Posti hii inahusu zaidi huduma muhimu anazopaswa kupewa mama mjamzito wakati akiwa na mimba, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua yaani ndani ya masaa ishirini na manne, tunajua wazi kuwa Mama akiwa mjamzito anaweza kupata matatizo mbalimbali kwa h
Huduma za msingi kwa mama mjamzito na mtoto.
1. Uzazi wa mpango.
Hivi ni huduma ya msingi kabisa ambayo Mama anapaswa kujua kabisa namba ya watoto anaowahitaji na ni namna gani wanapaswa kuachana kwa miaka, hali huu umsaidia Mama kupumzika kutoka kwenye nzao moja kwenda nyingine na kuwasaidia watoto kupata mda mzuri wa kukua, kupendwa, kupata malezi ya kutosha kwa mda mwafaka na kupata elimu ya kutosha. Kwa hiyo Mama anapaswa kuchagua njia ya uzazi wa mpango ambayo ni ya maana na faida kwake.
2. Usafi wakati wa ujauzito , kujifungua na wakati wa malezi ya mtoto.
Mama anapaswa kuwa msafi mda wote anapokuwa na mimba na kuandaa vifaa vyake kwa hali ya usafi wa hali ya juu kwa kufanya hivyo anazuia maambukizi bambayo yanaweza kuleta maendeleo kwa mtoto na kwa Mama mwenyewe, hali huu utokea kwa akina mama hasa wale wanojifungulia vijijini utumia viwembe vyenye kutu kukata kitovu na hatimaye kusababisha maambukizi kwa mtoto na hatimaye madhara makubwa yanayoweza kujitokeza. Kwa hiyo tunapaswa kuwahimiza akina mama kujiandaa na kuwa na vifaa vizuri wakati wa kujifungua.
3. Kuzuia maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.
Hivi ni njia ambayo umsaidia mtoto kutopata maambukizi ya HIV au AIDS na kaswende kwa hiyo Mama anapoanza mahudhurio ya kwanza anapaswa kuja na mme wake ili kupima Maambukizi na kabla ya Mama kujifungua anapaswa kuja kupima maambukizi ili kama wazazi wana Maambukizi waweze kumkinga mtoto ili hasipatwe na wakati wa kujifungua kuwa makini ili kumzuia mtoto hasipatwe na Maambukizi, na pia huwasaidia wazazi wote way kujua afya zao endapo walikutwa na Maambukizi wanaanza dawa mara moja.
4. Pia wakati wa ujauzito mama anapaswa kukingwa na Dalili za hatari.
Hizi ni Dalili ambazo ujionyesha kwa mama wakati akiwa na mimba na zisipotibiwa au kushughulikiwa mapema zinaweza kufanya mimba kutoka , Dalili hizo ni pamoja na kuvimba miguu kwa mama, kutokwa damu ukeni na uchafu ukeni, mtoto kushindwa kucheza akiwa tumboni, maumivu makali ya kichwa kwa mama mjamzito, Mama akisikia Dalili kama hizi anapaswa kuwahi mapema hospitali kwa ajili ya huduma zaidi, kwa hiyo mama anapaswa kujua wazi dalili za hatari na kuweza kuepukakana nazo au kwenda hospitali mara moja.
5. Kumtunza mama na Mtoto, baada ya Mama kumaliza kujifungua,
Hii ni huduma ambayo utolewa kwa Mama na mtoto ndani ya Masaa ishirini na nne, katika kipindi hiki Mama na mtoto upewa nafasi ya kupumzika ili kuweza kuangalia maendeleo yao au kuangalia kama kuna kitu chochote kinachoweza kubadilika lakini elimu utolewa kwa Mama namna ya kumlisha na kumtunza mtoto na chanjo mbalimbali utolewa kwa mtoto ili kumkinga na Magonjwa nyemelezi kwa mtoto, kama mtoto na Mama wanaendelea vizuri wanaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani.
6. Kwa hiyo tunajua wazi ,Mama akiwa na mimba kuna mabadiliko mengi ambayo utokea kwa hiyo tunapaswa kuwapa kipau mbele na kuwasikiliza wajawazito na kuwapa chakula na dawa zinazofaa kwa hiyo tuachane na mila potofu na imani zisizofaa kwa akina Mama wajawazito.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Majimaji msule sehemu za siriyanaweza kuashiria mambo mengi ka mwanamke. Ikiwemo ujauzitina maradhi. Pia yanaweza kuashiria kuwa mwanamke unaweza kuoatavujauzito amalaa.
Soma Zaidi...Swali langi ni hiliMama mjamzito anapo hisi uchungu je mtoto huendelea kucheza tumboni?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tabia mbalimbali za Ute wa ovulation kwa sababu Ute huu huwa tofauti na Ute mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa tabia zake za kipekee kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kutangulia kwa kitovu wakati wa mtoto anapozaliwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuhusu kwa mimba kutoka kabla ya mda wake,ni kitendo ambacho mimba utoka kabla ya wiki ishilini na na nane.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa madogo madogo kwa akina Mama wajawazito, ni magonjwa ambayo hayawezi kupelekea kupoteza maisha kwa Mama mjamzito, magonjwa haya upotea ikiwa Mama atajifungua.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili za saratani kwa watoto, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto na ikiwa mlezi au mzazi akiziona tu anaweza kutambua mara moja kwamba hii ni saratani au la na kama bado ana wasiwasi anaweza kupata msaada zaidi kutoka kwa wataa
Soma Zaidi...Je kutokwa na maji ukeni ambayo hayana harufu na meupe Hadi kuroanisha chupi, na je kutokwa na maji mengi wakati wa tendo la ndoa inaashilia nini?
Soma Zaidi...Je, unafahamu dalili za mwanzo za ujauzito? Kutoka kwa kichefuchefu hadi uchovu, ujue nini cha kutarajia.
Soma Zaidi...Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa
Soma Zaidi...