picha

CHUKUWA TAHADHARI HIZI KWENYE MAZINGIRA ILI KULINDA AFYA YAKO

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

CHUKUWA TAHADHARI HIZI KWENYE MAZINGIRA ILI KULINDA AFYA YAKO

2.TAHADHARI KWENYE MAZINGIRA
Kama tulivyoona hapo juu, mazingira yetu ni sababu tosha ya kuathiri ubora wa afya zetu. Hivyo mtu ahakikishe sikuzote anaishi katika mazingira salama na safi. Wataalamu wa afya wanatueleza kusafisha mazingira yetu ya ilasiku ili tuweze kukabilia na na wadudu hatara.

Hakikisha hewa unayoipata ni safi na salama. Futa mavumbi ndani ya nyumba na nguo za kujifunika ziwe safi, kwa namna hii ni rahisi kukabilia na na mafua. Epuka moshi kutoka viwandani, pia usilale ukiwa na jiko la mkaa linalowaka na ikawa madirisha na milango umefunga. Unaweza kupata tatizo la kukosa oxkyjeni na kufariki dunia. Kaa mbali na wavuta sigara kwani hewa yao inaweza kukuathiri na wewe pia. Jambo la msingi hapa ni kuchukua tahadhari dhidi ya hewa ambayo tunaipata kwenye mazingira hetu.

Hakikisha unafyeka na kupunguza nyasi zilizo karibu na wewe. Fukia madimbwi na majimaji yoyote yalotuwama hata kama yapo kwenye kifuniko cha soda kwani hayo ni machache lakini mamia ya mbu yanaweza kuzaliana hapo. Mashimo ya kutupia taka yawe mbali kidogo na nyumba na kuwepo utaratibu wa kuchoma moto mashimo hayo bada ya muda. Usafi wa mazingira unaweza kuwa njia tosha ya kuanza harakati za kukabiliana na malaria na kipindupindu.

Watu wahakikishe wanakunywa maji safi na salama pamoja na kula vyakula ambavyo vimehifadhiwa kwa usalama. Usafi wa maji unaweza kuwa njia ya kupambana na typhod (taifodi) na maradhi mengine ya tumbo. Kuwepo na utaratibu wa kuyatibu maji kama yamepatikana sehemu ambazo sio salama na safi. Maji yanaweza kutibiwa kwa njia za kisasa kama kuweka madawa. Lakini pia unaweza kutumia njia ya kuyachemsha na kuyachuja na kuyatumia.

Sikuzote hakikisha unaishi katika mazingira rafiki na afya yako. Watu ambao tayari wanamaambukizi ya maradhi maalumu wanatakiwa waishi katika mazingira ambayo ni rafiki na hali zao.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 659

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 ai web app     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Ijue timu ya upasuaji

Posti hii inahusu timu ya upasuaji hii ni timu ambayo inahusika katika chumba cha upasuaji, kwa sababu ya kutunza usafi na usalama chumba hiki kinapaswa juwa na timu ya watu wanne na walio na elimu kuhusu kazi hiyo.

Soma Zaidi...
ZIJUWE FIGO, KAZI ZA FIGO NA NAMNA YA KULINDA FIGO DHIDI YA MARADHI

Je unatambuwa namna fgo inavyofanya kazi, unazijuwa kazikuu za fogo mwilini, na je unajuwa namna ya kujilinda dhidi ya maradhi ya figo?. Basi makala hii itakujuza kuhusu masomo haya1

Soma Zaidi...