SIMU KUSUMBUWA MTANDAO NINI SABABU

Kuna mambo mengi sana ambayo yanachangia simu yako kutokuwa na mtandao mzuri yaani network kuwa ndogo. Mambo haya ni pamoja na:-
1. Umbali kutoka kwenye mnara
2. Hali ya hewa
3. Uwezo mdogo wa simu, ama simu kuwa mbovu
4. Vitu vinavyo kuzunguka na sehemu ulipo kama mabondeni, kwenye shimo, kwenye msitu mnene n.k
5. Kubadilika kwa mnara.

Kuna mambo mawili hapa nitaongezea. Hutokea wakati mwingine upo sehemu nzuri, na karibu na mnara na simu yako ni nzima, lakini mtandao unasumbuwa. Hapa kuna mambo mawili unatakiwa uyajue kama:-

  1. Kubadilika kwa mnara. Unapotoka sehemu moja kwenda nyingine kwenye mnara mwingine, simu yako itabadilisha mnara kutoka ule wa mwanzo na kutumia wa pili. Hivyo basi njia sahihi hapa ni ku restart au reboot simu yako. Ama izime kisha iwashe tena.
  2. Pia wakati mwingine huwenda simu yako ina app(program)nyingi ambazo zinatumia network kwa mfano ukiwasha data na ukiwa na application nyingi ambazo zinatumia data kwa kuonyesha matangazo, pic, sms n.k hili huweza kufanya network ya simu yako kuwa ndogo ama dhaifu.

Kwa maelezo zaidi ya makala hizi za sayansi na teknolojia usiwache kutembelea chanel yetu ya video youtube