Menu



Siku ya sita ya wageni

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

SIKU YA SITA YA WAGENI

Siku ya sita walianza mapema kama siku ya nne kisha wakamueleza baba awapeleke msituni. Baba aliwapeleka msituni maeneo yenye tembo. Baba alikuwa na lengo lake, akiamini kuwa kama watauwa tembo atapewa kichwa hivyo atauza meno na kupata pesa nyingi sana. Lakini wale mabwana walisha tambua hili, mmoja wao akasema “wala usitende wema kwa kutarajia malipo kwa mema wako, bali taka malipo kwa Mwenyezi Mungu”. nafsi yangu ilinisuta sana ila sikujali sana nilitambua kuwa ni kawaida yao. Haya ni maneno aliyojisemea baba.

 

Basi baba akawapeleka kwenye msitu wenye tembo. Wale mabwana walikuwa wanatumia mikuki, michale na mmoja wao alikuwa na bunduki iliyotengenezwa India. Niliitambua kutokana na hati ya maandish yaliyoandikwa. Basi baba akawapeleka kwenye msitu wenye tembo na akawapeleka sehemu ambapo tembo huwa wanapenda kunywa maji. Wale watu wakakaa sawa kwa kujiandaa kuwinda, ngafla kundi la tembo likaja. Baba akaanza kufurahia moyoni akidhani sasa utajiri unafata. Kitu cha ajabu mmojawao akapiga bunduki juu ili kuwatisha tembo.

 

Wale tembo wakakimbia na kubakiwa vinyama vijidogo. Baba akapata hasira moyoni lakini mmoja wa wale watu akasema “wala usikodolee macho kitu kilichopo kwa mwenzio”. muda si mrefu mamba wakaanza kuja mmoja kati ya wale watu akachukuwa mkuki na kumnyatia mamba na akapiga kwa nguvu. Mamba alitapatapa sana lakini wakafanikiwa kumvua. Nilianza kuhoji maswali mengi hata nikadhani wanataka kula mamba. Haya ni maneno ambayo baba alikuwa akiwaza.

 

Wakamtoa mamba na kumuandaa vyema na kuotoa sumu yake na kuifukia. Walipomaliza wakamkata kichwa na kumpatia baba. Yule mzee sana akasema “mamba huyu amezoea kula kambare wakubwa wanaojificha kwenye matope. Kihifadhi kichwa hiki mpaka siku ya miadi”. baba anasema niliwaacha kulekule baada ya kuniambia kuwa njia wanaijuwa hivyo watarudi wenyewe. Baba hakujuwa yule mamba wamemfanya nini alipokuja kichwa chake akakiweka tena sehemu nzuri. Wageni wetu tuliwasubiri hata ikafika usiku wa manane bila kutokea.

 

Baba akaamuwa aende kuwafatilia huenda wamepotea. Aliwakuta palepale alipowaacha, na walipomuona walimshukuru sana na kumuombea dua kwa ukarimu wake na kwa kujali kwake wageni. Wageni wakamweleze kuwa watalala pale asubuhi ndio wataonana. Basi baba akarudi na ilipofika subuhi wageni wakamwita baba uwani kwetu na kumwambia ahakikishe milango amefunga na hakuna mtu atakayesikiliza mazungumzo yao.

 

Baba ananieleza kuwa wakamwambia alete vichwa vile vitatu na kuviweka mbele yao. Wakakipasua kichwa cha kambale na kukuta alimeza dini la dhahamu kubwa. Kumbe madini yalikuwa yakihuka kwenye yale maporomoko ya maji na kwa kuwa makambale wanajitafutia chakula kwenye matope kwa bahati mbaya kambale yule alimeza dini nile na likamkwama kwenye kichwa chake. Baba akaambiwa auze dini lile na ndio zawadi yeke.

 

Walachukuwa kichwa cha kunguru na kukipasua wakatoa mkufu wa dhahabu. Wakamwambia auze mkufu ule baada ya mwaka mmoja. Maana mkufu ule ulikuwa ni mali ya msafiri mmoja ambaye alishawahi kusaidia na baba. Na mkufu ule aliusahau sehemu ambayo alilala siku moja baada ya kuondoka nyumbani. Kunguru yule aliubeba mkufu ule na ukamkwama kwenye koo lake. Wakamwambia kama baada ya mwaka hajatokea mwenyewe uza na utumie thamani yake.

 

Wakachukuwa kichwa cha mamba na kukipasua wakakuta kuna matope mengi sana.katika matope yale kulikuwa na madini ya dhahabu kadhaa. Wakamkabidhi tena baba na kumwambia hii ndio zawadi yako kwetu. Kishha wageni wakakusanya kila kilichochao na kuendelea na safari yao. Hatukupatapo kujuwa hata majina yao, wapi wametoka na wapi wanakwenda. Baada ya muda wa mwaka baba aliuza mali zile na hapo ndipo utajiri wetu ulipoanzia.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela2 Main: Post File: Download PDF Views 946

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Nani muuaji?

Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu muuaji wa mtoa burudani wa sultan

Soma Zaidi...
Hadithi ya Kaka wa tatu wa kinyozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
KIFO CHA MTOA BURUDANI WA MFALME

Hapo zamani katika mi wa Baghadani wakati wa utawala wa Sultani Harun Rashid alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa karibu sana na Sultani kwa kuwa alikuwa akimpa burudani.

Soma Zaidi...
ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KITABU CHA PILI HADITHI ZA ALIF LELA U LELA UFUPISHO WA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA.

Soma Zaidi...
Hadithi ya kinyozi yeye mwenyew

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani

Soma Zaidi...
Binti huyu Ni Nani?

Posti hii inakwenda kukuendelezea hadithi kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultan

Soma Zaidi...