picha

Sifa za mchumba

Sifa za mchumba

Kizazi, Rika na Elimu



Sifa nyingine za kuzingatia wakati wa kuchagua mchumba ni kizazi na rika. Kuhusu kizazi Mtume (s.a.w) anatunasihi:
"Oeni wale wanawake wenye upendo na huruma, wenye kizazi na hakika watakuwa ni wenye manufaa katika kuongeza idadi yenu miongoni mwa matafa." (Abu Daud, Nasai)



Kwa vijana ambao ndio mara yao ya kwanza kuingia katika maisha ya ndoa, pamoja na kuzingatia sifa za msingi zilizoelezwa, ni vema wakachaguana vijana kwa vijana kama alivyoshauri Mtume (s.a.w) katika hadithi ifuatayo:



Jabir (r.a) ameeleza: "Tulikuwa na Mtume (s.a.w) katika vita. Tulipokaribia Madina wakati wa kurejea nilisema: "Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika nimeoa hivi karibuni." Akauliza, "Umeoa"? Nikajibu, "Ndio" Akauliza: "Bikra au mjane?" Nikajibu "Mjane" Akasema, "Kwa nini asiwe bikra ili uweze kucheza naye, naye aweze kucheza nawe..." (Bukhari na Muslimu)



Jambo lingine Ia kuzingatia wakati wa kuchagua uchumba ni Elimu. Kama mume na mke watakuwa na Elimu sahihi juu ya Uislamu na taaluma nyingine za mazingira yao watakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuwalea watoto wao kimaadili na kitaaluma. Katika kusisitiza hili tuzingatie mchango wa bibi Khadija (r.a) alioutoa katika kuupeleka mbele Uislamu kutokana na utajiri wake na mchango wa bibi 'Aisha (r.a) alioutoa katika kuufundisha Uislamu kutokana na Elimu yake ya Uislamu.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views 1556

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 ai web app     👉3 web hosting     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'I TABI'IIN

Wakati wa Wafuasi wa Masahaba (Tabi'i Tabi'ina)201-300 A.

Soma Zaidi...
KUAMINI MALAIKA

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...