MUDA WA KUCHAJI SIMU YAKO

Wwatu wengi wamekuwa wakijiuliza ni muda gani hasa inapasa kuchaji simu, je nisubiri mpaka chaji iishe kabisa, ama nichaji ikiwa na asilimia ngap?. maswali kama haya na yanayofanana nitakwenda kuyajibu katika makala hii.

 

Kikawaida betri inaweza kudumu kuwa hai kati ya miaka 5 mpaka 10. lakini uwezo wa betri hupungua kadri siku sinavyoendelea. Unaweza kudhibiti hali hii kwa kuwa makini na baadhi ya mambo kadhaa. Miongoni mwa mabo hayo ni kuwa makini na muda wa kuchaji.

 

Wataalamu wa teknolojia wanatueleza kuwa muda mzuri wa kuichaji betri ni pale itakapobakiwa na asilimia kati ya asilimia 50% na 90%. na hakikisha kuwa huichaji mpaka ifikapo 100%. ni vyema kama unataka ifike 100 basi angalau ufanye hivyo mara chache.

 

Sio vyema sana kuilaza kwenye chaja japo jambo hili halina madhara kwa simu za kisasa kwani zenyewe zina kifaa cha kuifanya isimame kuchaji pindi ikifapo asilimia 100% ya chaji.

 

Hakikisha betri yako haivi chini ya asilimia 40% na mbaya zaidi isifike asilimia 2% ama 0%. na kama unahitaji kuihifadhi betri yako basi ichaji angalau asilimia 40% kisha uihifadhi.

 

Kama unataka kutumia simu ikiwa chaji hakikisha unatumia chaja yake ama chaja original ya simu hisika, na epuka kutumia simu yako inapokuwa imoto. Na kama unailaza kwenye chaja hakikisha unaondoa vitu vyote vitakavyo sababisha iwe na moto kama kuiweka juu ya kitu kimoto kama deki.