Safari ya damu kwa Kila siku


image


Posti hii inakwenda kukuletea mfumo wa damu mwilini na safari zake za Kila siku


SAFARI YA DAMU KWA KILA SIKU.

 

picDamu ni tishu iliyopo katika hali ya kimiminika. Bila ya damu mwanadamu hawezi kuishi. Moyo ndio kiungo kikuu wenye mwili chenye kazi ya kuisambaza damu mwili mzima. Ukubwa wa kiungo hichi hufanana na ngumi. Moyo husafirisha damu kwenye mishipa inayokadiriwa kuwa na urefu wa kilomita elfu tisini na saba (97) na hii hufanyika ndani ya sekunde 20 tu.pic

 

Damu imeundwa kwa seli hai nyekundu za damu, seli hai nyeupe za damu, plasma, maji na seli sahani. Kila moja kati ya hizi ina kazi yake maalumu. Katika makala hii fupi tutaona vitu hivi kwa ufupi tu. Pia itambulike kuwa kuna viumbe hawana damu kama minyoo na baadhi ya samaki. Na hii ni kutokana na jinsi maumbile yao yalivyo. Asilimia 7% ya mwili wa binadamu ni damu na mtu mzima ana damu kuanzia lita 3.7 mapaka lita 5.6.

 

Seli nyekunsu za damu (red blood cell), hizi kitaalamu huitwa erythrocytes na hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa yaani bone marrow. Kwa wastani seli hizi zinaweza kuishi kwa muda wa siku 120 tu baada ya kutengenezwa. Asilimia [email protected] ya damu ni seli hizi na ndio ambazo zinaipa damu rangi nyekundu. Seli zina protini na haemoglobin (chembechembe nyekundu) na hizi ndio huipa rangi nyekundu. Kazi ya seli hizi ni kubeba heya ya oxygeni kutoka kwenye mapafu na kuipeleka kwenye moyo ili isambazwe zaidi mwilini. Ka kutoa hewa ya kabondaioksaidi kutoka kwenye moyo na kuipelekwa kwenye mapafu ili itolewe nje. Pia hubeba viinilishe (nutrients) kupeleka sehemu zingine za mwili.

 

Seli n yeupe za damu (white blood cell) kwa jina la kitaalamu huit wa leukocytes. Kazi kubwa ya seli hizi ni kupambana na maambukizi na wadudu wa baya wanaoshambulia mwili. Seli hizi zinaweza kuishi kuanzia siku moja mpaka mwezi mmoja tu baada ya kutengenezwa. Pia hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa. Seli hizi zipo aina nyingi, kuna ambazo hupambana na kula bakteria na wadudu wengine wavamizi mwilini, kuna nyingine zinatoa antibodies kwa ajili ya kusaidia kupambana.

 

Seli sahani (platelets) kitaalamu huitwa thrombocytes pia hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa. Sinaishi siku sita tu baada ya kutengenezwa. Kazi yao kubwa ni kugandisha damu pindi kunapokuwa na jeraha. Plasma sio seli ni maji ya njano ambayo husaidia damu huogelea vizuri kupita kwenye mirija ya damu. Asilimia 90 ya plasma ni maji, ila pia ina madimi, vitamin na viinilishe (nutrients)



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    2 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    3 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani offline    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Muda wa kuchaji simu yako
Posti hii itakwenda kukujuza juu ya kuda mzuri wa kuchaji simu yako Soma Zaidi...

image Nini chanzo cha tatizo la computer au simu yako
Posti hii inakwenda kukupa elimu kuhusu chanzo cha tatizo la computer au simu yako Soma Zaidi...

image CONTACT US
Soma Zaidi...

image WIKIBONGO NI NINI?.
Bila shaka umekuwa ukijiuliza sana kuhusu wiki bongo hasa ni kitu gani. Hapa upo mahala sahihi. nitakwenda kukueleza hasa ni nini maana ya hili neno "wikibongo". Soma Zaidi...

image Safari ya damu kwa Kila siku
Posti hii inakwenda kukuletea mfumo wa damu mwilini na safari zake za Kila siku Soma Zaidi...

image Cheetah
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama cheetah Soma Zaidi...

image Jinsi ya kutuma sms ndefu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kutuma sms ndefu Soma Zaidi...

image Kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kulinda account yako ya Facebook dhidi ya waharifu wa kimtandao Soma Zaidi...

image Mbu (mosquito)
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mdudu mbu Soma Zaidi...

image OUR PRIVACY POLICIES.
Soma Zaidi...