MKATABA WA AL-FUDHUL
Baada ya vita hivi viongozi wa pande mbili hizi waliamuwa wakae chini na wakubaliane kuweka kanun i na utaratibu utakaozuia kutotokea uonevu kama huuu tena. Na hii ni kuwa maeneo mengi ya waarabu enzi hizo yalikuwa na utaratibu kama huu wa kuweza kusaidiana na kuzuia uonezu na unyanganyi wa haki. Makataba huu ulikuwa na lengo la kuwasaidia watu wanyonge ambao hawana urafiki na mahusiano na watu wenyenguvu, madaraka ama uwezo wa kipesa.

Hivyo lengo kuu la kiapo au mkataba huu ilikuwa kulinda haki za wanyonge, kuzuia dhulma na uonevu. Kuwapa haki watu wanaostahiki kupewa haki bila ya kujali wapi wametoka, ni nani ndugu zao au wanauwezo gani. Makataba huu ulifanyika kwenye nyumba ya mzee mwenye heshima,na mwenye umri aliyefahamika kwa jina la Abdallah bin Jad’an. Walohudhuria kwenye mkutano huu ni wawakilishi kutoka kabila la Banu hashim, Banu Al-Muttalib, Asad bin Abdul ‘Uzza, Zahran bin Kilab pamoja na Taim bin Murra.

Baada ya makubaliano yao ya kujenga amani kati yao wenyewe na wageni wao wanaokuja Makkah walikwenda kwenye Al-Ka’abah na kufanya kiapo. Kiapo chao ni kuyatekeleza walokubaliana kuwa watampa kila mtu haki yake na watapigana na yeyote ambaye atadhulumu na kumsaidia atakaye dhulumiwa. Watapigana na yeyote atakayevunja makubaliano haya mpaka haki ipatuikane. Walifanya kiapo ndani ya al-ka’aba mbele ya kiwe jeusi.

Miongoni mwa walohudhuria mkutano huu kutoka upande wa maquraysh ni Mtume s.a.w. na baada ya kupewa utume Mtume (a.s.w) alisema: “nilishuhudia (mkutano, makubaliano mkataba) kwenye nyumba ya Abdallah bin Jad’an, mkutano ninaoupenda kuliko ngamia mwekundu, na lau ningeliitwa tena kwenye mkutano kama huu hakika ningehudhuri”. Maneno haya yanathibitisha kuwa mkutano huu uliridhiwa na Allah. Hizi pia zilikuwa ni katika vitangulizi vya kuja kwa mtume wa mwisho.

Na inasemekana kuwa jimbuko na wao kukutana ni kuwa alitokea mfanyabiashara mmoja kutoka katika kabila la Zubaid alikuja Makkah kufanya biashara. Hivyo akamuuzia Al-‘As bin Wa’il As-Sahmy baadhi ya bidhaa zake. Baadaye Al-As akakataa kumlipa mtu huyu. Hivyo mfanyabiashara akawa anaomba msaada kwa Maquraysh waweze kumsaidia ili apate haki yake, lakini hakuna ambaye alimjali.