Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
6.VIDONDA VYA TUMBO
Ni vidonda vinavyotokea katika ukuta wa tumbo. Vidonda hivi tumezoea kuviita vidonda vya tumbo ila hapa nitataja kitaalamu kuwa vidonda hivi hufahamika kama peptic ulcers. Vidonda hivi hutokea kutokana na mashambulizi ya bakteria wanaoitwa H.pylori au kulika kwa ukuta wa tumbo kutokanana na athari za tindikali zilizopo tumboni (stomach acids) kama vile tindikali ya hydrocloric yaani hydrocloric acid. Kwa wakati tulio nao hili ni tatizo la kawaida maana limewapata watu wengi na halisabababishi vifo vya watu wengi kama maaradhi ya saratani na kisukari.
Vidonda hivi vimegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni:-
1.gastric ulcers hivi hutokea ndani ya tumbo la chakula
2.Esophageal ulcers hivi hutokea ndani ya esophagus. Hii ni sehemu inayounganisha kati ya koo la chakula na tumbo la chakula.
3.Duodenal ulcers hivi hutokea kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayoitwa duodenum
Sababu za kutokea vidonda hivi
1.mashambulizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori (H.pylori). Hawa bakteria wanaweza kusabababisha mashambulizi na kuathiri sehemu tajwa hapo juuu na kusababisha vidonda hivi.
2.Matumizi ya baadhi ya aina za madawa mara kwa mara. Kuna aina za dawa ambazo kwa sasa zimepigiwa marufuku lakini hutumika kwa njia za panya. Madawa haya huweza kusababisha vidonda hivi kwa mfano aspirin, ibuprofen na naproxene n.k
3.Uvutaji wa sigara
4.Kunywa pombe kupita kiasi
5.Athari ya miozi
6.Saratani ya tumbo
7.Misongo ya mawazo (stress)
8.Kukaa na njaa kwa muda mrefu.
DALILI ZA VIDONDA HIVI.
Dalili hizi hutofautiana kulingana na aina za vidonda. Ila hapa nitaorodhesha baadhi ambazo ni kawaida kwa vidonda hivi.
1.maumivu ya tumbo kutokea kitomvuni mpaka kifuani
2.Kukosa hamu ya kula
3.Kutoka na damu na kupata choo cheusi sana
4.Kupungua uzito bila sababu
5.Kutapika
6.Maumivu ya kifua
7.Tumbo kujaa.
8.Kuchoka ana
KUTHIBITI VIDONDA HIVI
1.wacha au punguza kunywa pombe
2.Usichanganye vilevi na madawa mengine
3.Punguza kutumia madawa aina ya aspirin n.k
4.Osha mikono yako mara kwa mara kuepuka maambukizi ya bakteria
5.Punguza misongo ya mawazo
6.Kula katika muda uleule.
Vidonda vya tumbo vinatibika bila ya shaka. Mgonjwa amuone mtaalamu wa afya na atimize masharti na ale dozi kulingana na kipimo husika. Pia kama sehemu imeharibika sana mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji. Kwa ambaye aansumbuliwa na vidonda hivi anashauriwa pia anywe maziwa.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 281
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 kitabu cha Simulizi
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Kitau cha Fiqh
KITABU CHA AFYA (kisukari, saratani, vidonda vya tumbo, HIV na UKIMWI) DALILI NA CHANZO
Soma Zaidi...
TAHADHARI KWENYE VYAKULA ILI KULINDA AFYA YAKO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Kwanini najihisi mchovu alafu tumboni kunavitu navihisi vinacheza sielewi
Habari yako Dokta. Soma Zaidi...
AFYA NA MAGONJWA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
DONDOO 100 ZA AFYA
Pata dondoo 100 za Afya Soma Zaidi...
Dondoo za afya 61-80
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dondoo za afya Soma Zaidi...
dondoo 100 za afya
Soma Zaidi...
Kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya mambo ya kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari Soma Zaidi...
ilinde Afya yako
Hiki ni kitabu kilichosheheni masomo zaidi kuhusu Afya yako, vyakula pamoja na maradhi sugu. Soma Zaidi...
ZIJUWE FIGO, KAZI ZA FIGO NA NAMNA YA KULINDA FIGO DHIDI YA MARADHI
Je unatambuwa namna fgo inavyofanya kazi, unazijuwa kazikuu za fogo mwilini, na je unajuwa namna ya kujilinda dhidi ya maradhi ya figo?. Basi makala hii itakujuza kuhusu masomo haya1 Soma Zaidi...
dondoo za afya
Basi tambua haya;- 1. Soma Zaidi...
NAMNA AMBAZO MWILI HUPAMBANA NA MARADHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...