image

Binti huyu Ni Nani?

Posti hii inakwenda kukuendelezea hadithi kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultan

BINTI HUYU NI NANI?

Siku iliyofuata nilioga mapema, kisha nikavaa ngu zangu safi na kuelekea pale dukani. Loo! Yule binti akaja tena, alipokuja moja kwa moja akakaa karibu nami na kutoa kitambaa kilichofungwa bundu. Kisha akaniambia “ Chukuwa hii malipo yako kwa bidhaa yako siku ya jana”. nikachukuwa na kumpatia muuzaji wangu ahifadhi. Sikuwa na haja ya kuhakiki kama pesa imetimia ama laa.

 

Basi nikaendelea kuzungumza naye maneno ya hapa na pale. Kisha nikaanza kuchomekea maneno ya ishara. Bila shaka alizifahamu vyema ishara zangu. Kwa ghafla alionyesha kukasirika na ndipo alisimama na kuondoka zake. Nilijijutia nafsi yangu kwa nini nimeongea naye kwa ishara za mapenzi. Aliondoka tena bila hata kuniambia anaitwa nani na wapi anakaa. Aluondoka hata sijazungumza hasa nini kipo moyoni kwangu.

 

Hakika siku hiyo niliiona ndefu sana na sikuweza kula chochote. Nilipata pia kujiwazia huenda binti yule sio mtu wa kawaida, huenda ni jini ama malaika ametumwa kuja kunijaribu. Siku ya tatu yake nikaamua kutembea mjini nkiamini huenda nikakutana naye kwa bahati mbaya. Loo! Sikuiliisha bila hata kukutana na sura yake.

 

Siku ya nne nilikaa kenye duka lile na ghafla akanijia bibi mmoja. Akanieleza kuwa ameagizwa na bosi wake aje anichukuwe ana mazungumzo. Bibi alikuwa ni mjakazi katika jumba la kitajiri. Nilifahamu hilo baada ya kuona mavazi yake. Nilikubali wito kwa kuamini atakuwa ni yule mrembo aliyeteka hsia zangu, aliyechukuwa moyo wangu, aliyenikosesha hamu ya kula wala kulala.

 

Niliongozana na bibi yule hata tukafika kwenye nyumba ya wageni. Hap akanieleza niingie kwani bosi wake yumbo ndani. Nilipoingia tu nikakaribishwa na manukato yanayonukia kwa uzuri sana, Loo! Alikuwa ni yule mrembo, alikuwa amependeza sana siku hii. Alvaa mavazi marefu yenye rangi za kuvitia kama tausi. Akanikaribisha kwnye busati lililotandika katikati ya chumba.

 

Hapo wakaja mabinti wengine wawili vigori, wakaleta vinywaji na kukaa pembeni. Akanieleza kuwa hawa pia ni wafanya kazi wake. Hawezi kukaa peke yake kwani faragha ya mwanaume na mwanamke wasio oana hairuhusiwi kwenye dini. Basi tulianza kuzungumza hapa na pale wakati huo mabinti wale wapo. Mwisho niamueleza uhalizi wa moyo wangu juu yake, ni kiasi gani ninampenda, ni taabu gani nimeipata kwa siku tatu hizi toka niutane naye.

 

Nilimueleza vyeote kuhusu kuwa sikuwa na usingizi wala sikuona tamu ya chakual. Wakati wote niliokuwa nachungumza yeye alikuwa akitokwa na machozi tuu. Moja wa mabinti wale akachukuwa kitambaa cha hariri kilicho zungushiwa na dhahabu nyekundu, na kutiwa manukato yanayonukia kama miski nyekundu ya kutoka india. Alimfuta machozi kisha akasema “ kwa hakika unayoyasema ndiyo yaliyomkuta bosi wetu, toka majuzi anakazi ya kukuwaza, kukutaja, kukufikiria, hali, halali, hanywi kwa upendo alionao kwako”.

 

Nilitamani kumfuta machozi ila nikaogopa kumvunjia heshima mbele ya wafanyakazi wake. Ndipo akasema kuwa “ kwa hakika walioyasema ndugu zangu ni sahihi, wewe ni mtu wa kwanza kukupenda, na amini nakupenda kweli, naomba tuoane. Kwani siwezi kukukosa tena, siwezi kuonja tena adhabu ya kuwa mbali nawe, uso wako kama lulu kwangu, katu sichoki kukutazama, tabasamu lako…… mmmhmmh nakupenda sana.”

 

Basi aliendelea kuzungumza kisha tukakubaliana kuwa tuoane ila ndoa iwe kwa siri kwa sababu, mimi ni mtu ambaye bado ni mgeni hivyo haitakuwa vyema kutangaza harusi yetu, na mimi ninatambulikamkwa utajiri nilio nao, hivyo wanaweza kukufanyia fitina, na hata kukuumiza. Siku ilofata ilikuwa ni ijumaa. Basi akanielekeza kwake ili niende baada ya kuswali ijumaa ili ndoa ikafanyike. Basi tukaagana pale na mimi nikaondoka na wao wakaelekea zao.

 

Sikuwa na haja tena ya kulijuwa jina lake maana niliamini kuwa nitalijuwa siku ya harusi. Nilijuwa kuwa yeye ni tajiri na ni mtoto wa tajiri. Niliamini ili niweze kuishi naye ni lazima nitumie pesa vyema. Basi siku hiyo sikuweza tena kulala kwa kuisubiri asubuhi ifike, ili nikamuoe kipenzi maridhawa.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1074


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

HADITHI YA KAKA WA NNE WA KINYOZI
Soma Zaidi...

Utajiri wa baba na kifo chake
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

JARIBIO LA KWANZA LA ALADINI
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kinyozi kaka wa kwanza
Soma Zaidi...

MSHENGA WA ALADINI MBELE YA MFALME KWA MARA YA PILI
Soma Zaidi...

Hadithi iliyosimuliwa na mshona nguo
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

HADITHI YA KILEMA WA VIUNGO
HADITHI YA KILEMA, MTANASHATI ASIYE NA MKONO Basi tambu kuwa mimi ni Mtu wa Baghadad na ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabishara mkubwa sana. Soma Zaidi...

HADITHI YA MLEVI
Soma Zaidi...

Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Harusi ya aladini na binti sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

KIFO CHA MTOA BURUDANI WA MFALME
Hapo zamani katika mi wa Baghadani wakati wa utawala wa Sultani Harun Rashid alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa karibu sana na Sultani kwa kuwa alikuwa akimpa burudani. Soma Zaidi...

KWA NINI DIRISHA MOJA?
KWA NINI DIRISHA MOJA? Soma Zaidi...