Hadithi ya mjakazi wa Mfalme

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika.

Hadithi ya mjakazi wa Mfalme

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI
Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika. Tulikuwa tupo kwenye tafrija moja hivi jana wakati wa jioni kabla ya juwa kuzama. Katik tafrija hiyo tulipata kusikiliza usomaji wa quran kwa sauti nzuri sana hata machozi yakatutoka. Baada ya hapo tukabahatika kusikiliza mashiri. Mshairi maarufu kutokea India alikuwepo, na alighani kwa sauti njema sana.Baada ya burudani kuisha ndipo tukaletewa chakula kizuri sana. Vyakula vya kuoka, na nyama iliyo kaushwa vizuri ililetwa bele ya hadhara. Vinywaji vilivyo vizuri vikahudhurishwa mbele yetu. Basi tulikaa vikundi vikundi kuzunguruka sahani za vyakula. Katika kundi nililokaa nilikuwa na aliyekuwa na shughuli yake siku ile. Na hapa kitu cha kushangaza ndipo kikatokea.Katika vyakula vilivyoletwa kulikuwepo na zerbajeh. Hiki ni chakula zilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa vyakula kadhaa na matunda. Chakula hiki unapokila harufu yake inaweza kukaa kwa muda wa siku nzima kwenye mikono. Ni chakula kitamu na kipendwacho na watu wa Baghadad. Basi ghafla mwenzetu mmoja alipoona chakula kile akaanza kutetemeka na kutokwa na majasho kana kwamba ameona kitu cha kutisha sana.Yule bwana hakutaka hata kula chakula kile. Sikuwa na wasiwasi sana nikajuwa lamda hali chakula kile, ama lamda kuna mtu anamdai ndio maana akapata woga. Wakati tunakula nikamuona yule bwana kidolechake gumba kimekatwa. Alipokuwa nakata nyama, nikagundua vidole vyake gumba vya mikono vyote vimekatwa. Hapo nilishindwa kujizuia kuwa na shauku, nikataka kumuuliza kulikoni. Lakini ikabidi nimsubiri amalize kula.Kumbe wakati ule hata yule mwenye shughuli yake alikuwa anashuhudia yanayotokea. Alikuwa akinisubiri nianza kuuliza. Kwa kuwa yeye ndiye mwenye shughuli isingekuwa vyeka kumkera mgebi wake. Ndipo naye akasubiri amalize kula ili amuulize. Yule bwana alipomaliza kula nikamuuliza 'ndugu yangu nimeona hata huugusa chakula hiki 'zerbajeh' ama hukupendi' naye akajibu 'ninakipenda ila baada ya kula ni lazima nioshe mikono yangu mara 40 kwa maji, mara 40 kwa alita na mara 40 kwa sabuni. Sasa vitu hivi hapa havipo na si vyema kusumbuwa watu kwenye shughuli hii'Kwa shauku zaidi nikamuuliza ana nini hasa. Ndipo akanieeza kuwa chakula hiki ndio sababu ya yeye kukatwa vidole gumba vya mkono wake. Kisha akatuonyesha na vidole kumba vya miguu yake, pia vimekatwa. Hapo nikapata shauku zaidi kujuwa hasa kwa nini amekatwa vidole gumba vyake vyote vinne kwa sababu ya chakula tu.Wakati mazungumzo yetu haya yanaendelea yule bwana Mansur mwenye shughuli yake alikuwa anasikiliza. Basi akaagizwa kuletwe ndoo mbili za maji, sabuni na alita. Hapo kopo la kunawia na alita zikaandaliwa kwa ajili ya kutoa povu vyema. Kisha ikaletwa tena sahani yenye zerbajeh. Akaambiwa ale kisha atanawa kama anavyotaka. Basi akala vyema akanywa maji na kumshukuru Mungu. Kisha akaanza kunawa na alita mara 40 kisha sabuni mara 40 kisha maji mara 40. alipomaliza tukamtaka atusimulie hadithi yake ndipo akasimulia hadithi ifuatayo:-Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 158

Post zifazofanana:-

HADITHI YA TABIBU NA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA TABIBU WA MFALME Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Soma Zaidi...

alif lela u lela
Download kitabu Hiki Bofya hapa Kupata mwendelezo wa hadithi hii Download App yetu. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 17
5. Soma Zaidi...

SHAIRI KUTOA NI USHUJAA
KUTOA NI USHUJAA KUTOA NI USHUJAASalamu kwanza awali, wasikizi tikieni, Mwambaje nazenu hali, kheri nawatakieni, Mungu awape sahali, muifuzu mitihani, Kutoa niushujaa, ubakhili nitamaa,Kila alie akili, hutunza yake thamani, Hilo sote twakubali Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA KITABU CHA TATU: HADITHI YA NURDINI
Soma Zaidi...

Sababu ya kukatwa vidole gumba
KWA NINI VIDOLE GUMBA VILIKATWA? Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 12
8. Soma Zaidi...

SABABU YA NENO LAKO
Sababu ya neno lako, nasema nimesikia,Sababu ya neno lako, nasema hongera pia,Sababu ya neno lako, nishajua yakonia,Wasema afukuzwae, sihadi pasemwe toka,Sababu ya neno lako, maumivu yanijia,Sababu ya neno lako, nami leo nakwambia,Sababu ya neno lako, sit Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME
Soma Zaidi...

MAAJABU YA MBU
7. Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 22
4. Soma Zaidi...

ALADINI NA BINTI WA MFALME.
ALADINI NA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...