Utajiri wa baba na kifo chake


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani


UTAJIRI WA BABA NA KIFO CHAKE.

Baba yangu akawa tajiri kwa ghafla. Utajiri wa baba haukumfanya abadili tabia. Siku zote aliendelea kuwa mkarimu kwa watu wote. Aliamini kuwa utajiri ule amepewa na Mwenyezi Mungu kwa sababu maalumu. Baba aliwawezesha na ndugu zake kwa kuwapatia mali alizo nazo. Jina la baba lilibadilika na kuwa muheshimiwa. Utajiri wa baba haukumfanya akose amni kama walivyo matajiri wengine.

 

Baada ya miaka kadhaa baba alifariki na mimi ndiye nikarithi mai za baba yangu. Baba zangu wadogo walikuwa ni wafanyabiashara wa kusafiri maeneo mbalimbali. Sikumoja na mimi nilivutiwa kwenda Yemeni nikiamini huenda nikakutana na wale wageni wa baba wanipe ushauri. Nilisafiri kwa muda wa masiku na hatimaye nikafika. Nikakodi nyumba ya wageni, na kulipia kodi ya miezi kama mitatu.

 

Sikuwa nikifanya bishara nilikuwa nikitumia tu pesa niliyonayo. Nyumbani biashara zangu niliachia ndugu zangu na baba zangu. Nilipokuwa nimekaa kwenye mgahawa alikuja binti mmoja hivi mrefu na mwembaba. Urefu wake haukunizidi mimi na alikuwa mweupe wa wastani. Alikuwa na nywele ndefu na nyusi nyeusi sana. Hakuwa na kope ndefu kama wahindi wa vijijini. Alivaa hijabu ndefu iliyofunika kifua chake. Miinuko miwili iliweza kuonekana kwa mbali kwenye kifua chake. Hakuwa amefunika sura yake, hivyo nikapata muda wa kumtazama vyema, midomo nywekundu, yenye kutengeneza tabasamu pana.

 

Alikuja na kunong’onezana na mama muuza mgahawa. Sikupatapo kusikia sauti yake. Alipomaliza akaondoka zake. Uwepo wake haukusumbua akili yanngu hata kidogo maana nilijisemea hapa mjini ninaweza kulizwa sasahivi. Ijapokuwa nilikuwa namkumbuka lakini wala sikuwaza hata kidogo. Sikumoja nilipokuwa nikinunua farasi kwa ajili ya kutembelea nilipungukiwa na pesa. Nikiwa naomba nipunguziwe ghafla akanieleza kuwa nimelipiwa tayari.

 

Sikuamini nikauliza nani amenilipia, nikaonyeshwa nikamuona ni yule binti wa jana. Sikutaka kujuwa mengi zaidi maana nilifikri huenda ukawa ni mtego wa mimi kuliwa pesa apa mjini. Nikatoa kiasi nilicho nacho na kilichobaki nio nikamwambia huyo aiyenilipia atamaliza. Niliamini kuwa siku yeyote akihitaji pesa yake nitaweza kuilipa. Nilijiuliza inakuweje mtu asiyekujuwa anakulipia mapesa mengi.

 

Sikumoja nikaelekea kwa kadhi wa mji kwenda kumuomba ushauri kuhusu mambo ya kishria biashara halali na haramu. Nilikuwa natamani kuanzisha biashara ya kuuza viatu vya ngozi. Nikataka kujuwa kama naweza kutumia ngozi ya wanyama wasioliwa, kama chui na viatu vile nikaruhusiwa kuingia navyo kwenye nyumba ya ibada. Nilipofika kwa kadhi nkaelezwa kuwa kadhi ana mgeni. Nikaambiwa mgeni ni meya wa mji ana mazungumzo hivyo nirudi baadaye kidogo. Nilizunguka na baadaye niliporudi nikapishana na watu wawili wanatoka kwa kadhi.

 

Mtu mmoja alikuwa ni mwanaume mzee wa makamo aliyepaka hina ndevu zake. Na mwingine alikuwa ni yule binti. Niliwasalimia wote kwa pamoja salamu alykum yaani “Amani iwe juu yenu” wakaitukia waalykum salaam yaani “Na wewe pia amani iwe juu yako”. ghafla moyo ulinidunda mara tu baada ya kusikia sauti ile. Sikujuwa maradhi gani niliyo nayo. Nilipenda sauti ile hasa kwa kuwa namfahamu kidogo mwenye sauti ile.

 

Nikafika kwa kadhi na kumueleza shida yangu. Kadhi alinijibu kuwa inawezekana na bishara hiyo ni halali kabisa. Hivyo kwa pesa niliyo nayoo nikaanza kuweka ahadi kwa wawindaji na washonaji viatu. Baada ya wiki 2 nikawa na hazina ya viatu vingi sana vya ngozi vilivyo katika maumbo mazuri sana. Nilianza kuuza mwenyewe ili kuweza kulifahamu soko. Nikaanza kutengeneza jina kwa ubora wa viatu vyangu.

 

Katika duka langu nikaweza sehemu kwa ajili ya watu waheshima. Niliamini kuwa matajiri na watoto wa mabosi hawaji kwangu kwa sababu hawataki kuchanganyika na watu wa kawaida. Nikaweka chumba ambacho bei zake zilikuwa za juu ijapokuwa bidhaa ni ile ile na ubora uleule. Niliamini kuwa sikuzote matajiri hawapendei kuwa sawa namasikini. Kitu nilichowabadilishia ni rangi na uwezo wa kuweka oda kwanzia wiki mpaka mwezi.

 

Jina langu lilikuwa na bidhaa zangu ziliendwa. Sikumoja alikuja mteja wangu, ni yule binti niliyemuonaga. Binti hakufuata viatu ila alitaka kuweka oda ya viatu kwa mtindo autakao yeye. Alitaka viatu vpea tata. Pea moja iwe na umbo la kichwa cha mamba, pea moja iwe na picha ya kichwa cha kunguru na peya nyingine iwe na umbo la kichwa cha kambale. Moyo ulinidunda na kuchanganyikiwa kwa nini anaeleza sifa zinazohusiana na wageni wa ajabu. Wageni ninaowatafuta. Nikaamini kuwa makutano yangu na binti huyu hata si ya kawaida. Bila shaka kuna jambo.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    2 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Kukatwa mkono na kuurithi utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Nani muuaji?
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu muuaji wa mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Mshenga wa aladini mbele ya mfalme kwa mara ya pili
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi ya chongo wa kwanza mtoto wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Post hii inahusu zaidi hadithi ya vijana wawili ambapo mitihani inaisha na wanaanza kuhukumiwa mmoja baada ya mwingine. Soma Zaidi...

image Hadithi ya Kaka wa pili wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya vijana wawili, kuhusu hadithi hii ni pale Jackie anaandikiwa barua na Julius ili apotezwe akili na wavulana wengine kwa sababu Jackie aliwapita darasani. Soma Zaidi...

image Upendo uliotafsiriwa kwa michoro
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Hadithi ya Kaka wa tano wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...