HATIMA YA KIJANA MCHONGANISHI
Mansur akaondoka haraka akiwa na majozi sana huku akiwaza nitampata wapi kijana huyu. Mansur alijisemea, Mungu aliyeniokoa na janga la kwanza ataniokoa na hili la pili. Mansuri alipofika kwake aliwaeleza kla kitu, na akabakia kwake kwa siku tatu bila kwenda kokote. Manzur ilipofika siku ya tatu akajiwa na mjumbe kutoka kwa khalifa kuwa anahitajika akiwa na muhalifu ama ajiandae kwa kifo. Mansur akaanza kuagana na famiia yake na kuacha usia.
Kabla ya kuondoka mwanae mdogo aliyekuwa akimpenda sana alikuja kumkumbatia baba yake kama ishara ya kuagana. Mansur wakati akimkumbatia mwanaye alihisi ugumu kwenye tumbo la mwanaye. Akamuuliza ameweka nini. Mtoto akajibu kuwa nimeweka tunda epo nimepewa na Manyakazi wetu, alikuwa hataki kunipa eti amemnyangโanya mtoto wa watu ambaye baba yake amekwenda mbali kununua maepo matatu kwa gharama ya vipande 15 vya dhahabu.
Mansur aliposikia habari hii alifurahi sana na kusema ssa nimeokoka. Hapo akamchukuwa mfanyakazi wake na kwenda naye kwa khalifa. Kijana akaulizwa na kukirikonsa. Khalifa akaagiza habari hii iandikwe kwa wino wa dhahabu na ihifadhiwe kwenye kumbukumbu ya nyaraka za kushangaza na kutisha. Kisha waziri Mansur akasema ewe khlifa ninakiri kuwa mfanyakazi wangu amepatwa na hatia. Ila ninakuomba kuwa nitakusimulia kisa cha kushangaza zaidi ya hiki, na endapo utakirikuwa kimeshangaza zaidi naomba iwe fidia umuache huru mfanyakazi wangu.
Khalifa alikubaliana na maneno haya na hapo Mansur akaanza kusimulia hadithi ya Badrudin.
Tukutane kitabu cha tatu hadithi ya badrudin
Huu ndio mwisho wa kitabu cha pili hadithi za Alif lela u lela. Usiwache kuwa nasi tukutane kitabu cha tatu. Kama unahitajikitabu cha kwanza na pili wasiliana nasi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukuletea hadithi ya kilema, mtanashati asiye na mkono
Soma Zaidi...MTIHANI PENZINI Sikuwa na wasiwasi maana niliamini kuwa nitafanikiwa tu.
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu
Soma Zaidi...HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika.
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela
Soma Zaidi...