image

Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri

Pamoja na kudhihirikiwa na ukweli wa udhaifu wa miungu wa kisanamu, watu wa NabiiIbrahiim(a.

Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri

Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri


Pamoja na kudhihirikiwa na ukweli wa udhaifu wa miungu wa kisanamu, watu wa NabiiIbrahiim(a.s) hawakusilimu,badala yake wakapitisha hukumu ya kumteketeza kwa moto wakasema:

“Mteketezeni kwa moto na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi ni watendao jambo.” (21:68)

Allah(s.w) alimnusuru Mtume wake kwa kuuamrisha moto uwe “baridi na salama” kwa Ibrahim:

Tukasema:“Ewe moto! Kuwa baridi na salama juu ya Ibrahimu.” (21:69)

“Basi walitaka kumfanyia vitimbi (vya kumchoma moto) lakini tukawafanya wao kuwa wadhalilifu. Na Tulimuokoa yeye na Lut....... (21:70-71)Nabii Ibrahiim(a.s) Kuhama Iraq


Nabii Ibrahiim(a.s) pamoja na jitihada zote alizozifanya za kuulingania Uislamu kwa hekima na kwa hoja madhubuti kwa baba yake, Mfalme na jamii kwa ujumla hakupata watu walioamini ila mkewe Sarah na mpwawe Lut(a.s). Kwa hali hiyo, Nabii Ibrahiim(a.s) baada ya kupata idhini ya Mola wake, alihama nchini mwake, Iraq, na kwenda katika nchi nyingine za Mashariki ya kati ili kulingania Uislamu humo. Alianza kuhamia Shamu (Syria).
“Basi Lut akamuamini na akasema (Ibrahiim). Hakika mimi nahamia katika (nchi aliyoniamrisha) Mola wangu, bila shaka yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (29:26) Na (Ibrahiim) akasema:Nakwenda. Mola wangu ndiye atakayeniongoza.” (37:99)Nabii Ibrahiim(a.s) baada ya kuhama Iraq alizizungukia nchi nyingi za Mashiriki ya kati ikiwa ni pamoja na Misri, Palestina, Trans-jordan na Hijaz. Sehemu zote hizi aliweka vituo vya harakati alivyokuwa akivitembelea. Alimuweka mpwa wake, Lut(a.s),katika kituo cha T rans-jordan.Aliporuzukiwa watoto wema aliowaomba,Ismail(a.s) na Is-haq(a.s) aliwaingiza kwenye harakati,na akamfanya Ismail(a.s) mkuu wa kituo Hijaz na Is-haq(a.s) mkuu wa kituo cha Palestina. Allah(s.w) aliwateua viongozi hawa wa vituo vya harakati kuwa Manabii wa sehemu hizo na Mzee Ibrahiim(a.s) akiwa kiongozi wao.Mji wa Makka katika nchi ya Hijaz alipokuwa akiishi Ismail (a.s), ulifanywa kuwa makao makuu ya harakati za kuhuisha Uislamu. Makka ilianza kutumika rasmi kama kituo kikuu cha harakati pale Mzee Ibrahiim (a.s) walipokamilisha kujenga upya Ka’abah na Allah(s.w) kumuamrisha awatangazie watu kuja kuhiji pale kila mwaka.
“Na Ibrahiim alipoinua kuta za nyumba (hii ya Al-Ka’abah) na Ismail (pia) (wakaomba wakasema:) “Ee Mola wetu! Tutakabalie (amali yetu hii ya kujenga huu msikiti). Hakika wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua.” (2:127)
Na (kumbuka) tulipomkalisha Ibrahimu mahali penye ile Nyumba (takatifu na tukamwambia): “Usinishirikishe na chochote na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya waizungukao na wanaokaa hapo (kufanya ibada yao) na wanaorukuu na kusujudu, (wanaosali).” Na (tukamwambia) “Utangaze kwa watu habari za Hija, watakujia, (wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyekonda (kwa machofu ya njiani) wakija kutoka katika kila njia ya mbali. (22:26-27)                   

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 353


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Nasaba ya mtume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD
Baada ya Nuhu(a. Soma Zaidi...

Upinzani Dhidi ya Dola ya Kiislamu Wakati wa Makhalifa
Soma Zaidi...

fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

Vita vya Badr: Chanzo na sababu za vita vya Badr, Mafunzo ya Vita Vya Badr
Vita vya Badri. Soma Zaidi...

vita vya ahzab, sababu ya kutokea vita hivi na mafunzo tunayoyapata
Vita vya Ahzab- Maquraish waliungana na mayahudi, wanafiki na makabila mengine ya waarabu baada ya kuona kuwa wao peke yao hawawezi kuufuta Uislamu. Soma Zaidi...

Tukio la kupasuliwa kifua Mtume Muhammad S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 7 Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ibrahiim(a.s)
Soma Zaidi...

Kuangamia kwa Mtoto na Mke wa Nuhu(a.s)
Tukirejea Qur’an (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SALIH(A.S
Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Nini maana ya tabii tabiina
Soma Zaidi...

Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Soma Zaidi...