HISTORIA YA KUJENGWA UPYA KWA AL-KA'BAH (NYUMBA TUKUFU YA ALLAH)

KUJENGWA UPYA KWA AL-KA’ABAHItambulike kuwa Al-ka’abah ndio mjengo wa kwanza kujengwa duniani.

HISTORIA YA KUJENGWA UPYA KWA AL-KA'BAH (NYUMBA TUKUFU YA ALLAH)


KUJENGWA UPYA KWA AL-KA’ABAH
Itambulike kuwa Al-ka’abah ndio mjengo wa kwanza kujengwa duniani. Kuna baadhi ya wanahistoria wanazungumza kuwa Al-ka’abah kwa mara ya kwanza ilijengwa na Malaika. Kisha ikawa inajengwa kwa kurekebishwa na kuboreshwa muda baada ya muda na binadamu wenyewe. Huenda pia aliyejenga al-ka’bah ni nabii Adamu. Kilicho sahihi zaidi katika maneno haya ni ile kauli ya Allah aliposema kwenye quran kuwa “kwa hakika nyumba ya kwanza kujengwa kwa na watu ni ile iliyopo Makka (al-ka’aba).

Kilipita kipindi kirefu toka kwa Nabii Adamu hadi kwa nabii Ibrahimu. Wakati huo wote al-ka’abah ilikuwa imebakia msingi tu lakini ulisha angukaga zamani sana. Nabii Ibrahimu na mtoto wake Nabii Ismaili (amani iwe juu yao) ndio waliokuja kuijenga upya baada ya kusahaulikwa kwa muda wa miaka mingi sana. Mitume hawa wawili waliweza kuzinyanyua kuta za al-ka’abah na kuunyanyua mjengo wake. Baada ya mitume hawa kujenga al-ka’abah watu wakatangaziwa hija na wakawa wanakwenda kutoka mataifa mbalimbali.

Al-ka’abah iliweza kudumu kwa muda wa miaka mingi bila hata ya kufanyiwa ukarabati upya. Miaka mingi ilisha pita hivyo kutokana na uzee jengo hili kuta zikawa zina nyufa, na zilipoteza ule upora wake. Hata hivyo jengo hili halikuwa madhubuti kwa wezi waliweza kuingia na kuiba baadhi ya hazina zilizohifadhiwa mule. Pia wakati huu al-ka’abah haikuwa na dari. Miaka mitano (5) kabla ya utume kulitokea mafuriko makubwa katika mji wa Makkah. Mafuriko haya yaliweza kuharibu mjengo huu na kuudhoofisha zaidi.

Baada ya tukio hili waarabu wakakaa shura ili wajadiliane namna ya kunusuru jengo hli. Katika shura yao wakakubaliana kujenga upya mjengo huu. Chifu wa maquraysh akaamuwa kuwa watatumia gharama (pesa) za kujengea mjengo huu peza za halali tu. Na hairuhusiwi kutumia pesa yeyote ya haramu kujenga mjengo huu. Baada ya makubaliano haya kazi ya kujenga al-ka’abah ilianza maramoja.

Mwanzo kabisa walikuwa wanaogopa kubomoa jengo hili tukufu. Woga wao uliendelea mpaka alipotokea Al-waleed bin al-Mugheerah al-makhzumi huyu ndie aliyeanza kubomowa ukuta, na baada ya waarabu kuona hakuna lolote baya lililomkuta ndipo wakaungana nae katika kubomoa kuta nyingine. Waliendelea kubomoa mpaka wakakuta msingi aloanzia nabii Ibrahim kujenga al-ka’abah. Waarabu wakagawana kazi kulingana na makabila yao, hivyo kila kabila likapewa jukumu lake.

Hivyo makabila yakaanza kuokota mawe na kazi ikaanza. Mtu ambaye alijenga msingi ni fundi mwenye asili ya kiroma aliyefahamika kwa jina la Baqum. Kazi ya kujenga al-ka’abah ilikwenda vizuri mpaka walipomaliza. Sasa kukawa na mzozo juu ya kulirudisha jiwe jeusi mahala pake. Hapa walitofautiana na mzozo ukawa mkubwa zaidi juu ya nani aweke ziwe tukufu jiwe jeusi mahala pake. Mzozo ulifikia hatua ya watu kuweza kupigana na hata kuwana.

Mzozo huu ukiendelea kati ya machifu wa makabila mpaka ukadumu kwa muda wa siku 4 ama 5 kila mmoja akitaka aipate yeye heshima ya kuliweka jiwe tukufu mahala pake. Mpaka pale mzee mmoja kwenye kuheshimika na mwenye budsara aliyetambulika kwa jina la Abu omaiyah bin Mughiirah al-Makhzum alipotowa rai ambayo ilikubwaliwa na watu wote rai ambayo ililenga kumaliza mzozo huu. Mzee huyu alitowa rai ya kuwa yeyote atakayekuwa wa kwanza kuingia msikitini awe ndiye hakimu wa kutoa maamuzi. Hivyo wote wakakubaliana kwa rai hii. Basi akawa mtu wa kwanza kuingia msikitini ni mtume muhammad (s.a.w).

Wazee wote walipomuona mtu wa kwanza kuingia Msikitini ni Muhammad basi walikubali kwa moyo mmoja kwani walimtambuwa ukweli na uaminifu wake. Na pia alikuwa ni kijana mwenye tabia njema kuliko vijana woote wa Makkah. Basi akachukiwa kilemba na akaliweka lile jiwe kisha akataka kila kiongozi wa kabila akamate ncha ya kilemba kie na kulinyanyua jiwe kwa pamoja. Walipofika sehemu yake akalichukuwa na kuliweka kwa mikono yake. Hapa wazee wote walimsifu na kumkubali kwa busara yake. Hatimaye walimaliza kulijenga jengo hili tukufu, wakati huu Mtume muhammad akiwa na umri wa miaka 35 yaani miaka mitano kabla ya kupea utume.


                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1466

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Mafunzo yatokanayo na vita vya uhudi

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi

Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri.

Soma Zaidi...
Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kulingania watu wake na Miujiza Aliyoonyesha Nabii Isa(a.s)

Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyewawezesha Mitume na Manabii kufanya miujiza.

Soma Zaidi...
Historia ya Vijana wa Pangoni

Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na maandalizi ya mtume ki-wahay

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...