image

KWA NINI DIRISHA MOJA?

KWA NINI DIRISHA MOJA?

KWA NINI DIRISHA MOJA?


KWA NINI DIRISHA MOJA?Siku hiyo Aladini aliamka mapema, na kuelekea sehemu ya kuogea. Aliridhishwa vyema na usafi wa chooni na alivyovikuta. Alifanya usafi wa mwili wake, huku akimuacha binti Sultani akiwa bado amelala kwa uchovu wa pirikapirika za jana nzima. Baadaye binti mfalme aliamka na kufanya usafi kisha wote wakaelekea kupata kifungua kinywa. Wote walikuwa wamevaa pete sawa kwa rangi. Pete zilizokuwa za dhahabu huki vichwa vya pete vilikuwa ni almasi yenye kichwa cha yule ndege wao. Mama Aladini alipowaona watoto wake machozi ya furaha yalimtoka, hata akatamani mzee Mustapha angelikuwa hai siku kama ya leo.


Kama mfalme alivyoahidi, alifunga safara wake na matarumbeta yake kwenda nyumbani kwa Aladini. Walijipanga wananchi kwa kumuheshimu mfalme wao kila alipopita. Haukuchukuwa muda mrefu saana, hatimaye msafara ukawa nje ya jumba kubwala Aladini. Halikuwa ni umba la gorofa matarumbeta yote yalinyamaza punde sauti za kasuku zilipoanza kusiika. Sauti zilizidi uzuri wa matarumbeta. Mfalme alifurahi na kutabasamu. Sharubu za mfalme zilipepea vyema kwenye upepo mwanana mbele ya miti ya mauwa na matunda nyumbani kwa Aladini.


Macho ya mfalme yakaelekea kwenye ukuta wa jumba hili, na baada ya kujidhisha kwa uzuri ulioje ghafla mfalme akakaza macho a sura. Pale alipoona dirisha moja. Mfalme alimlaumu Aladini kwenye nafsi yake. Mfalme alimlaumu na kuwaza laiti kama angeliishiwa na pesa ya wajenzi ama vifaa angelinambia tu ningemtekelezea. Wakati haya yanaendelea kutokea Aladini, mkewe na Mama yake wakaja kuwapokea. Ilikuwa ni furaha juu ya furaha. Msafara ukaingia ndani na mjakazi mukuu akaendelea kupanga kila mtu kumpa majukumu yake. Kisha mfalme akaa kupata chakula. Na mazungumzo ya hapa na pale yakaanza.


Mfalme alionyesha kuridhika sana na ubora wa nyumba na wajenzi. Wakiwa wanazungumza hapa na pale binti mfalme alikuwa anahisi kitu kwa baba yake kana kwamba ana jambo anataka kulisema. Binti akaanza kumdadisi baba. Hatimaye mfalme akafunguka. “baba umejenga jumba zuri sana ila sikuridhishwa na dirishao majo., baba uliishiwa na wajenzi ama vifaa”? “baba nimewacha kusudi ili na wew utie baraka zako, umalizie dirisha lile iwe sifa kuwa hata mfalme amechangia katiaka ujenzi” ni majibu ya Aladini. Mfalme alifurai sana na kuona kumbe mkwe wake anampenda sana. Basi mfalme akaahidi kuanza kazi kesho kuleta wajenzi.


Mazungumzo yaliendelea na baadaye mama Aladini akajiunga na mazungumzo kisha Mama Aladini akaondoka na binti mfalme. Hapo mfalme akapata fursa ya kuwa pekee na mkwewe. Wakatoka nje na kuendelea kupata upepo na kuzungumza kwa undani. Walizungumza sana hata mfalme akazungumza ya moyoni kabisa kuwa anatarajia kupata mjukuu apema. Na oia Aladini ajiandae kuwa mfalme ajae pindi atakapo fariki. Basi ilkuwa ji furaha juu ya furaha. Ilipofika jioni Mfalme akarudi kwake ikulu. Waliangana kwa ucheshi sana hasa mama Aladini na Mfalme walikuwa kama dada na kaka sasa.


Baada ya mfalme kuondoka mama Aladini naye akaaga kuondoka kurudi kwake. Aladini ijapokuwa liamsihi sana mama yake waishi wote lakini mama alikataa. Watu wote walipondoka aladini alibaki yeye na mkewe na wafanyakazi. Aladini aliuweka mshumaa wake juu ya meza na kumwambia mkewe asijeutoa mshumaa ule. Lakini hakumwambia siri hasa ya mshumaa ule. Pia Aladini alikuwa navaa pete mbili moja ile ilofanana na mkewe na nyingine ni ile pete ya ajabu. Pia hakumwambia mkewe siri ya pete ile. Hata hivyo mkewe hakuonyehsa kutaka kujuwa chochote katika vitu hivi.


Siku ilofata mfalme alileta mafundi kujenga bila mafanikio. Hawakuwa na ujuzi hata hivyo hawakuwa na vifaa pia. Nchi nzima ilitafutwa madini yaliyoweza kurekebisha dirisha bila kupatikana. Hatimaye mfalme akakiri kushndwa kazi. Basi kwa Aladini haikuwa ni kazi kubwa. Ilikuwa ni kazi ya usiku mmoja chini ya nguvu ya jini wa mshumaa. Asubuhi dirisha lkawa safi. Basi maisha yaliendelea kwenda hatimaye miezi kadhaa ikapiata. Aladinia kawa anakwenda kuwinda na mkwewe kujifurahisha.


Maendeleo ya Aladini yaliweza kushangaza uma na hayakuweza kuridiwa na watu wote. Mmoja wapo alikuwa ni waziri mkuu. Ambaye mpaka sasa alipo hakujulikani. Ukweli ni kuwa baada ya tukio la ndoa ya Aladini waziri aliondoka kwenda kutafuta siri ya aladini. Waziri alifika mbali sana mpaka nchi za Afrika huko alikutana na mchawi mkubwa sana. Mchawi huyo ndiye aliyetoa siri nzima ya Aladini na maisha yake. Waziri mkuu alimpatia mchawi hongo kubwa sana ili ahakikishe kuwa Aladini anapotea, na anapata aibu kubwa na udhalili.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 222


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA KAKA WA SITA WA KINYOZI
Soma Zaidi...

HADITHI YA KILEMA WA VIUNGO
HADITHI YA KILEMA, MTANASHATI ASIYE NA MKONO Basi tambu kuwa mimi ni Mtu wa Baghadad na ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabishara mkubwa sana. Soma Zaidi...

Mtihani penzini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Kwa nini vidole vimekatwa
HADITHI YA ALIYEKATWA VIDOLE GUMBA Mimi nilikuwa mfanyabiashara mdogo sana, katika mji wa Baghdad. Soma Zaidi...

HARUSI YA ALADINI NA BINTI SULTANI
Soma Zaidi...

MUENDELEZO WA HADITHI YA MSHONA NGUO
Soma Zaidi...

Historia ya zamani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Wagen wa Ajabu
UJIO WA WAGENI WA BARAKA. Soma Zaidi...

Hadithi ya tunda la tufaha (epo)
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na kijakazi wa sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Familia mpya baada ya harusi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...