picha

Kuchimbwa upya kwa kisima cha Zamzam

Sura na historia ya mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 3.Hapa utajifunza kuhusu kufukuliwa kwa kisima cha Zamzam baada ya kufukiwa muda mrefu.

KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAM
Kwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Basi akachimba na ndipo akakuta chini ya kisima vitu ambavyo vilifukiwa pamoja na kisima.

 

Walofukia vitu hivi ni watu kutoka kabila la Jurhum. Hawa pindi walipolazimika kuondoka Maka walikifukia kisima cha zamzam na kufukia baadhi ya vitu vya thamani kama mapanga, nguo za vita, na dhahabu. Baada ya hapo mlango wa alka’aba ukatengenezwa kwa hii dhahabu waloipata. Na unyweshwaji wa maji ya zamzam kwa mahujaji ukarudi upya.



Basi kisima cha zamzam kilipoanza kutoa maji, watu kutoka kabila la quraysh walitaka kufanya makubaliano juu ya maji yale lakini Abdul Al-Muttalib alikataa kwa kudai kuwa Allah amempa mamlaka yeye tu.

 

Basi wakakubaliana wakamuulize kuhani kutoka ukoo wa Bani Sa’ad juu ya swala hili. Basi Allah akawaonesha alama za ukweli juu ya madai ya Abdul Al-Muttalib. Baada ya hapo mzee Abdul Al-Muttalib kwa shukran yake kwa Allah akaapa kumtoa kafara mtoto wake kwa Mwenyezi Mungu.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views 2255

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰3 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     πŸ‘‰6 ai web app    

Post zinazofanana:

Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga

Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.

Soma Zaidi...
Historia ya Dhulqarnain

Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: β€œMwenye Pembe Mbili”.

Soma Zaidi...
Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake

Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri.

Soma Zaidi...