image

Historia ya Watoto Wawili wa Nabii Adam

“Na wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): “Nitakuua”.

Historia ya Watoto Wawili wa Nabii Adam

Historia ya Watoto Wawili wa Nabii Adam .

“Na wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): “Nitakuua”. Akasema (yule aliyeahidiwa kuuawa): “Mwenyezi Mungu huwapokea wamchao tu”. “Kama utanyoosha mkono wako kwangu kuniua, mimi sitanyoosha mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi ninamuogopa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu .


“Mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako, na kwa hivyo uwe miongoni mwa watu wa motoni. Na haya ndiyo malipo ya madhalimu”.“Basi nafsi yake ikamwezesha kumwua nduguye, na akawa miongoni mwa wenye kukhasirika”. Hapo Mwenyezi Mungu akamleta Kunguru anayefukua katika ardhi ili amwonyeshe jinsi ya kuificha maiti ya ndugu yake. Akasema: (yule ndugu aliyeua) “Ole wangu: Nimeshindwa kuwa sawa na kunguru huyu na kuficha maiti ya ndugu yangu”? Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta. Kwa sababu ya hayo tukaawandikia wana wa Israel ya kwamba atakayemuua mtu bila ya yeye kuua mtu, au bila ya kufanya fisadi katika nchi, basi ni kama ameua watu wote, na mwenye kumwacha mtu hai (kumsaidia kuishi) ni kamaH amewaacha hai watu wote. Bila shaka Mitume waliwafikia na hoja zilizo wazi; kisha wengi katika wao baada ya haya walikuwa waharibifu sana katika nchi” (5:27-32).Katika ya hizi majina ya watoto hawa wa Adam hayakutajwa. Bali majina hayo yamechukuliwa kutokana na maandishi mengi ya historia hasa historia ya Mayahudi. Wafasiri wengi wa Qur’an wanataja katika kuzitafsiri aya hizi kuwa, Habil na Kabil ni watoto wa moja kwa moja wa Adam na Hawwa. Na sio imetajwa kwa ishara tu kwa kuzingatia kuwa watu wote wametokana na Adam na Hawwa. Kwa mujibu wa maelezo ya Sheikh A. S. Farsy, hiki ndicho kisa cha awali cha mtu kumuua mwenziwe. Na aliyeuawa ndiye mwanaadamu wa mwanzo kufa. Kwa sababu hiyo basi aliyefanya mauaji hakujua nini la kufanya na yule maiti. Ndipo Allah(s.w) akamleta kunguru kumwonyesha namna ya kuhifadhi maiti ya ndugu yake.Ili kuyafahamu vyema mafundisho ya kisa hiki cha watoto wa Adam(a.s) ni vyema tuyazingatie mazingira na wakati ziliposhuka aya za kukielezea kisa chenyewe. Tunafahamu kuwa awali Allah(s.w) aliwachagua Mayahudi na kuwapa ujumbe wake ili watekeleze wao wenyewe na kisha waufikishe kwa watu. Kwa hiyo akawatuma Mitume wengi miongoni mwa Mayahudi. Kutokana na neema hii waliyopewa kuletewa mwongozo na kupewa jukumu la kuusimamia, wakawa ni watu wenye hadhi kubwa.“Enyi kizazi cha Israil (Mayahudi); Kumbukeni neema zangu nilizokuneemesheni na nikakutukuzeni kuliko viumbe wengine (wa wakati huo)” (2:47).

Hata hivyo Mayahudi hawakuithamini neema hii ila wachache tu. Zaidi ya wao wenyewe kutokufuata mwongozo waliwaua mitume na kufuata baadhi ya kitabu huku wakiacha sehemu nyingine. Hii iliwapelekea kupata laana ya Allah(s.w).

Aidha Mayahudi waliobashiriwa kuja kwa Mtume(s.a.w) na waliahidi kuwa watamfuata. Bali alipokuja walimkataa.
Na(wakumbushe)aliposema (Nabii) Isa bin Maryam(kuwaambia Mayahudi): Enyi wana wa Israil! Mimi ni mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, nisadikishaye yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na kutoa habari njema ya Mtume atakayekuja nyuma yangu ambaye jina lake litakuwa Ahmad(Muhammad). Lakini alipowajia na hoja zilizo wazi walisema: Huu ni udanganyifu ulio dhahiri. (61:6)Mayahudi hawakuishia kumkataa tu Mtume(s.a.w) walidhamiria kumwua pia. Hapakuwa na jingine lililowapelekea kufanya hayo, bali ni husuda na kibri. Ilikuwa wao baada ya kunyan’ganywa neema ya kuwa wafikishaji wa ujumbe wa Allah, watanabahi na kufanya mema ili Allah aweze kuwasamehe. Lakini wao walimwonea husuda Mtume(s.a.w) na wakawa wanafanya njama za kumwuua.Ni katika mazingira haya Allah(s.w) anabainisha kisa hiki cha watoto wa Adam(a.s) ili kuwaonya Mayahudi na sisi sote kuwa: Tusiwe na husuda juu ya Neema na amali njema za watu weninge hata tukaingia kwenye makosa kama ya mtoto wa Adam. Bali nasi tuzitakase nafsi zetu kwa kutenda mema asaa Allah(s.w) nasi akatuinua daraja.Allah hawaongoi na kuwapokelea maombi watu madhalimu. Aidha uongofu haupatikani kwa kumwonea husuda na kijicho mwenye kufanya mema. Bali kwa kujitakasa na kufanya amali njema.


……….Akasema (yule asiyokubaliwa sadaka yake) nitakuwa” Akasema (yule aliyeaahidiwa kuuawa) “Mwenyezi Mungu huwapokealea wamchao tu.” (5:27)Vile vile Uislamu unatutaka tusiwe ni wenye kulipiza ubaya juu ya ubaya tunaotendewa. Mtu anatakiwa ajitetee na awatetee wengine dhulma inapotaka kufanyika. Lakini asipike uovu dhidi ya wengine. Bali amuogope Allah(s.w) na kushika njia iliyo sawa:“Kama utanyosha mkono wako kwangu kuniua; mimi sitakuyooshea mkono wangu kukuua, hakika mimi namwongopa Mwenyezi. Mola wa walimwengu pia.” (5:28)                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 578


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Tamko la suluhu baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUJENGWA UPYA KWA AL-KA'BAH (NYUMBA TUKUFU YA ALLAH)
KUJENGWA UPYA KWA AL-KA’ABAHItambulike kuwa Al-ka’abah ndio mjengo wa kwanza kujengwa duniani. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII MUSA(A.S) NA HARUN(A.S)
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

Kukomeshwa kwa Riddah na Chokochoko Nyingine katika dola ya kiislamu
Soma Zaidi...

Nasaba ya mtume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Waliomshambulia na kumuuwa Ali, makhawariji na si muawiya
Soma Zaidi...

Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu
Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Ibrahiim(a.s)
Soma Zaidi...

Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII ADAM
Soma Zaidi...

Vitimbi vya Wapinzani Dhidi ya Ujumbe wa Nabii Shu’ayb(a.s)
Kama ilivyokuwa katika kaumu zilizotangulia, waliomuamini Shu’ayb(a. Soma Zaidi...