picha

Bara la Arabu Zama za Jahiliyyah

Wakati Mtume(s.

Bara la Arabu Zama za Jahiliyyah

Bara la Arabu Zama za Jahiliyyah
Zama za Jahiliyyah ni zile zama ambazo watu walikuwa wakiendesha maisha yao ya kibinafsi na kijamii kwa kufuata matashi yao kinyume na mwongozo wa Allah(s.w) na mitume wake.



Wakati Mtume(s.a.w) anazaliwa katika karne ya Sita (570 A.D) dunia ilikuwa katika giza totoro la ujahili. Wakazi wa Bara Arab, katika kipindi hicho walikuwa chini sana katika maadili. Ubabe, unyang’anyi na uporaji mali ya misafara ya biashara yalionekana matendo ya kishujaa na ya kujivunia. Wanyonge hawakuwa na haki, wanawake walinyanyaswa na kudhalilishwa hadi kufikia watoto wa kike kuzikwa wangali hai na wanawake kurithiwa kwa nguvu kama ilivyorithiwa mali.



Kwa muhtasari hali ya Bara Arab wakati huo ilikuwa kama alivyoeleza Jaffari bin Abu Twalib mbele ya Mfalme Najash wa Uhabesh:

“Ewe Mfalme, sisi tulikuwa waovu na majahili, tukiabudia masanamu na kula nyamafu hata mizoga ya wanyama waliokufa wenyewe.Tulifanya kila aina ya matendo machafu na ya aibu. Hatukuwa wenye kuwajibika kwa jirani na jamaa zetu. Wenye nguvu miongoni mwetu waliwakandamiza wanyonge. Kisha Allah akamleta Mtume miongoni mwetu ambaye tulimfahamu vema kwa nasaba yake, utukufu wake na uzuri wa tabia yake adhimu. Alituita tumuabudu Mungu mmoja tu na akatukataza kuabudia masanamu na mawe. Alitufundisha kusema ukweli kutunza amana, kuwaangalia ndugu na jamaa na kuwafanyia wema na kuacha maovu. Alituamrisha kusimamisha swala na kutoa Zakat. Alituamrisha kujiepusha na maovu na kujiepusha na umwagaji damu. Alitukataza zinaa, kusema uwongo, kula mali ya yatima na kuwasingizia uovu wanawake watwaharifu.
Alitufundisha Qur-an...” 4 (A Guillaume – The life of Muhammad).



Hali hii ya ujahili haikutawala Bara Arab peke yake, bali katika karne hii ya 6 A.D ulimwengu wote, Mashariki na Magharibi, ulizama katika giza totoro la uovu na ujahili. Ulimwengu katika zama hizo, wanyonge na watu wa chini walikandamizwa na kudhulumiwa pasina chembe ya huruma na wenye uwezo na watukufu miongoni mwao.



Katika kipindi hicho, hata wale waliodai kufuata mafundisho ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, Mayahudi na Wakristo, walikuwa katika giza hilo hilo la uovu na ujahili. Mayahudi waliacha mafundisho ya Mtume wao na wakaamua kuishi kulingana na matamanio ya nafsi zao. Walipotokea Mitume waliwafanyia maovu mengi kama ilivyobainishwa katika Qur-an. Wakristo nao waliacha mafundisho sahihi ya Nabii Isa(a.s) badala yake wakafuata ushirikina wa Warumi. Walileta uzushi mwingi juu ya Dini ya Allah(s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:




“Na Mayahudi wanasema: ‘Uzeiri ni Mwana wa Mwenyezi Mungu’ na Wakristo wanasema; ‘Masihi ni Mwana wa Mwenyezi Mungu’; haya ndiyo wayasemayo kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa! (9:30)



Wamewafanya Wanavyuoni wao na Watawa wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu, na wamemfanya Masihii Mwana wa Maryamu (pia Mungu) hali hawakuamrishwa isipokuwa kumuabudu Mungu mmoja, hakuna anayestahiki kuabudiwa ila Yeye. Ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo.” (9:31).





“Enyi Mlioamini! Wengi katika Makasisi (Wanavyuoni wa Mayahudi na wakristo) na Watawa (wao) wanakula mali za watu kwa batili na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu..........” (9:34)



Katika kipindi hicho cha historia utawala wa Kikristo Ulaya Magharibi uliwakandamiza na kuwanyonya wanyonge kama utawala wa kishirikina ulivyokuwa ukifanya huko Mashariki ya Kati na Mashariki ya mbali. Katika kipindi hiki wanasayansi walioibuka na ugunduzi ulio kinyume na maelezo ya Wakuu wa Kanisa walisulubiwa na kuuliwa kinyama miongoni mwao ni mwanasayansi maarufu, Galileo.




                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 2375

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

NI UPI MKATABA WA AL-FUDHUL NA ASILI YAKE, ATHARI ZAKE NA WALOHUSIKA

MKATABA WA AL-FUDHULBaada ya vita hivi viongozi wa pande mbili hizi waliamuwa wakae chini na wakubaliane kuweka kanun i na utaratibu utakaozuia kutotokea uonevu kama huuu tena.

Soma Zaidi...
Mfumo wa ulinzi na usalama katika fola ya uislamu madinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Sababu za makafiri wa kiqureish kuupinga ujumbe wa uislamu

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtume amezaliwa mwaka gani?

Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake.

Soma Zaidi...
Kuangamia kwa Mtoto na Mke wa Nuhu(a.s)

Tukirejea Qur’an (11:36-48) na (23:26 -29) tunapata maelezo juu ya mchakato wa kuangamizwa makafiri na kuokolewa waumini katika kaumu ya Nabii Nuhu(a.

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na maandalizi ya mtume ki-wahay

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...