picha

Vidonda vya tumbo chanzo chake na dalili zake

Katika post hii utajifunz akuhusu vidonda vya tumbo na jinsi vinavyotokea. Utajifunza pia tahadhari anazopasa mtu achukuwe na vyakula salama anavyopaswa kula.

VIDONDA VYA TUMBO, CHANZO CHAKE NA DALILI ZAKE.

Vidonda vya tumbo ni katika matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa yakiathiri watu wengi leo. Si wanawake tu lakini hata wanaume, wazee kwa watoto. Kumekuwa na fikra nyingi potofu kuhusu vidonda vya tumbo nini hasa sababu zake, dalili zake na kwa namna gani vidonda vya tumbo hutokea. Je na wewe ni katika watu wahawa?. makala hii ni kwa ajili yako. Lengo la makala hii ni kukujuza dalili za vidonda vya tumbo.

 

Vidonda vya tumbo ni vidonda ambavyo hutokea kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vinaweza kutokea kuanzia eneo la juu la tumbo la chakula, kuelekea kwenye tumbo, utumbo mdogo hadi utumbo mkubwa. Vidonda hivi pia vinaweza kuathiri koo la chakula. Mara nyingi watu wamekuwa wakidhani vidonda vya tumbo vipo kwenye tumbo la chakula tu. Hii sio sahihi kabisa. Lamda tuone aina za vidonda vya tumbo.

 

Vidonda vya tumbo vimegawanyika katika aina zisizopunguwa tatu. Miongoni mwazo ni  vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye tumbo la chakula, vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye sehemu inayounganisha koo la chakula na tumbo la chakula na vidonda vya tumbo vinavyotokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo.

 

Nini chanzo cha vidonda vya tumbo?

Watu wengi wamekuwa wakidhania kuwa chanzo cha vidonda vya tumbo ni kukaa na njaa muda mrefu. Kwa namna moja wapo sahihi. Lakni ukweli ni kuwa hiki sio chanzo kikuu. Na wanaopata vidonda vya tumbo kwa sababu hii ni wachache sana. Chanzo kikuu cha vidonda vya tumbo ni mashambulizi ya bakteria wanaojulikana kama Helicobacter pylori (.pylori) hawa ni bakteria ambao wanakwenda kushambullia tumbo na utumbo hatimaye kusababisha vidonda.

 

Vyanzo vingine vya vidonda vya tumbo ni kama matumizi ya aina flani za dawa kwa muda mrefu. Mfano mzuri ni dawa za kutuliza maumivu zinazofahamika kama NSAIDs kirefu chake ni kusema nonesteroidal anti-inflamatory drugs mfano wa dawa hizi ni kama advil na aleve. Chanzo kingine cha vidonda ni misongo ya mawazo kwa muda mrefu, na chanzo kingine ni uzalishwaji wa tindikali kuongezeka ndani ya mwili.

 

Je ni kivipi vidonda hutokea?

Kwa ufupi vidond hutokea baada ya utando mlaini kwenye tumbo na utumbo kulika na kubakisha tumbo ama utumbo kuwa wazi hivyo kuruhusu shughuli za tindikali kuathiri tumb na utumbo. Hii husababisha michubuko na hatimaye kuleta vidonda vya tumbo. Bila shaka huwenda hujaelewa hapa. Wacha nikujuze zaidi

 

Katika tumbo na utumbo kuna tindikali (acid) ambazo huzalishwa mwilini kwa ajili ya kuuwa bakteria kwenye vyakula. Zipo kazi nyingine pia. Tindikali hizi zina nguvu kiasi hata kuraruwa bati. Sasa kwa nguvu hii hata ngozi inaweza kuchubuka na kusababisha vidonda. Sasa kwa kuwa kwenye tumbo na utumbo kuna utando wa utelezi huu husaidia kuzuia athari ya bakteria haiathiri utumbo na tumbo.

 

Sasa endapo utandu huu utaathirika na hautakuwepo tena ama utakuwepo kwa uchache hali hii itaruhusu tindikali zinazozalishwa kwenye tumbo na utumbo kuchubuwa kuta za utumbo na utumbo na hatimaye kusababisha vidonda.

Kuhusu bakteria wanavyosababisha vidonda inaweza kuwa tofauti kidogo. Wao bakteria kwanza mara nyingi hawana shida wanweza kuishi mika mingi bila ya kusababisha vidonda. Sasa wakati mwingine wanaweza kusababisha kuta laini za utumbo na tumbo kuvimba. Hii mivimbo baadaye kusababisha vidonda.

 

Hutokea pia tindikali zikaunguza utando laini huu unaokinga ngozi ya tumbo na utumbo. Hii hutokea endapo uzalishwaji wa tindikali utaongezeka. Hii inaweza kusababishwa na vyakula, misongo ya mawazo ama matumizi ya dawa kama ilivyoelezwa hapo juu.

 

Ni zipi dalili za vidonda vya tumbo?

