SURA YA NNE
HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA
HUKUMU ZA MIYM SAKINA:
Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( مْ). Wataalamu wa tajweed wanataja hukuma zifuatazo kuhusu mym yenye sakina;-
i. إِدْغامُ الشَّفَ وِي Idghaam Ash-Shafawy
Hii hutokea pale ambapo miym yenye sakina ikukutana na miym yenye i’rabu yaani fataha, kasri au dhuma. Na inatakiwa mym yenye sakina ianze mwanzi kisha ifuatie mym yenye i’rabu, hivyo mym hii ya kwanza itaingizwa kwenye mym ya pili na kuwekwa shada ya pili na kusomwa kwa ghunnnah. Aina hii ya idgham pia huitwa إَدْغَامُ الْمُتَماثِلَيْن (Idghaamul-mutamaathilayni).
ii. إِخْ فَ اء الشَّفَ وِي Ikhfaaush-Shafawiy
Hukumu hii itapatikana pindi miym saakinah ( مْ) na herufi ya . ب, hivyo hapa mym sakina itafanyiwa ikhfaau kwenye ب, yaani mym ifafichwa kwa ghunnah.
iii. إظْهارُ الشَّفَ وي Idhwhaar Ash-Shafawiy
Hukumu hii hutokea wakati mym sakina inapokutana na herufi zozote isipokuwa م na ب, hivyoo hapa mym sakina itadhihirishwa yaani itatamkwa kama ilivyo pamoja na kuitenga na herufi inayofata bila ya kuleta ghunnah.