Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
SURA YATISA
HUKUMU ZA WAQFU AL-IBTIDAI
l-Waqfu Wal-Ibtidaai โ Kisimamo Na Kianzio
Msomaji si kwamba muda wote atakuwa anasoma bali, wakati mwingine anapumzika, au anasimama kidogo kumeza mate au kupumua ana atakata kabisa kusoma. Hivyo hapa kuna kauli tatu ambazo inatupasa tuzijue kabla ya kuenddelea. Kauli hizo ni;-
1.Al-waqfu: maana yake ni kisimamo nako ni kukata kusoma kwa muda wa kawaida kwa ajili ya kuvuta pumzi huku msomaji akiwa na nia ya kuendelea kusoma.
2.Al-sakt:maana yake ni kipumziko nako ni kupumzika kwa muda kwa kiasi cha haraka mbili huku msomaji akiwa na nia ya kuendelea kusoma.
3.Al-qatwโu;maana yake ni ukataji nako ni kusimama kusoma kwa lengo la kumaliza kusoma. Hapa inabidi mtu amalize kusoma kwake mwishoni mwa aya au sura. Na inatakikana pindi anapotaka kuendelea kusoma aanze na istiโadha
ALAMA ZA WAQFU KATIKA QURAN:
1.aAlama hii(ุตูู) inamaanisha inajuzu kuunganisha.
Yaani pindi msomaji anapokuta alama hii anaweza kuunganisha maneno hayo, yaani neno la nyuma na maneno yanayofata. Hivyo hapa msomaji ana hiyari ima kuunganisha au kusimama (kufanya waqfu).
2.Alama hii (ููู) inamaanisha inajuzu kusimama.
Yaani pindi msomaji anapokuta alama hii atakuwa na hiyari ya kusimama.
3.Alama hii (ุฌ) inamaanisha inajuzu kusimama ila kwa ufupi. Yaani msomaji anapokutana na alama hii ataweza kusimama hapa, ila usimamaji wake usiwe mrefu.
4.Alama hii (ู
) inamaanisha kusimama kwa lazima. Yaani msomaji anapokutana na alama hii kusimama kwake ni kwa lazima.
Alama hii (ูุง) inamaanisha hairuhusiwi kusimama sehemu hii. Hii inamaanisha msomaji hatakiwi kusimama pindi anapokutana na alama hii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Sura hii inazungumzia kuhusu hali ya Abulahab namke wake wakiwa kama Watu waovu. Ni moja katika sura ambazo zilishuka mwanzoni toka Mtume alipoamrishwa kulingana dini kwa uwazi.
Soma Zaidi...SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina iโrab ( ู ู).
Soma Zaidi...Sura hii imetermka Makkah na ina aya 11. Sura hii ni moja ya sura ambazo zimeshuka mwanzoni wakati ambapo Mtume ameanza kazi ya utume.
Soma Zaidi...Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.
Soma Zaidi...Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto.
Soma Zaidi...