image

Utajiaje kama simu/kompyuta ina virusi

Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta..

Utajiaje kama simu/kompyuta ina virusi

UWANJA WA TEKNOLOJIA

Sehemu ya 12

.

UTA JUAJE KAMA SIMU AU KOMPYUTA YAKO INA VIRUSI?
Katika post hii vip utaweza kujuwa kuwa kifaa chako kina virusi.Malware ni pamoja na virusi worm na trojan. Wote hawa hwanaweza kuharibu mafaili katika kifaa chako. Ila jambo ya kujuwa ni kuwa huwa wana baadhi ya sifa za kufanana wanapokuwa wanadhuru kifaa chako.Kwa kutumia mfanano huo utaweza kugunduwa uvamizi katika kifaa chako.

            NJIA ZA KUTAMBUWA VIRUSI KATIKA KIFAA CHAKO:
1.Kifaa chako kutokuwa na kasi katika ufanyaji kazi (slow); Hapa inaweza ikatokea unabonyeza batani lakini inachelewa kufanya kazi. Wakati mwengine unaweza ukabonyeza batani ya kuangalia meseji lakini ikachelewa kufunguka mpaka unasubiria kwa muda kidogo.

Ijapokuwa tatizo la kifaa chako kuwa slow linaweza kusababishwa na mabo mengine kama vile RAM, kuwepo kwa Spyware, na kujaa kwa hard disk, lakini kuwepo kwa virusi huwa ni chanzo kikubwa kama RAM na Hard disk ikawa safi yaani ikawa na uwezo wa kutoshelezea mahitaji yako.

kuweza kutatuwa tatizo hili tulisha eleza katika baadhi ya post zetu, ila kwa ufupi hakikisha kifaa chako kina nafasi ya kutosha katika memory yake au hard disk. Hkikisha mstari mwekundu wa kuonesha kuwa memory au Hard disk imejaa haupo, Hakikisha kompyuta yako ina RAM ya kutosha kwa mahitaji ya kifaa chako. Skann virusi kwa kutumia ant virus iliyo madhubuti\ na iliyo up to date.

2. Kuchelewa kufunguwa internet, Hapa huwa kifaa chako unapofunguwa intanet kinachelewa kuload. inatokeaa unabonyeza batani ya kusearch lakini unasubiria muda mrefu. Unapokuwa unadownload kifaa chako kinachelewa sana kudawnload. Kwa ufupi intanet kuwa slow husababishwa na kuwepo kwa virusi kwenye kifaa chako.

Ijapokuwa zipo sababu zingine zinazosababisha kifaa chako kuwa slow kwenye intanet kama vile netwprk kuwa kidogo. HIvyo kabla haujajiridhisha kuwa kifaa chako kina virusi kwanza hakikisha kuwa unamtandao wa kutosha kwenye kifaa chako. Pia hakikisha umeruhusu 3G au 4G katika kifaa chako. Kama itakuwa bado slow anza taratibu za kuondowa virusi katika kifaa chko.

3. Program kujifunguwa zenyewe; Hapa inatokeya baadhi ya program katika kifaa chako ziajifunguwa zenyewe bila ya kuruhusiwa. Hiki ni kiashiria kimojawapo cha kuwepo kwa virusi katika kifaa chako. Jambo la kufanya hapa ondowa proram hizo zinzojifunguwa zenyewe kisha skan viruri katika kifaa chako.

Tatizo la kuwa na virusi katika vifaa vya kielectronoc ni lakawaida, na ni vigumu kuliepuka kabisa. Jambo la kufanya ki kuwa na utaratibi wa kutazama kifaa chako kila wakati kama kuna athari yoyote. kuwa na utaratibu wa kuskani kifaa chako. Au ruhusu auto scan. yaani kifaa chako kiwe kinajiskani chenyewe kulingana na muda utakaotaka. Jambo la kuzingatia zaidi hapa ni kuhakiisha ant virusi uliyo nayo ipo vizuri kwa kufanya kazi hii.



         › WhatsApp ‹ Whatsapp






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 296


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

NINI HATMA YA FACEBOOK BAADA YA KUFA KWAKO? nini kitatokea kwenye akaunti yako ya fesibuku (facebook)
Facebook hawana mpango wa kufunga akaunti ambazo hazijatumiwa kwa muda mrefu, haijalishi akaunti ni ya marehemu ama yupo hai. Soma Zaidi...

Kujaa kwa memory au hard disc
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vitu vya kufanya endapo memory au hard disk itajaa Soma Zaidi...

Njia rahisi ya kudownload video YouTube
Posti hii inakwenda kukuelekeza kuhusu njia rahisi ya kudownload video YouTube Soma Zaidi...

Njia za kujilinda na malware
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujilinda na malware Soma Zaidi...

Nini chanzo cha tatizo la computer au simu yako
Posti hii inakwenda kukupa elimu kuhusu chanzo cha tatizo la computer au simu yako Soma Zaidi...

Chanzo cha matatiza ya simu/kompyuta
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Sababu za simu kusumbua mtandao
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sabau za simu kusumbua mtandao Soma Zaidi...

UTUNZAJI WA BETRY YA KIFAA CHAKO
Namna ya kutunza betri yako iweze kudumu kwa muda mrefu Soma Zaidi...

teknolojia
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Nini Chanzo
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

KIPI KINGINE UTAFANYA UKIWA FACEBOOK: matumizi mengine ya facebook
Facebook ni mtandao wa kwanza wa kijamii (social media) unaotembelewa na watu wengi. Soma Zaidi...

OCR
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...