NINI MAANA YA LEGACY CONTACT KATIKA FACEBOOK?

Facebook hawana mpango wa kufunga akaunti ambazo hazijatumiwa kwa muda mrefu, haijalishi akaunti ni ya marehemu ama yupo hai. Kama hutaki akaunti yako ya facebook kuna njia moja tu nayo ni kuifuta. Hata hivyo mchakato huu inachukuwa kuanzia siku 114 yaani siku 14 za akaunti kuwa haipo active na aiku 90 za kuthibitisha kufuta akaunti hii.

 

Kwa waliofariki akaunti zao zitabakia milele ama mpaka facebook wakibadili sera ya kutofunga akaunti zilizotumika. Wakati mwingine akaunti za waliofariki zinatumiwa vibaya, hivyo unaweza kuchagua nini kifanyike utakapo fariki, aidha akaunti yako ifungwe ama ibakie kama ya kumbukumbu.

 

Kufanya haya yote mawili unatakiwa umchague mtu atakayefanya haya. Na mtu huyu itamchagua ukiwa hai. Mtu huyu anatambulika kama LEGACY CONTACT. Legacy contact ni friend kwenye akaunti yako ya facebook ambaye imemchagua kuwa ndiye utampa madaraka ya kuweza kuomba akaunti yako ya facebook ifungwe pindi utakapo fariki, ama akaunti yako iwe ni akaunti ya kumbukumbu yaani memorization account.

 

Mtu huyu hataweza kulog in kwenye akaunti yako. Yaani hataweza kuona taarifa zako za siri hata moja. Yeye atakuwa na madaraka kama:

1. Kuomba akaunti yako ifungwe ama iwe ya kumbukumbu
2. Kubadili profile picture ama profile cover picture.
3 .Kukubali friends request chache kutoka katika watu wa familia
4. kuzuia ni picha zipi ziweze kuonea na ni nani aweze kuziona
5. kuzuia watu wasidownload picha zako ana kama utamruhusu kupitia legacy ataweza kudownload yeye tu.
6. kuondoa tag kama kuna mtu amekutag

 

Memorization account
Kama legacy wako ameomba akaunti yako isifungwe bali iwe memorization account basi itakuwa na sifa hizi

1. Haitaonekana kwenye ukurasa mkuu wa facebook
2. hata mtu akisach nina halitakuwa
3. waliokuwa friend ndio watakaoweza kuona akaunti tu.
4. Ni akaunti kwa ajili ya kumbukumbu kwa ndugu na jamaa
5. Facebook wataweza lebo karibu na profile picture kuonyesha kuwa huyu amefariki
6. Hautaweza kutumiwa meseji akaunti hii

Ukitaka kujua namna ya kumchagua mtu huyu atakayekuwa na mamlaka ya kufunga akaunti yako ama kuihamisha iwe ya kumbukumbu, angalia video kwenye link hapo chini

https://youtu.be/NKN41RXYNcg