NUHU(A.S) NA WATU WAKE NA UOVU WALIOKUWA WAKIUFANYA WATU WAKE


Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a.s)katika Mitume waliotajwa katika Qur-an ni Nabii Nuhu(a.s). Nuhu(a.s) ni miongoni mwa Mitume wa mwanzo mwanzo kabisa. Kutokana na mabaki ya kihistoria tunajifunza kuwa Nabii Nuhu na kaumu yake waliishi katika nchi ya Iraq.Mazingira ya Jamii Aliyoikuta Nabii Nuhu (a.s)
Nabii Nuhu(a.s) aliwakuta watu wa jamii yake wakimshirikisha Allah(s.w)kwa namna mbali mbali nawalikuwa wakiabudia masanamu waliyoyachonga na kuyapa majina ya W adda , Suwa’a , Y aghuutha , Y a’uuka na Nasraa . Kama tulivyofahamishwa katika Qur-an kuwa viongozi wa jamii ya kishirikina ambao walikuwa ndio wapinzani wakubwa wa ujumbe wa Nabii Nuhu waliwanasihi wafuasi wao:
“Msiache miungu yenu, wala msiwache Wadda wala Suwa’a wala Yaghuutha na Ya’uka na Nasraa.” (71:23).Mtume(s.a.w) anatufahamisha katika Hadith kuwa Wadda na wale waliotajwa pamoja naye walikuwa ni watu wacha-Mungu katika jamii yao. Walipofariki,watu wakaanza kuyazungukiamakaburi yao na shetani akakichochea kizazi kilichofuata kuunda sanamu za watu hao. Kwa kufanya hivyo walidhani wangeliweza kuwaiga vitendo vyao vyema kwa kuwa na taswira za watu hao daima katika akili zao. Kizazi cha tatu kilishawishika kirahisi sana kuwa watu hao walikuwa ni miungu wanaostahiki kuabudiwa badala au pamoja na Allah(s.w). Masanamu yote yanayoabudiwa yana historia ya namna hii.Wito wa Nabii Nuhu(a.s) kwa Watu Wake
Nabii Nuhu(a.s) kama walivyofanya Mitume wote, aliwafundisha watu wake Tawhiid kuwa wamuamini Allah (s.w) kwa kuzingatia ishara mbali mbali zilizowazunguka, na kwamba wamuabudu yeye peke yake na wasimshirikishe na chochote. Aliwaonya juu ya adhabu kali itakayowafika iwapo hawatakoma kumshirikisha Allah(s.w) na miungu wengine.Juu ya wito wa Nuhu(a.s) kwa watu wake Qur-an inatufahamisha:
“Tulimpeleka Nuhu kwa watu wake, naye akasema: “Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila yeye. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya siku (hiyo) iliyo kuu.” (7:59).