SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( مْ).
SURA YA NNE
HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA
HUKUMU ZA MIYM SAKINA:
Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( مْ). Wataalamu wa tajweed wanataja hukuma zifuatazo kuhusu mym yenye sakina;-
i. إِدْغامُ الشَّفَ وِي Idghaam Ash-Shafawy
Hii hutokea pale ambapo miym yenye sakina ikukutana na miym yenye i’rabu yaani fataha, kasri au dhuma. Na inatakiwa mym yenye sakina ianze mwanzi kisha ifuatie mym yenye i’rabu, hivyo mym hii ya kwanza itaingizwa kwenye mym ya pili na kuwekwa shada ya pili na kusomwa kwa ghunnnah. Aina hii ya idgham pia huitwa إَدْغَامُ الْمُتَماثِلَيْن (Idghaamul-mutamaathilayni).
ii. إِخْ فَ اء الشَّفَ وِي Ikhfaaush-Shafawiy
Hukumu hii itapatikana pindi miym saakinah ( مْ) na herufi ya . ب, hivyo hapa mym sakina itafanyiwa ikhfaau kwenye ب, yaani mym ifafichwa kwa ghunnah.
iii. إظْهارُ الشَّفَ وي Idhwhaar Ash-Shafawiy
Hukumu hii hutokea wakati mym sakina inapokutana na herufi zozote isipokuwa م na ب, hivyoo hapa mym sakina itadhihirishwa yaani itatamkwa kama ilivyo pamoja na kuitenga na herufi inayofata bila ya kuleta ghunnah.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu srat al fatiha, faida zake na maudhui zake
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake.
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Kusoma Qur'an kuna faida kubwa kwa Muislamu, kwanza kunampatia thawabu, kunatoa nuru maisha yake, mwili wake na kumlinda na mashetani na watu wabaya. Quran ni dawa na pozo kwa magonjwa. Thawabu za Qur-an hulipwa kwa kila herufi. Quran pia huja kutet
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha fadhila na faida za kusoma surat al Imran
Soma Zaidi...Hapa utajifunza usomaji wa Quran pindi utakapokuta nuni yenyebsakina au tanwin
Soma Zaidi...