Shukurani za Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Allah(s.w)

Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Is- haqa(a.s), Nabii Ibrahim(a.s.) alimshukuru Allah(s.w) kwa maneno yafuatayo:

“Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa juu ya uzee (wangu watoto wawili hawa):- Ismail na Is-haqa. Hakika Mola wangu ni mwenye kusikia maombi (ya waja wake)” (14:39).

Is-haqa alipofikia utu uzima naye alipewa Utume na akaruzukiwa mtoto - Ya‘aquub(a.s) naye pia akapewa Utume..............Tulimpa Is-haqa na Ya‘akub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.Na tukawapa rehema zetu na tukawafanyia sifa za kweli tukufu(za kusifiwa na viumbe). (19:49-50).Na tukawajaalia kuwa maimamu wanaoongoza kwa amri yetu, na tukawapelekea wahyi wa kuzifanya kheri na kusimamisha Sala na kutoa Zaka. Na walikuwa kwetu ni wenye kutunyenyekea. (21:73).Aya tulizozinukuu zaweka wazi kuwa Is-haqa na mwanawe Ya’aquub, walikuwa Mitume na viongozi wa kusimamia utekelezaji wa sheria za Allah(s.w).Mafunzo Yatokanayo na Historia Nabii Is-haqa na Ya’aquub(a.s)

(i) Kutenda mema kunampatia muumini faida kubwa hapa duniani na huko akhera.

(ii) Tunatakiwa tuwachague kuwa viongozi wetu wa jamii wale waliotuzidi katika matendo mema.

(iii) Ni wajibu wa Waumini kumshukuru Allah(s.w) baada ya kupata ushindi, kufaulu au kupata mafanikio yoyote yale katika mchakato wa maisha.