MAISHA YA MTUME (S.A.W) KABLA YA UTUME
Muhammad alipokuwa ni kijana alikuwa ni mwenye tabia njema, mwenye mwenendo mwema, mkweli na muaminifu. Waarabu walimwita jina la Al-Amini yaani mwaminifu. Alikuwa ni mwenye busara na akili sana. Alikuwa si muongeaji sana muda mwili alikuwa mkimya huki akitafakari ukweli katika maumbile ya mbingu na ardhi.

Katu hakuwahi kusujudia sanamu wala ibada za kijahilia. Hakuwahi kupigana wala kugombana. Katu hakuthubutu kula nyama iliyochinjwa kwa ajili ya ibada za masanamu na mila zao za kijahilia. Pia hakuweza kumvumilia yeyote ambaye anaapa kwa jina la Al-lat au Al-Uzaa na haya ni majina ya miungu yao.
ITAENDELEA…….