Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)

Kutokana na historia ya Nabii Lut(a.s) tunajifunza yafuatayo:

(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.s) na waumini aliokuwa nao.(ii) Tusichelee watu katika kukemea maovu.(iii) Kila mtu atahesabiwa na kulipwa kulingana na amali zake.
Hatafaidika mtu kwa amali njema za mwingine na wala hataadhibiwa mtu kwa matendo mabaya ya mwingine.(iv) Tumuogope Allah(s.w), kwani adhabu yake ni kali na hakuna awezaye kujinusuru nayo inapokuja.(v) Tujitahidi kusimamaisha Uislamu kwa mali na nafsi zetu bila ya kumchelea yeyote.(vi) Hatma ya mapambano dhidi ya makafiri ni Waislamu kuibuka washindi.