KAZI ALIZOKUWA AKIFANYA MUHAMMAD (S.A.W) ZA KUMPATIA RIZKI
Muhammad (s.a.w) hakuwaga na shughuli maalumu ya kuweza kumpatika kazi. Kama ilivyokuwa ni desturi ya mitume kuchunga mifugo kama mbuzi na kondoo hivyo hivyo kijana Muhammad (s.a.s) alikuwa akifanya kazi hii. Muhammad (s.a.s) alikuwa akichunga mifugo ya bani Sa’ad kwa malipo maalum.

Pia kijana Muhammad (s.a.s) alikuwa ni mfanya biashara. Aliweza kupata uzoefu wa biashara kutoka kwa Baba yake mdogo Abu Tallib ambaye pia alikuwa ni mfanya biashara. Alipokuwa na umri wa miaka 25 alisafiri kuwenda Sham (Syria) kwa ajili ya kufanya biashara. Na itambulike kuwa wakazi wa Makwa wakati huo walikuwa ni wafanya biashara wakubwa sana. Matajiri wengi wa Makkah walikuwa wakitegemea biasha. Kutokana na uadilifu, uaminifu na ukweli alokuwa nao kijana Muhammad (s.a.s) Bi Khadija alimtaka akamuuzie biashara zake Syria.

Bi khadija alikuwa ni katika wanawake wafanyabiashara wakubwa Mjini Mkkah. Alikuwa akiajiri wanaume kwa ajili yakufanyiwa biashara zake. Aliposikia sifa za Muhammad (s.a.s) alivutiwa kufanyabiashara nae. Hivyo akazungumza nae na awalikubaliana kuwa atamlipa zaidi kuliko wenzie. Akamtuma Muhammad (s.a.s) akiwa na mfanyakazi wa bi Khadija aitwaye Maisarah, aliwatuma waende kufanya biashara Syria. Basi Muhammad (s.a.s) alikubali ombi aba safari akaelekea kwenda Sham. Na katika safari hii Bi Khadija aliona miujiza mikubwa sana kwa Muhammad (s.a.s).