambaye naye alikwisha tangaza utume wake. Sajah aliungana na Musailamah mzandiki na kutambua utume wake. Wakati huo huo, Khalid bin Walid alifika makao makuu ya kabila la Bani Tamim na kutuliza uasi. Baada ya kutuliza fujo za kabila la Bani Tamim Khalid alimgeukia Musailimah Al-kadh-dhab.


Katika siku za mwisho za Utume katika mwaka wa kumi Hijriya(10 A.H.) Musailimah aliyeishi katika kitongoji cha Yamen (kakatikati ya Bara Arab) katika kabila la Bani Hanifa alijitangazia utume na akamuandikia Mtume (s.a.w.) juu ya utume wake na kumtaka wagawane Dunia nusu kwa nusu katika kuiendesha. Mtume (s.a.w.) alimjibu:


“Kutoka kwa Muhammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Musailimah alkadhab (mzandiki). Dunia iko chini ya ufalme wa Mwenyezi Mungu na humuachia kuitawala amtakaye. Na mwisho mwema ni wa wakweli.”35


Musailimah alikuwa na wafuasi wengi. Hivyo alikusanya jeshi la watu arobaini elfu lililopigana na jeshi la Waislamu la watu elfu kumi na tatu liliongozwa na Khalid bin Walid. Ikrima na Shurahbil walitangulia lakini walishindwa. Kuwasili kwa Khalid kuliwapelekea kukusanya nguvu na kufikia askari kumi na tatu elfu dhidi ya adui aliyekuwa na jeshi la watu arubaini elfu. Pambano hili ambalo matokeo yake yalikuwa “Bustani ya Vifo”, lilikuwa kali sana na lenye matokeo ya kuelemewa kwa adui. Waislamu waliwaangamiza Bani Hanifa na wasaidizi wao, wakawauwa adui 21,00046 (ishirini na moja elfu) pamoja na Musailimah aliyeuliwa na Wahshiy aliyemuua Hamza katika vita vya Uhud. Waislamu waliouawa ni mia nane (800) wakiwemo maswahaba 360 (mia tatu sitini) wengi wao wakiwa mahifadhi wa Qur’an. Vita hivi vilipiganwa mnamo mwaka 633 A.D. au 11 A.H. vilichukua miezi Saba. Vita vya Yamama vilimalizia uasi wa Riddah na Dola ikarudia utulivu.Chokochoko nyingine dhidi ya uongozi wa Abubakar zilitoka kwa Waajemi (Persians) waliokuwa washirikina na Warumi au Dola ya Wakristo wa Kirumi. Abubakar, aliwahamasisha Waislamu kuingia katika Jihad ili kuihami Dola ya Allah(s.w). Moja ya barua aliyoandika katika kuhamasisha Waislamu ni hii:


Kutoka kwa Khalifa wa Mtume(s.a.w) kwenda kwa Waislamu wote wanaume na wanawake wa Yemen. Nawasalimia wote wanaosomewa barua hii. Namshukuru Mwenyezi Mungu anayepaswa kuabudiwa. Mwenyezi Mungu ameifaradhisha Jihad na kuwaamuru (waumini) waitekeleze wakiwa katika halinzuri au hali ngumu, wanatakiwa wajitokeze kwenda katika Jihad kwa mali zao na nafsi zao. Jihad ni wajibu na malipo yake ni makubwa. Nawasihi Waislamu mjitokeze kwenda kwenye Jihad dhidi ya Warumi wa Syria. Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, shirikini katika Jihad kwa ikhlaswi. Hamtakosa moja ya zawadi hizi,ama kufa Shahid au ushindi na ngawira ..........36


Waislamu walihamasika na kujitokeza kwa wingi na kuwashinda maadui zao ushindi wa kishindo katika Ukhalifa wa Abubakar, ‘Umar na Ukhalifa wa ‘Uthman pale Waislamu walipokuwa hawajaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe.
                   


           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 252


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Kuzaliwa kwa Musa(a.s) na kukua kwake na maisha ya ujana wake na kupata Elimu
Musa(a. Soma Zaidi...

Kuangamizwa kwa jeshi la tembo mwaka alizaliwa Mtume Muhammad s.a. w
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w sehemu ya 4. Hapa utajifunza kuhusu historia ya kuangamiza kwa jeshi la tembo. Soma Zaidi...

tarekh 01
NASABA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Hawa ndio waaasi wakwanza wa Dola ya kiislamu wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...

Mtume(s.a.w) Kulingania Uislamu Siku za Hija
Baada ya Mtume(s. Soma Zaidi...

tarekh11
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Soma Zaidi...

Msafara wa vita vya Tabuk Dhidi ya Warumi
Ukombozi wa mji wa Makka (Fat-h Makka) mwaka 8 A. Soma Zaidi...

Hatua na Mambo (Taasisi za Kisiasa) za msingi alizotumia Mtume (s.a.w) katika kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah
Kuanzishwa kwa Dola ya Kiislamu Madinah. Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kiafrika hapo zamani
3. Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUUMBWA KWA NABII ADAMU (A.S)NA HADHI YAKE NA HADHI YA WANAADAMU DUNIANI
Adam(a. Soma Zaidi...

Maana ya kusimamisha uislamu katika dini
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)
Mtume(s. Soma Zaidi...