Wakati Nabii Musa(a.
Wakati Nabii Musa(a.s) amekwenda kupokea Taurati, katika hizo siku arobaini alizoahidiwa na Mola Wake, Saamiriy alitengeneza sanamu la ndama wa ng'ombe linalotoa sauti unapovuma upepo na kuwashawishi Bani Israil walifanye mungu sanamu hilo la ndama.
"Na kumbukeni tulipomuahidi Musa siku arobaini (afanye ibada mfululizo) Mkamfanya ndama (kuwa Mungu) baada yake, na mkawa madhalimu (wa nafsi zenu)" (2:51).
Harun(a.s) aliyemkaimu Nabii Musa(a.s) aliwakataza watu wake wasiabudie sanamu la ndama. Baadhi wakamtii na wengine wakamuasi.
Na Harun aliwaambia zamani (akasema): "Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mumefitinishwa tu kwa (kitu) hiki. Na kwa yakini Mola wenu ni yule Mungu Mwenye kurehemu. Basi nifuateni na tiini amri yangu (muache kuabudu Mungu huyu)".
Wakasema: "Hatutaacha kabisa kumuabudu mpaka Musa arejee kwetu, (aturudie)" (20:90-91).
Musa(a.s) aliporejea alimlaumu Harun(a.s) kwa kutomfuata huko alikokuwa baada ya watu wake kumuasi. Harun(a.s) alijitetea kuwa hakufanya hivyo kwa kuchelea kuwafarakanisha Bani Israil kwa kuondoka na kundi moja na kuliacha lingine nyuma kabla ya kauli yake (Musa(a.s)) - rejea (Qur'an 2:92-94).
Musa(a.s) aliondoa ile fitina kwa kumuadhibu Saamiriy na walioshirikiana naye na kuliangamiza lile sanamu.
Ikumbukwe kuwa ni muda mfupi sana toka Bani Israil walipokombolewa kutokana na utumwa wa Firauni. Lakini mara wanamsahau Mola wao na kuanza kuabudu ndama. Hii inaonesha ni kwa kiwango gani Bani Israil waliathiriwa na maisha ya ushirikina kwa kipindi walichoishi Misr. Ni muhimu basi tuone jinsi mazingira yanavyoathiri imani, maadili na mwenendo wa mtu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 11
Soma Zaidi...Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno ยSwalaatย lina maana ya ยombi au ยdua.
Soma Zaidi...Uasi katika dola ya kiislamu na matokeo yake.
Soma Zaidi...