Dalili za vidonda vya tumbo zinaweza kuwa tofauti kutokana na mtu mwenyewe, mahali vilipo na mengineyo lakini zipo ambazo hutokea kwa watu karibia wote. Dalili hizo ni kama:-

  1. Tumbo kujaa gesi
  2. Kiungulia cha mara kwa mara
  3. Maumivu ya tumbo hasa unapokuwa na njaa
  4. Uchovu wa mra kwa mara
  5. Kupata choo cheusi ama chenye damu
  6. Huwenda ukatapika damu
  7. Inaweza tokea ukapunguwa uzito
  8. Kukosa hamu ya kula

 

Mgonjwa anaweza kupata nafuu ya maumivu baada ya kula na kshiba. Pia kuna wengine wanapata nafuu baada ya kunywa maziwa. Lakini tambuwa kuwa ijapokuwa maziwa yanaweza kukupa nafuu lakini sio mazuri huwenda yakaja kukuletea madhara huko siku za mbele.

 

Je vidonda vya tumbo vinatibika?

Jibu fupi ndio, vidonda vya tumbo hutibika tena bila ya ugumu wowote. Vindonda vya tumbo vinaweza kutibika kwa dawa za asili kama bamia, kabichi, kitunguu thaumu, asaili na nyinginezo. Lakini pia ni vyema kutumiadawa za hoospitali kwa sababu zina vipimo maalumu.

 

Vidonda vya tumbo vinaweza kuwa sugu. Na hii hutokea endapo utumiaji wa dozi hautafata masharti. Lakini pia inawez akutokea bila ya sababu maalumu. Wakati mwingine vidonda vya tumbo huwa sugu kwa sababu tiba yake sio inayotumika. Ili kuweza kutokomeza vidonda vya tumbo kwanza ni kujuwa sababu gani inayosababisha vidonda vya tumbo.

 

Kama sababu ni tindikali kuzaliwa nyingi bai mgonjwa apewe dawa za kuzuia uzalishwaji wa tindikali kutokuwa mwingi zaidi. Na kama sababu ni matumizi ya dawa mgonjwa iangaliwe kama ataweza kubadilishiwa dawa. Na kama sababu ni bakteria mgonjwa atapewa dawa ya kuuwa bakteria hao tumboni.

 

Imanipotofu kuhusu vodona vya tumbo

Kama nilivyokueleza mwanzoni mwa makala hii kuwa kuna imani nyingi potofu na hazina ushahidi wa kitaalamu. Inaweza kuwa watu ndivyo wanavuyoamini kutokana na jamii zaoama kutokana na tafiti za zamani ambazo kwa sasa zimekosolewa kutokanana tafiti mpya. Imani hizo ni kama:-

  1. Vyakula vyenye pilipili husababisha vidonda vya tumbo, hii si kweli
  2. Kukaa na njaa ndio sababu kubwa ya kutokea vidonda vya tumbo, hii si kweli
  3. Vidonda vya tumbo havitibiki, hii ia si kweli.

 

Tukutane makala ijayo tutakapoona vyakula vizuri na vibaya kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 2363

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     ๐Ÿ‘‰2 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game     ๐Ÿ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Sababu za wanawake kuwa na maumivu kwenye kiuno

Posti hii inahusu zaidi sababu za wanawake kuwa na maumivu kwenye viungo, ni ugonjwa unaowapata na wanaume ila kwa wanaweza unaowapata sana ukilinganisha na wanaume.

Soma Zaidi...
Shinikizo la damu (High Blood Pressure): Sababu na vyakula vya kuepuka.

Shinikizo la damu (Hypertension) ni tatizo sugu la kiafya linaloathiri mamilioni ya watu duniani kote. Makala hii inachunguza kwa kina kiini cha shinikizo la damu, sababu zake kuu, na umuhimu wa lishe katika kudhibiti hali hii. Kwa kuelewa vyakula vya kuepuka na mabadiliko ya mtindo wa maisha, unaweza kulinda afya ya moyo wako na kuzuia madhara makubwa kama kiharusi na ugonjwa wa figo.

Soma Zaidi...
Sababu za mdomo kuwa mchungu

Hapa utajifunza sababu zinzopelekea mdomo kubadilika ladha na kuwa mchungu, ama mchachu.

Soma Zaidi...
Njia za Kuongeza Hamu ya Mapenzi kwa Mwanaume

โ€‹Kupungua kwa hamu ya mapenzi kwa mwanaume ni jambo linaloweza kusababishwa na mambo ya kisaikolojia, kimwili, au mtindo wa maisha. Makala haya yatajadili njia madhubuti za kuboresha hamu ya mapenzi kupitia mabadiliko ya afya, lishe, na mawasiliano.

Soma Zaidi...
Matibabu ya vidonda sugu

Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu matibabu ya vidonda vya tumbo sugu

Soma Zaidi...
โ€‹Ishara za Uchungu wa Kujifungua Zinapoanza

โ€‹Kipindi cha mwisho cha ujauzito kinaweza kuambatana na mchanganyiko wa msisimko na wasiwasi. Posti hii inaangazia ishara kuu ambazo mwili hutoa wakati uchungu wa uzazi unapoanza, ikikupa mwongozo wa wakati mwafaka wa kwenda hospitali.

Soma Zaidi...