image

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina

Wanafiki


Muda mfupi baada ya Mtume(s.a.w) kuhamia Madinah, ukiwaacha Mayahud, takriban watu wengi wa Madinah walisilimu. Hata hivyo si wote waliosilimu kwa dhati. Baadhi ya watu walisilimu tu kuwaonyesha watu, lakini hawakufurahia kabisa mafanikio ya ujumbe wa Mtume(s.a.w). ‘Abdullah bin Ubayyi aliyekuwa anatazamia kuvishwa taji la Ufalme kabla ya Mtume(s.a.w) kuhamia Madinah alikuwa ndiye kiongozi wa wanafiki. ‘Abdullah bin Ubbayyi na kundi lake pamoja na kutoa kwao shahada walikuwa na chuki dhidi ya Mtume(s.a.w) na Waislamu. Kundi hili lilidhihirisha chuki yao dhidi ya Uislamu kama ifuatayo:



Kwanza katika siku za mwanzo mwanzo za kipindi cha Madinah, Abdullah bin Ubayyi alitumiwa barua na Maquraish ili amuue Mtume(s.a.w) au amfukuze Madinah. ‘Abdullah hakuweza kufanya chochote kwa kuhofia kuwa watu wake wa Madinah watakuwa dhidi yake, hasa pale Mtume(s.a.w) alipomwambia:

“Unataka kuzusha vita dhidi ya ndugu zako na vijana wako?”20


Pili, wanafiki walishirikiana na Mayahudi katika kuwatia wasiwasi waumini juu ya mabadiliko ya Qibla.



Tatu, walishirikiana na Mayahudi na maadui wengine wa Uislamu katika njama za kutaka kumuua Mtume(s.a.w) na kuhilikisha Uislamu. Kwa mfano, Mayahudi wa Banu Nadhir walipopewa amri na Mtume(s.a.w) ya kuondoka Madinah,
‘Abdullah bin Ubayyi, kiongozi wa wanafiki, aliwatumia ujumbe kuwa wasikubali kuhama na akawaahidi kuwa atawasaidia katika mapambanao dhidi ya Mtume(s.a.w) na Waislamu.




Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu kabla yenu (Mayahudi) (Wanawaambia): “Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hatutamtii yoyote kabisa juu yenu. Na kama mkipigwa vita lazima tutakusaidieni.” Na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa wao ni waongo. (59:11)



Nne, wanafiki 300 wakiongozwa na ‘Abdullah bin Ubayyi walijiengua katika jeshi la Waislamu katika vitu vya Uhud.

Tano, katika msafara wa vita vya Banu Mustaliq, ‘Abdullah bin Ubayyi alichochea ugomvi baina ya Answar na Muhajirina na kutishia kuwafukuza Muhajiriina watakaporejea Madinah.




Wanasema: “Tukirudi madina, Mwenye utukufu atamfukuza mnyonge,” (yaani Abadallah bin Ubay atamfukuza Mtume). Na utukufu hasa ni wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waislamu; lakini wanafiki hawajui. (63:8)



Sita, wanafiki chini ya uongozi wa ‘Abdullah bin U bayyi, walimzulia mkewe Mtume(s.a.w), Aysha bint Abubakar, kitendo kichafu cha zinaa ili kumuudhi Mtume(s.a.w) na Waislamu na kuupaka Uislamu matope.



Saba, wanafiki walikuwa wakitoa nyudhuru za uwongo ili kuepa jukumu la kuupigania Uislamu. Kwa mfano katika msafara wa Tabuuk, wanafiki kutokana na ugumu wa safari, hali ya njaa iliyokuwepo na woga wa kupambana na jeshi kali la Warumi, walitoa nyudhuru za uongo mbele ya Mtume(s.a.w) ili wasiende vitani.



Kama ingalikuwa faida iliyo nyepesi (kupatikana) na safari fupi, kwa yakini wangalikufuata (hao wanaojipa Uislamu wa uwongo). Lakini safari hii ya taabu imekuwa ndefu kwao. Nao wataapa kwa Mwenyezi Mungu, “Kama tungaliweza bila shaka tungelitoka pamoja nanyi.” Wanaangamiza nafsi zao; na Mwenyezi Mungu anajua (kwa hakika) kuwa hao ni waongo (tu). (9:42)

Pia wanafiki walikuwa wakiwashawishi Waislamu wasiende vitani, wakawahofisha adha na madhara watakayopata.




