Menu



HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)

HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.

HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)


HISTORIA YA BI KHADIJA
Bi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara. Baadhi ya historia zinataja kuwa alifariki wakati wa vita vya Alfijar mwaka 585 BK, tumetaja muhusu vita hivi kurasa za hapo juu. Nasaba yake pia inakutana na nasaba ya Mtume Muhammad kwa upande wa bab yake na baba yake. Mama yake aliitwa Fatima Bint Zaโ€™idah na alikuwa katika kabila la maqurayshi, kabila la Mtume Muhammad (s.a.w). mama yake Khadija alifariki mwaka 575 KK. Khadija aliolewa na Muhammad mwaka 595.

Bi Khadija alishapata kuolewa na wanaume wawili kabla hata ya kuolewa na Muhammad na lishazaa watoto. Khadija alikuwa na katika wafanyabiashara wa Makkah wakubwa sana wakati huo. Historia inaonesha kuwa wakati waarabu wa kikurayshi walipokuwa wakikusanya bishaa zao ili kwenda kuziuza maeneo ya Syria na Yemen, msafara wa Khadija ulikuwa ni sawa misafara ya maquraysh wote ikusanywe pamoja. Hii inaonesha alikuwa ni tajiri zaidi wakati huo.

Tofauti na biashara Hadija alifahamika kuwa ni katika wanawake wazuri na wenye akili zaidi kuliko wanawake wote wa Makkah wakati huo. Watu wenye vyeo vyao na utajiri walikuwa wakienda kutoa posa lakini walikuwa wakirudi patupu. Hadija alikuwa ni katika wanawake waliokuwa wakiheshimika sana. Alikuwa ni mkarimu na mwenye kusaidia sana masikini na wasio na kitu. Na aliendeleza tabia hii hata baada ya kuolewa na Muhammad.

Hadija alipewa majina mbalimbali kutokana na cheo chake mbele za watu wa Makkah. Waarabu walimuita Ameerat-Quraysh (princess of quraysh) pia walimuita Khadija al-Kubra (Khadija the great). ijapokuwa Makkah wakati huo watu walikuwa wakiabudu masanamu lakini Khadija katu hajapatapo kusujudia masanamu.

Ijapokuwa Khadija alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa lakini hajapatapo kusafiri na biashara zake ili kwenda kuuza. Alikuwa akiajiri wanaume waendde kumfanyia biashara na anawalipa kwa makubaliano maalumu. Mwaka 595 Khadija alihitaji mtu wa kwenda kumfanyia biashara zake maeneo ya Syria. Kwa kuwa alipatapo kusikia sifa za Muhammad kuwa ni Mwaminifu na ni mkweli hivyo akamtafuta na wakakubaliana kuwa atamlipa zaidi kuliko ambavyo anawalipa watu wengine.

Nafisa alikuwa ni rafiki wa karibu sana wa Khadija, hata wakati Khadija alipotaka kuolewa na Muhammad alimtumia nafisa ili aende kuzungumzana Muhammad kuhusu jambo hili. Tumeshazungumza khabari hii hapo kurasa za nyuma. Mjomba wake Khadija alifahamika kwa jina la Waraqa bin Nawfal. Huyu alikuwa ni mkristo na ni mchamungu na alitambua vyema ujio wa Mtume wa Mwisho. Hata wakati watu wote wa Makkah hawakujuwa kuwa Muhammad atakujakuwa Mtume Waraqa alishatambua jambo hili. Waraqa ndiye aliyesimamia ndoa ya Khadija na Muhammad. Dada yake alifahamika kwa jina la Hala bint Khuwayld.

Bi Khadija anajulikana kwa kuwa ndiye Mtu wa kwanza kutamka shahada ya kuamini utume wa Mtume Muhammad s.a.w. Khadija alitumia mali zake katika kuendeleza harakati za dini mpaka alipofariki mwaka wa 10 baada ya utume (yaani Miladiya) ni sawa na 620 katika mji wa Makkah. Khadija alifariki akiwa na umri wa miaka 65. na alizikwa sehemu iitwayo jannat al-Muโ€™allah mjini Makkah. Bi kahdija alishapataga kuolewa na โ€˜Atiq bin โ€˜Aidh Al-Makhzum na Abu Hala Malak ibn Nabash. Na alizaaa pamoja na waume wote hao watoto. Alizaa na Mtume Muhammad (s.a.w) watoto sita.


                   

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 3709


Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰5 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa
Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu
Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUT(A.S) NA WATU WA SODOMA NA GOMORA
Mtume Lut(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII AYUBU
Soma Zaidi...

Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao
Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Fat-h Makkah (Kukombolewa Makkah) baada ya mkataba wa hudaibiya
Fat-h Makkah (Kukombolewa Makkah). Soma Zaidi...

Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake
Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a. Soma Zaidi...

Imam Nasai na kitabu cha Sunan
Soma Zaidi...

KAZI ALIZOFANYA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) KABLA YA UTUME
KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S. Soma Zaidi...

Kwanini mwanadamu hawezi kuunda dini sahihi
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...