Ujuwe mlo sahihi kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo
Post hii itakwenda kuangalia mlo sahihi wa mwenye vidonda vya tumbo. Hata utajifunza ni vyakula vipi hapaswi kula na vipi ana paswa kula.
VYAKULA VYA KUVIEPUKA KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo ni nini?
Vidonda vya tumbo ni aina za vidonda ambavyo hutokea kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vidonda vivi vinaweza kutokea kwenye tumbo ama utumbo. Hata hivyo koo la chakula linaweza kuathirika kupata vidonda, jambo hatuviiti vidonda vya tumbo. Vidonda vya tumbo vinaweza kuleta maumivu makali sana ya tumbo na mara nyingi hutokea wakati mtu ana njaa.
Nini husababisha vidonda vya tumbo?
Sababu kuu ya kutokea kwa vidonda vya tumbo ni mashambulizi ya bakteria wanaojulikana kama Helicobacter pylor (H.pylor). bakteria hawa wanaishi kwenye tumbo. Mtu anaweza kuishi na bakteria hawa kwa miaka kwa miaka mingi bila ya kusabbabisha madhara yeyote yale. Lakini si mara zote, bakteria hawa wanaweza kusababisha kuvimba (inflamation) kwenye kuta za tumbo, na kupelekea kutokea kwa michubuko na hatimaye vidonda vya tumbo. Vingine vinavyosababisha vidonda vya tumbo ni kama:-
- Misongo ya mawazo
- Ongezeko la uzalishwaji wa tindikali tumboni
- Matumizi mabaya ya dawa
- Saratani ya tumbo
Dalili za vidonda vya tumbo
Maumivu ya vidonda vya tumbo ni makali, pia mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kupatwa na changamoto nyingine ambazo ni katika dalili za vidonda vya tumbo. Kwa mfano kutapika, kiungulia cha mara kwa mara, tumbo kujaa gesi, maumivu ya kifua, kupungua kwa damu na uzito. Endapo vidonda vya tumbo vitadumu kwa muda mrefu bila ya kupatiwa matibabu afya ya mgonjwa inaweza kuwa mbaya ijapokuwa vidonda vya tumbo havisababishi kifo.
Vipi nitatuliza maumivu?
Unaweza kutuliza maumivu ya vidonda vya tumbo kwa kutumia dawa za hospitali. Pia kwa kutumia dawa za kienyeji pia. Lakini unaweza kutuliza maumivu haya kwa kutumia vyakula. Wapo baadhi ya wagonjwa wa vidonda vya tumbo hutumia baadhi ya vyakula kutuliza maumivu. Mfano wa vyakula hivyo ni maziwa. Endelea na makala hii hapo chini utajifunza vyakula hivi vilivyo vizuri kwa vidonda vya tumbo.
Nini husabaabisha maumivu?
Maumivu ya vidonda vya tumbo pia yanaweza kusababishwa na matumizi ya madawa na vyakula ama vinywaji fulani. Pia kukaa kwa njaa kwa muda mrefu kunaweza kuleta maumivu kwa mgonjwa. Hutokea pia misongo ya mawazo ikawa pia ni vichochezi vya maumivu haya. Huenda mgonjwa anatumia hivi bila ya yeye kujua ama anatumia kwa sababu hana namna nyingine ya kufanya. Kwa mfano ijapokuwa maziwa hutuliza maumivu lakini kitaalamu sio mazuri sana kwa mgonjwa. Endelea na makala hii hapo chini utajifunza vyakula hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Vyakula anavyopasa kula mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Ni ngumu sana hapa kuanza kukuorodheshea orodha ya vyakula vyote anavyotakiwa kula mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Hata hivyo kila jamii ina aina ya vyakula vyao ambavyo ni ngumu kujulikana kwa watu wa jamii nyingine. Hapa nitakuletea tu kanuni ambazo utaziangatia pindi unapochaguwa chakula kwa ajili ya kutumiwa na mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Angalia vyakula vyenye sifa hizi:-
- Vyakula ambavyo havina gesi
- Vyakula ambavyo havina uchachu sana
- Vyakula ambavyo havina chumvi nyingi sana
- Vyakula ambavyo havina mafuta mengi
- Pia vyema ukatumia na vyakula vifuatavyo kwa namna ambayo unaona itafaa kwa upande wako:-
- kabichi
- matunda aina ya maepo
- karoti
- mboga za majani za kijani
- asali
- kitunguu thaumu
Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo:
Kama nilivyokueleza hapo juu kuhusu kanuni za kuzishikili unapochaguwa vyakula basi hapa pia utaendelea na kanuni zile zile pindi unapotaka kuepuka vyakula ukiwa kama mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Epuka vyakula hivi:-
- vyenye gesi kama maharagwe
- vyenye uchachu sana
- vyenye pilipili kwa wingi
- vyenye mafuta mengi
- vyenye chumvi nyingi
Pia punguza matumizi ya vifuatavyo ama wacha kabisa iwezekanapo:-
- sigara
- pombe
- kahawa
- maziwa unaweza kupunguza tu matumizi
- pilipili kwa wingi
Vipi nitajilinda na vidonda vya tumbo?
