Mtume Muhammad s.a.w analelewa na Babu yako ikiwa na umri wa miaka 6

Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 9.

KULELEWA NA BABU YAKE:
Mzee ‘Abdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana. Mzee huyu alimpenda sana mjukuu wake kuliko ambavyo alivyokuwa anawapenda watoto wake.

 

Alikuwa katu hamuachi mjukuu wake akiwa peke yake. Mzee Abdul Al-Muttalib alikuwa akiwekewa godoro kwenye kivuli cha Al-kabah na watoto wake wanakaa pembeni ya godoro kwa heshima ya baba yao, basi alikuwa Mtume (s.a.w) anakaa kwenye godoro lile. Baba zake wadogo wanapomtoa mzee Abdul al-Muttalib alikuwa akiwakataza na kuwaambia kuwa kijana huyu atakujakuwa na nafasi nzuri.



Mzee Abdul al-Muttalib alikuwa sikuzote akipendezwa na vitendo vya mjukuu wake. Mzee huyu aliendelea kumlea yatima huyu mpaka alipofikia umri wa miaka nane, na hapa ndipo mzee huyu alipofariki dunia na kuongeza majonzi zaidi kwa kijana huyu.

 

Mzee Abdul al-Muttalib alifariki wakati Mtume (s.a.w) alipokuwa na umri wa miaka nane na miezi miwili na siku kumi (10).

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 2391

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰5 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana: