Hadithi ya tunda la tufaha (epo)


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela


HADITI YA TUNDA LA TUFAHA (EPO)

Khalifa Harun Rashidi alikuwa ana tabia ya kutembea usiku kuchunguza habari zinazofanyika wakati wa kiza katika utawala wake. Alikuwa akitembea yeeye na waziri wake Mansur pamoja nna mjakazi mmoja. Sikumoja katia matembezi yao walikutana na bwana mmoja ambaye alikuwa akiilaumu sana nafsi yake kwa kuwa masikini. Alikuwa akizungumza maneno ambayo hakupaswa luzungumza hata ikafikia akawa anamlaumu Mwenyezi Mungu. Khalifa alipolina jambo hilo akamuagiza waziri Mansuri aende akamuulize mtu yule hasa nini kilichomkuta.

 

Wazizi alipomuendea mtu yule na kujitambulisha waziri akapata habari kuwa yule bwana ni mvuvi. Na ana familia kubwa nayomtegemea. Lakini leo amekwenda kuvua bila kupata kitu chochote, na familia yake haikweza kula kitu chochote toka asubuhi, sasa anailaumunafsi yake pamoja na Mwenyezi mungu kwa kuwa yeye ni masikini.basi khalifa akamuagiza tena Mansuri nenda ukamueleze kuwa nitarudi naye baharini na chochote atakachokivua nitakinunua kwa vipande 100 vya dhahabu. Mvuvi kupata habari hizo alifurahi sana.

 

Basi walitoka khalifa na watu wake pamoja na mvubi, walipofika baharini mvuvi akawza mambo sawa na kurusha nyavu yake. Baada ya muda akaanza kuvuta nyavu. Loo! Nyavu ni mzito sana. Mvuvi alijuwa saa ni samaki mkubwa sana amevua. Baada ya kumaliza kuivuta nyavu Loo! Hakuwa ni samaki bali ni boksi kubwa la mbao. Mvuvi alipovua hakutaka kujuwa mengi alilikabdhi kwa Khalifa na akakabidhiwa pesa yake vopande 100 vya dhahabu.

 

Khalifa na kundi lake wakaondoka na boksi lao. Walipofika nyumbani wakaalifungua kwa mbinde sana. Ndani wakakuta likapu kubwa la minyaa. Ndani ya likapu wakakuta vundu kubwa lililofungwa kwa nguo nzri ya hariri. Bundu hili lilikuwa limejaa damu. Baada ya kulifungua bundu wakakuta kichwa cha mwanamke mzuuri huku viungi vya mwanamke huyo vikiwa vimekatwa katwa vipande vidogovido. Khalifa alshangaa zana “kweli katika uongoziwa ngu huu inawezekana mtu kuuliwa kwa kifo kama hiki na kutupwa majini na mimi sultani nisiwe na habari? Sasa mansur waziri ninakutaka uniletee aliyefanya kitendo hiki.

 

Mansur moyo ulimruka ghafla, kwa kuwaza kuwa mimi na khalifa wote tulikuwa pamoja, sasa ananitupia mimi mzigo wa lawama. Khalifa akazungumza tena “na endapo hutaaniletea mtu huyu nitakuuwa mbele ya hadhara ya watu wewe na watu 40 kutoka katika ukoo wako” Mansuri aliposikia maneno yale alizidi kuchanganyikiwa. Mansuri akaomba apewe siku tatu. Hapo khalifa akakubaliana. Mansuri alipofika kwake hakujuwa vipi ataanza. Basi akabakia nyumbani kwake kwa siku 3 bila ya kufanya kitu chochote. Siku ya tatu mjumbe kutoka ikula akaja na kumueleza mansur kuwa anahitajika haraka iwezekanavyo mbele ya khalifa akiwa na mtuhumiwa.

 

Mansuri hakufanya chochote hivyo akaenda mbele ya khalifa kichwa kitupu. Khalifa alikuwa ni mtu mwenye msimamo sana nna asiye tetreka. Khalifa alipomuona Mansur akiwa mtupu akaagiza afungiwe ndani. Mbiu kubwa ikapigwa na kutaarifu watu wote waje sokoni kesho ili wajepata kumuona waziri mansuri anapochinjwa yeye na watu 40 kutoka katika ukoo wake. Basi hapo askari wakaagizwa kenda kukamata yeyote katika ndugu wa mansur watakayempata. Idadi ilipotimia wote wakawekwa ndani.

 

Siku ya kuchinjwa ikafika, Mansur na wenziwe wakawekwa kitanzini. Tayari wachinjaji wakaja mbele na kusubiri oda. Hapo kiongozi wa tukio akawasomea shitaka lao “mansur unahukumiwa kifo kwa kosa la kutokumleta muuwaji aliyemuuwa Binti mmoja na kumtia kwenye boksi na kumtupa kwenye maji unahukumiwa kifo wewe na watu 40 kutoka katika kabila lako iwe ni fundisho kwa watu wa sasa na wajao.

 

Wakati mchinjaji anataka kuanza, ghafla mzee mmoja akatokea na kusema “tafadhali usimuuwe mansur bali niuwe mimi maana mimi ndiye muuwaji, niliyemuuwa huyo bint” Loo hapo mansur alifurahi sana kuona saa amepona. Hapo yule mzee akakamatwa. Kabla ya mambo kuendelea zaidi ijana mmoja mtanashati akaja mbele na kusema kuwa “tafdhali kiongozi, usimuuwe huyo mze, kwani yye hana kosa. Mimi ndiye muuwaji wa huyo binti. Basi ikawa kila mmoja anadai kuwa ndiye muuwaji. Hapo kiongozi akaamuwa kesi aipeleke kwa khalifa tena.

 

Basi kundi la watu watatu likiongozwa na kiongozi wa uchinjaji wa watuhumiwa sugu.Mbele ya Khalifa wakaendelea kubisha na kila mmoja akaidai kuwa yeye ndiye muuwaji. Hapo Khalifa akataka kijana afafanue zaidi. Kijana akasema kuwa amemuuwa huyo binti na kumkata vipande na kuvifunga kwenye bundu lla nguo ya hariri kisha kumtia kwenye likapu kubwa na kuliweka kwenye boksi kubwa. Na kisha kulitupia kwenye maji. Hapo khalifa akajiridhisha kuwa ni kweli kijana ndiye muuwaji. Khalifa akampa nafasi kijana aelezee kwa nini alimuuwa huyo binti?



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    2 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    3 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani offline    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Hadithi ya tabibu wa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Utajiri wa baba na kifo chake
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image Usuluhishaji wa walio dhurumiwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Ndoa ya Siri yafanyika
Posti hii inakwenda kukuendelezea hadithi kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Hadithi ya Mama mchoyo na mwehu
Posti hii inahusu zaidi habari za Mama mmoja aliyekuwa mchoyo akampa mkate mwehu na kuutia Sumu ila kwa sababu mwehu alikuwa mkarimu sana aliutunza mkate na kuwapatia watoto wa yule mama waliokuwa wakitoka shule na njaa kali Soma Zaidi...

image Hadithi ya jini na mfanya biashara
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya mke na kasuku
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya mahusiano ya vijana wawili baada ya kuhamia shule mpya. Soma Zaidi...

image Hadithi ya samaki wa Rangi nne
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya mji uliogeuzwa mawe
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...