Walifurahi walioachwa nyuma (wasende vitani. Walifurahi) kwa kule kukaa kwao nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walichukia kupigana kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wakasema (kuwaambia wenzao): “Msende (vitani) katika joto hili.” Sema (uwaambie): “Moto wa Jahanamu una joto zaidi. Laiti wangefahamu.” (9:81)

Nane, Wanafiki walijenga msikiti wakishirikiana na maadui wengine wa Uislamu, ili uwe kichaka cha kupanga njama za kuhujumu Uislamu.




Na wako (wanafiki wengine) waliojenga msikiti wa (kuleta) udhia na kutia nguvu ukafiri, na kuwafarikisha walioamini na kuufanya mahali pa kuwangojea wale waliomfanyia vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake zamani. Na bila shaka wataapa (waseme): “Hatukukusudia ila wema.” Lakini Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo. (9:107)

Katika kuondosha chokochoko na taathira ya wanafiki katika jamii ya Kiislamu, Mtume(s.a.w) aliamrishwa na Mola wake kuwa mgumu kwao:




Ewe Nabii! Shindana na makafiri na wanafiki na uwe mgumu kwao; na makazi yao ni Jahanamu; nayo ni marejeo mabaya kabisa. (66:9)

Katika kuwa mgumu kwao, Mtume(s.a.w) alivunja msikiti wao kwa amri ya Allah(s.w).



Jengo lao hilo walilolijenga (likavunjwa na Mtume) litakuwa Sababu ya kutia wasi wasi (uchungu) nyoyoni mwao (siku zote), mpaka nyoyo zao zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na Mwenye hikima. (9:110)

Vile vile Mtume(s.a.w) aliwatenga wanafiki na jamii ya Waislamu, alipoamriwa na Mola wake kutomswalia na kumuombea msamaha mmoja wao akifa.




(Ewe Mtume)! Waombee msamaha (hao wanafiki) au usiwaombee; (yote sawa sawa). Hata ukiwaombea msamaha mara sabiini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa Sababu ya kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu wavunjao amri (Zake). (9:80)




Wala usimsalie kamwe mmoja wao yoyote yule akifa, wala usisimame kaburini kwake (kumuombea dua). Hakika hao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na wakafa, na hali ni wenye kuvunja amri (za Mwenyezi Mungu). (9:84)





                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 747


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Chokochoko na Upinzani wakati wa khalifa uthman khalifa wa Tatu
KUPOROMOKA KWA DOLA YA KIISLAMU ALIYOICHA MTUME(S. Soma Zaidi...

Ghasia na chokochoko za Makhawariji na kuuliwa kwa Ally
Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA MTUME IDRISA (A.S)
Mtume aliyemfuatia Nabii Adam(a. Soma Zaidi...

Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija. Soma Zaidi...

tarekh 10
KULELEWA NA BABA YAKE MDOGOBaada ya kufariki kwa mzee huyu, kiongozi mkubwa wa maquraysh na makkah, kiongozi ambaye jeshi la Abrah liliangamizwa ndani ya utawala wake. Soma Zaidi...

Matukio mbalimbali katika historia ya uislamu kabla na baada ya Mtume (s.a.w) na makhalifa wake wanne
1. Soma Zaidi...

Kukomeshwa kwa Riddah na Chokochoko Nyingine katika dola ya kiislamu
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII MUSA(A.S) NA HARUN(A.S)
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

Imam Abu Hanifa: Nuuman Ibn Thabit
Soma Zaidi...

Mitihani aliyopewa Nabii Ibrahimu kutoka kwa Allah
Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...

Hawa ndio waaasi wakwanza wa Dola ya kiislamu wakati wa makhalifa
Soma Zaidi...

Watu waliovunja amri ya kuheshimu siku ya Jumamosi.
Katika zama za kale Mayahudi walikatazwa kufanya kazi siku ya Jumamosi. Soma Zaidi...