MTUME MUHAMMAD (S.A.W)ANAKUTANA NA BAHIRA (MTAWA WA KIYAHUDI)

KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara.

MTUME MUHAMMAD (S.A.W)ANAKUTANA NA BAHIRA (MTAWA WA KIYAHUDI)


KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDI
Mzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Sikumoja wakati Mtume alipokuwa na umri wa miaka kumna mbili (12) alitoka yeye na kijana wake kuelekea Sham (Syria) kwa ajili ya kufanya biashra. Basi walipofika sehemu inayoitwa Busra walikutana na kuhani mmoja wa kiyahudi aliyeitwa Bahira na inasemekana jina lake halisi ni George (Joji kwa matamshi ya kiswahili). Mtu huyu aliwaonesha ukaribu mkubwa sana, a katu hajawahi kuonesha ukarimu huu kwao watu hawa kwani walikuwa ni wageni kwake.

Bahira aliushika mkono wa Mtume na akasema 'huyu ndiye kiongozi wa watu wote, Allah atamtuma kwa kumpa ujumbe ambao utakuwa ni rehma kwa viumbe wote' hapa mzee Abu Talib akamuuliza 'umejuaje jambo hili' Mzee huyu akajibu kwa kumwambia 'mlipokuwa mnakuja alipotokea upade wa Aqabah niliona miti na majabali vyote vinamsujudia (yaani vinampa heshima) na huwa vitu hivi havifanyi hivi ila kwa mitume tu. Pia naweza kumjuwa kwa kuwa ana mhuri wa mitume chini ya bega lake kama tunda la tofaha (epo) yote haya tumeyasoma kwenye vitabu vya dini yetu'

Baada ya mazungumzo Bahira akamwambia mzee Abu Talib amrudishe kijana Makkah kwani Bahira alihofia kuwa watu wa huko wendako huenda wakamgunduwa kuwa huyu atakujakuwa mtume wa mwisho hivyo wakamfanyia hasadi na kumuua. Kwani Mayahudi walikuwa wakihubiri kuhusu Mtume wa Mwisho lakini walitarajia kuwa atatokea miongoni mwa kabila lao hivyo wakitambua kuwa Mtume wa Mwisho ni Muarabu wanaweza kumuuwa kama walivyowauwa mitume wao huko nyuma. Basi mzee Abu talib alitii na kumrudisha kijana wake Makkah.

Wanazuoni wa sirah wanazungumza maelezo mengi kuhusu habari hii ya Bahirah na Kijana Muhammad. Wapo wanaoeleza kuwa Bahira baada ya kutamka maneno ya kuwa huyu kijana atakujakuwa ni mtume alitaka kujiridhisha zaidi hivyo akaanza mazungumzo na kijana ili aweze kubaini mengi zaidi. Basi katika mazungumzo yake Bahira alisema 'Nakuapia kwa Mungu Lata na Uzza' bahira alitambuwa kuwa Lata na Uzza ni miungu wa washirikina wa Makkah hivyo Mtume hatavumilia maneno haya. Basi kijana Muhammad aliposikia maneno yake akamwambia 'Usitaje Lata na Uza mbele yangu, ninawachukia' Kufika hapa Bahira akawa amejiridhisha kabisa kuwa huyu ndiye Mtume wa Mwisho.

Katika masimulizi mengine ni kuwa Bahira alikaribisha msafara mmoja wa kibiashara kwenye tafrija yake. Msafara huu ndio ulikuwa msafara wa Abu Talib na wenzie. Basi bahira akawaambia watu wote waingie ndani kwenye tafrija isipokuwa hyuy mtoto (Muhammad) abakie nje ili kulinda mizigo. Basi wakati tafrija inaendelea bahira akaanza kuona miujiza kama Kusujudi kwa mitu (kutoa heshima) na kufunikwa na mawingu wakati kwa ajili ya kivuli. Hapo ndipo Bahira akatambua kuwa huyu ni Mtume.

Na hapo ndipo alipomsahuri mzee Abu talib kuwa kijana huyu asiendenae huko Syria kwani mayahudi wakimjuwa watamuua. Mzee abu Talib alitii ushauri huu hivyo akauza bidhaa zake paleple kwa bei iliyo nafuu ili aweze kurudi zake Makkah. Abu Talib safari yake ya biashara ikaishia palepale bila ya kufika Syria.


                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 213

Post zifazofanana:-

Mipaka katika kumtii mzazi, na mambo yasiyopasa kumtii mzazi
Soma Zaidi...

MINYOO NA HATARI YEKE KWA AFYA: kuwashwa matako, kupungua uzito, kukosa hamu ya kula, kupungua damu
MINYOO NA HATARI YEKE KWA AFYA Utangulizi Karibu tena kwenye makala zetu za afya. Soma Zaidi...

SHARTI ZA KUWAJIBIKA KWA ZAKA
Soma Zaidi...

Dalili za gonorrhea - gonoria
Jifunze dalili za gonorrhea na namna inavyoambukiza, zipi athari za gonori kwa wanawae na wanaume Soma Zaidi...

maktaba
Soma Zaidi...

dondoo za afya
Basi tambua haya;- 1. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Pensheni
Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Soma Zaidi...

Kwa mjamzito kuumia wakati wa tendo la ndoa tatizo linaweza kuwa ni nini?
Soma Zaidi...

Uthibitisho kuwa quran ni maneno ya Allah kutokana na Historia (Hadith)
Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Kwa nini lengo la kutoa zaka halifikiwi na watoaji zaka?
Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu? Soma Zaidi...