Ni ngumu sana kwa sababu mpaka leo bado haijajulikana sababu ya kupata bakteria wa vidonda vya tumbo. Hivyo kujikinga na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na mashambulizi ya bakteria ni ngumu. Ila kwa kuwa sababu za kutokea kwa vidonda vya tumbo ni nyingi, unaweza kujikinga na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na sababu nyingine. Njkia hizo ni kama:-
- Punguza misongo ya mawazo
- Wacha ama punguza kutumia kilevi
- Punguza ama wacha kabisa kuvuta sigara
- Wacha kutumia dawa kiholela
Je vidonda vya tumbo vinaweza kupona kabisa?
Tambuwa kuwa vidonda vya tumbo vinatibika bila ya wasi wowote ule. Unaweza kutibiwa na ukapona kabisa. Hakuna muda maalumu wa kupona lakini haiwezi kumaliza miezi hata sita utapona kabisa. Tukutane makala inayofata ttakapojifunza kuhusu matibabu na dawa za vidonda vya tumbo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 web hosting ๐2 Kitau cha Fiqh ๐3 kitabu cha Simulizi ๐4 ai web app ๐5 Simulizi za Hadithi Audio ๐6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Msaada kwa aliye na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
Posti hii inahusu zaidi msaada kwa aliye na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni huduma maalumu ambayo utolewa kwa mtu ambaye ana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo. Zifuatazo ni huduma maalumu kwa mwenye uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Matatizo ya kisaikolojia kwa watoto (mfano, ADHD): Dalili zake.
Afya ya akili ya watoto ni msingi wa maendeleo yao ya baadaye. Katika ulimwengu wa sasa, matatizo ya kisaikolojia kama ADHD (Upungufu wa Umakini na Usikivu) yanazidi kuongezeka, lakini mara nyingi huchanganyikiwa na utovu wa nidhamu. Makala haya yanalenga kutoa mwongozo wa kitaalamu kuhusu dalili za matatizo ya kisaikolojia kwa watoto, yakigusia kwa kina hali ya ADHD na jinsi wazazi wanavyoweza kutofautisha kati ya tabia za kawaida za utotoni na changamoto zinazohitaji msaada wa kisaikolojia.
Soma Zaidi...Kazi ya figo: Dalili za awali za kushindwa kufanya kazi.
โKatika ulimwengu wa sasa wenye kasi kubwa, uchovu wa mwili umekuwa changamoto sugu kwa wengi. Makala hii inachunguza kwa kina vyanzo mbalimbali vya uchovuโkuanzia mambo ya mtindo wa maisha, matatizo ya kisaikolojia, hadi magonjwa ya msingi ya kiafya. Lengo ni kutoa ufahamu wa kina kuhusu jinsi ya kutambua dalili, sababu za kisayansi, na mikakati madhubuti ya kurejesha nishati yako ya mwili na akili.
Soma Zaidi...Madhara ya fangasi.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya fangasi za ukeni kwa kawaida tunajua kubwa fangasi zikiingia kwenye uke usababisha madhara mbalimbali ambayo mengine yanaweza ya kudumu na mengine ya mda kama yametibiwa mapema.
Soma Zaidi...Madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya gonorrhea endapo haitotibiwa
Soma Zaidi...Jinsi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa (STIs).
Magonjwa ya zinaa, yanayojulikana pia kama STIs (Sexually Transmitted Infections), ni miongoni mwa changamoto kubwa za afya ya umma duniani. Kila mwaka, mamilioni ya watu hupata maambukizi mapya ya magonjwa haya, huku wengi wakikosa kutambua kuwa wameambukizwa kutokana na kutokuwa na dalili katika hatua za awali. Habari njema ni kwamba sehemu kubwa ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa inaweza kuzuilika kwa kufuata mbinu sahihi za kinga na kufanya maamuzi salama kuhusu afya ya uzazi. Katika makala hii utajifunza maana ya magonjwa ya zinaa, namna yanavyoenea, sababu zinazoongeza hatari ya maambukizi, njia bora za kujikinga, umuhimu wa kupima afya mara kwa mara, pamoja na ukweli muhimu ambao kila mtu anapaswa kuufahamu kuhusu STIs.
Soma Zaidi...