HISTORIA YA KUPASULIWA KWA KIFUA AU TUMBO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AKIWA MTOTO KWA BI HALIMA
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO.
![]()
![]()
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO.
Mtume alipokuwa mtoto tukio hili la kupasuliwa kwa kifua chako na kutolewa moyo wake na kusafishwa. Yote haya yalitokea kipindi akiwa analelewa na bi Halima katika kabila la bani Saโad. Wanazuoni wa sirah wameeleza kwa urefu tukio hili jinsi lilivyotokea. Na hapa tutaangalia kwa ufupi tu.
Ni kuwa siku moja mtume (s.a.w) alikuwa anacheza na watoto wenzie. Ghafla akatokea mtu mmoja naye ni Jibrib akamshika Muhammad na kumlaza chini kisha akamtoa moyo wake na kuuosha kwa maji ya zamzam na aliondoa uchafu wa shetani kisha akaurudisha kwenye kifua na kukifunika.
Watoto walokuwa wakicheza na Mtume (s.a.w) wakakimbia na kwenda kumueleza bi Halima kuwa Muhammad kauliwa. Bi Halima akatoka kwa haraka kufika akamkuta Muhammad akiwa amebadilika rangi. Muhammad alikuwa ni mzima wa afya, hapa bi Halima alipata mashaka makubwa mpaka akawa na hofu juu ya kuendelea kumlea kijana Muhammad.
Katika maelezo mengine waandishi wa sirah wameeleza tukio hili kama kupasuliwa kwa tumbo. Kwani zimekuja nukuu kuwa sikumoja waroto walipokuwa wakisheza pamoja nao alikuwepo Muhammad (s.a.w) basi ghafla wakaja wanaume wawili walovaa nguo nyeupe (Malaika) wakaulizana ni hyu? Basi yule mwingine akajibu ndio ni huyu, wakamlaza kisha wakampasua tumbo lake na kutoa uchafu wa shetani kisha wakafunika kama lilivyo. Basi watoto walokuwa wakicheza nae wakaenda mbio kusema wa bi halima na alipokuja kuulizwa Muhammad (s.a.w) akasema kuwa watu wawili wamekuja na kunipasua tumbo langu. Utapata maelezo zaidi ya kisa hiki kwenye kitabu kiitwacho Nurul- Yaqin.
Bi Halima aliendelea kumlea Mtume (s.a.w) kwa muda wa miaka miwili mingine hata alipotimiza miaka minne aliamuwa kumrudisha mtoto kwa mama yake. Alihofia kuendelea kumlea mtoto huyu huenda akapatwa na jambo. Miaka minne alikuwa imemtosha mtoto huyu kuwa na mwili imara na kuweza kuzungumza lugha ya kiarabu wa ufasaha tofauti na watoto walolelewa maeneo mengine.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) ๐2 kitabu cha Simulizi ๐3 Simulizi za Hadithi Audio ๐4 Madrasa kiganjani ๐5 ai web app ๐6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Yusufu(a.s)
โKwa yakini katika (kisa cha) Yusufu na ndugu zake yako mazingatio mengi kwa wanaouliza (mambo wapate kujua)โ.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Musa(a.s) na Harun(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Musa na Harun(a.
Soma Zaidi...Muhutasari wa sifa za wanafiki
Kwa kuzingatia aya zote tulizozipitia juu ya wanafikitunaweza kutoa majumuisho ya sifa za wanafiki kama ifuatavyo:- (1)Hutenda kinyume cha imani wanaodai kuwa nayo.
Soma Zaidi...HISTORIA YA FAMILIA YA MTUME MUHAMMAD S.A.W
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 02.
Soma Zaidi...Jinsi tukio la Karatasi lilivyotokea wakati wa Mtume siku chache kabla ya kifo chake
Tukio la kartasiTukio la โkartasiโ lililonakiliwa katika vitabu vya Muslim na Bukhari kuwa siku tatu kabla ya kutawafu Mtume (s.
Soma Zaidi...