Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
4.TABIA
Tabia za watu pia zinaeza kuwa ni sababu ya kupata maradhi na kuathiri afya. Watu wamekuwa wakikulia katika koo, familia na kabila mbalibali ambapo wanajifunza tabia tofautitofauti. Tabia hizi kama hazitakuwa katika hali inayotakiwa zinaweaa kusababisga kupata maradhi
Nitoe mfano mzuri kuhusu maradhi ya fangasi sehemu za siri. Fangasi hawa wanafurahia sana mazigira yenye majimaji. Mara nyingi usafi wa nguo za ndani na mwili kwa ujumla hususan sehemu zile umaweza kuwa sababu ya kuendelea kuwalea wadudu hawa. Tabia ya kuvaa nguo mbichi hususani zile za ndni inaweza kuendelea kuwalea fangasi hawa.
Tabia ya kula mara kwa mara inaweza kusababisha kupata kitambi. Mtu akiwa anakula mara kwa mara bila ya kufanya mazoezi anaweza kupata tatizo la kuzidi kwa uzito. Tatizo hili linaweza kuathiri mwili kushindwa kuzalisha homoni za insulin kwa kiwango kinachotakiwa na hatimaye kupata kisukari.
Tabia ya kuchelewa kualal yaani kukosa muda mzuri wa kulala inaweza kuwa sababu ya kupata matatizo ya kiafya. Mwili unahitaji muda wa kutosha wa kulala ili uweze kurekebisha mwili ndani ya muda huo. Mwili unahitaji kupumzika pia.
Tabia ya kukaana misongo ya mawazo na kupenda kukasirika na kukaa na vinyongo. Hii ni hatari sana ka afya ya mtu kisaikolojia na kimwili pia. Misongo ya mawazo inaweza kuwa sababu nzuri ya kupata maradhi kama vidonda ya tumbo. Maumivu ya kichwa na tumbo pia huweza kuletwa na misongo ya mawazo
Umeionaje Makala hii.. ?
Kama unasumbuliwana tumbo upande wa kulia, kushoto, kitomvuni ama kuoande wa kuliavkwachini, basi muulizaji huyu atakupa uelewa.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kukosa usingizi. Usingizi ni ugonjwa unaoendelea ambao unaweza kufanya iwe vigumu kusinzia, vigumu kubaki usingizini au vyote viwili, licha ya fursa ya kupata usingizi wa kutosha.Ukiwa na kukosa usi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi utumiaji wa pombe na sigara pamoja na madawa katika jamii.
Soma Zaidi...Kujiepusha na Vishawishi vya ZinaaKatika macho ya sheria kitendo cha zinaa kinahesabiwa pale wanapokutana kimwili mwanamume na mwanamke nje ya ndoa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya mambo ya kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu kauli mbalimbali za wataalamu wa afya
Soma Zaidi...