Post hii inahusu zaidi upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo dalili zake na namna ya kumsaidia mgonjwa mwenye tatizo hilo.
Upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo na dalili zake na jinsi ya kuzuia.
1. Upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo, utokea sana kwa watu wanaoishi sehemu za ziwani au kwenye majimaji mbalimbali na mnyoo huyo kwa kitaalamu huitwa Necatir Americans na Aina hii ya upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo huitwa Hookworms Anemea.
Dalili za mgonjwa wa Anemia inayosababishwa na minyoo.
-ukifunua kwenye jicho utakuta Kuna weupe na kiasi kidogo Cha damu kinachoonekana na kama damu Iko kidogo jicho uonekana jeupe kabisa na pia kwenye mikono huwa nyeupe kuliko kawaida na hivyo hivyo kwenye ulimi hali ya ulimi uwa nyeupe kuliko kawaida na midomoni hasa kwenye lips napi pia uwa peupe.
2. Mgonjwa wa kupungukiwa damu usikia uchovu, hii ni kwa sababu damu ndiyo inayohusika na kusafisha chakula pamoja na hewa ya oksijeni kwa hiyo vitu hivyo vikikosa mwilini na kuwepo kwa kiwango kidogo lazima mwili utakosa chakula na hewa itakuwa ndogo kwa hiyo mtu ataanza kusikia uchovu mara kwa mara na kushindwa kufanya kazi zake za kila siku hatimaye kama damu haitaongezewa haraka anaweza kuzimia .
3.Dalili za moyo kushindwa kufanya kazi ujitokeza.
Hii ni pamoja na mapigo ya moyo kubadilika yanaweza kwenda mbio kwa Sababu ya kutumia nguvu kusukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili kuliko kawaida kwa sababu damu haifiki sehemu zote na siyo ya kutosha kwa hiyo moyo utumia nguvu Ili kusfilisha damu kila mahali hali ambayo usababisha mishipa ya damu kupasuka na kusababisha madhara makubwa.
4. Kiasi Cha madini ya chuma kupungua.
Kama mtu ana upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo kiasi Cha madini ya chuma upungua kwa kiasi kikubwa kwenye damu hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa minyoo kwenye mwili ambao usababisha kupungua kwa madini ya chuma.
5. Kupumua kwa shida.
Kupumua kwa shida utokea kwa sababu ya kutokuwepo kwa hewa ya kutosha kwenye damu, tukumbuke kuwa kazi ya damu ni kubeba hewa kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu mbalimbali za mwili na kwa sababu ya maambukizi hewa haitoshi kwa hiyo lazima mgonjwa atapumua kwa shida kwa sababu ya kutokuwepo kwa hewa ya kutosha kwenye mwili.
6.Mapigo ya moyo upungua.
Kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye mwili na idadi ya damu kwenye mwili ni kidogo na mapigo ya moyo upungua kwa sababu ya kupungua kwa kiwango Cha damu mwilini.
Angalisho:tunajua kuwa damu ni muhimu mwilini na ikipungua ni hatari sana kwenye mwili kwa hiyo tuwe makini ikiwa damu itapungua kuliko kawaida na tule vyakula vya kuongeza damu na pia tutumie sana dawa za kuua minyoo inayosababishwa upungufu wa damu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowPosti hii inazungumzia dalili na namna ya kujikinga tusipate mafua .mafua kwa jina lingine hujulikana Kama baridi ya kawaida (common cold).baridi ya kawaida husababishwa na virusi kwenye pua na hutoa makamasi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza na kuonyesha kwamba moyo umetanuka.
Soma Zaidi...Kuharisha ni Hali ya kupitisha kinyesi Cha maji chenye damu au kisicho na damu
Soma Zaidi...Malaria husababishwa na vijidudu vidogo parasite wanaojulikana kama plasmodium. Vijidudu hivi hubebwa na mbu aina ya anophelesi. Kuna ina nyingi za plasmodium lakini aina 5 tu ndizo husababisha malaria
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi ambayo kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili inashuka.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Sababu za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, hali hii uwatokea sana wanawake zaidi ya wanaume, kwa kitaalamu hali hii ya kuwa na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo huitwa cystitis.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya Tiba homoni, ni madhara- ambayo utokea kwa mgonjwa anayetumia homoni kama Tiba kwenye kutibu saratani.
Soma Zaidi...Uchovu wa joto ni hali ambayo dalili zake zinaweza kujumuisha kutokwa na jasho kubwa na mapigo ya haraka, ambayo ni matokeo ya joto la mwili wako. Ni mojawapo ya magonjwa matatu yanayohusiana na joto, huku tumbo la joto likiwa kali zaidi na Kihar
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya fikra potofu kuhusu vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...